Trump asema Iran ‘inaogopa’ kukubali kuwa kuna majadiliano huku Tehran ikikanusha ripoti hizo

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 26, 2026 06:07 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader
.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema katika mahojiano ya televisheni ya taifa ya Iran kwamba kwa “siku kadhaa” Marekani “imeanza kutuma ujumbe mbalimbali kupitia wapatanishi tofauti”.

Lakini amesema ukweli kwamba jumbe hizi “ziliwasilishwa kupitia nchi rafiki”, na kwamba Iran ilikuwa ikijibu kwa kusema “misimamo yao na kutoa maonyo”, “sio mazungumzo wala majadiliano, wala chochote cha aina hiyo”.

Araghchi pia amesema kwamba sera ya Iran kwa sasa ni kuendelea “kujitetea”, na “hawana nia ya kujadiliana kwa sasa”.

Anaongeza kwamba, “Hii ni vita vya Israeli na watu wa eneo hilo na watu wa Marekani wanalipa gharama yake.”

TANGAZO

https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQu3lFleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFDaHJMNDVrZUx6VXRNY3NUc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHj3J-oZN3HqbjD7V9XaumO03MtdAKWqx7SIqWHSUUr8BWukkOEEpeLne6xWt_aem_1WY6FZPnX5UmceUPLC_RAg

Kilichofanyika hivi karibuni kuhusu mazungumzo kati ya Marekani na Iran?

Kilichotokea kufikia sasa:

  • Waziri wa Habari wa Ikulu ya Marekani Karoline Leavitt amesema siku ya Jumatano, Rais Trump amekuwa akishiriki katika “mazungumzo yenye tija” na Iran kwa siku tatu zilizopita.
  • Pia alisema hatua hiyo ilikuwa “imefanyika kwa haraka” na utawala wa Iran ulikuwa unatafuta “njia ya kutokea”
  • Ujumbe huo ni tofauti kabisa na sauti ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi, ambaye baadaye alisema kwamba Iran ” haina nia ya kufanya majadiliano kwa sasa “
  • Alisema ujumbe “umewasilishwa kupitia nchi rafiki”, lakini mabadilishano haya “si mazungumzo wala majadiliano, wala kitu chochote cha aina hiyo”
  • Bila kukata tamaa, Trump anasisitiza kwamba Iran “inajadiliana”, akisema ” wanaogopa kusema hivyo kwa sababu wanafikiri watauawa na watu wao wenyewe”. Aliongeza: “Pia wanaogopa watauawa na sisi”
  • Pia kumekuwa na ripoti zinazokinzana kuhusu mapendekezo ya kukomesha vita. Siku ya Jumatano, kulikuwa na ripoti kwamba Iran ilikuwa imepokea mpango wa vipengele 15 kutoka Marekani kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano.
  • Kwa upande wake, “afisa mwandamizi wa usalama wa kisiasa” wa Iran alinukuliwa na mtangazaji wa serikali Press TV akisema walikuwa na masharti matano ya kukomesha vita, ikiwa ni pamoja na malipo ya “fidia ya vita” na kumaliza vita katika nyanja zote.
  • Wakati huo huo, mapigano yanaendelea – moshi ulionekana ukitoka kwenye kituo cha umeme cha Israeli baada ya kuripotiwa kwa shambulio la kombora la Iran, huku mifumo ya ulinzi wa anga ya Iran ikisikika mjini Tehran.

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Google athibitishwa kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa BBC

.

Aliyekuwa mtendaji mkuu wa Google Matt Brittin amethibitishwa kuwa mkurugenzi mkuu mpya wa BBC.

Rais huyo wa zamani wa kampuni ya Google barani Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika atachukua nafasi ya Tim Davie, ambaye alisema alikuwa akijiuzulu mwezi Novemba kufuatia kesi iliyohusu jinsi hotuba ya Rais wa Marekani Donald Trump ilivyohaririwa.

Mwenyekiti wa BBC Samir Shah alisema Brittin, ambaye aliondoka Google mwaka wa 2025 baada ya miaka 18, “analeta uzoefu wa kipekee BBC wa kuongoza shirika la ngazi ya juu na tata sana kupitia mabadiliko”.

Brittin, mwenye umri wa miaka 57, alisema “nina hamu sana kuanza kazi hii”, akielezea kama “wakati halisi wa hatari, lakini pia fursa yenyewe”.

Biashara ya utumwa ni uhalifu dhidi ya ubinaadamu

Waaafrika waliosafirishwa Marekani kutokana na biashara ya utumwaPicha: Glasshouse Images/picture alliance

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linalotambua kuwa biashara ya utumwa dhidi ya Waafrika kuwa ni “uhalifu mbaya zaidi dhidi ya ubinadamu.”

Azimio hilo lililopendekezwa na Ghana lilitaka biashara haramu ya utumwa wa kuvuka bahari ya Atlantiki kutambuliwa kama uhalifu mbaya zaidi katika historia ya binadamu licha ya upinzani mkali kutoka Ulaya na Marekani.  Pia Umoja wa Mataifa umezitaka nchi zilizohusika kulipa fidia kama hatua thabiti katika kurekebisha makosa ya kihistoria.

Baraza hilo lenye wanachama 193 lilipitisha azimio hilo kwa kura 123 za ndio, kura 3 za kupinga ambazo ni za Argentina, Israel na Marekani huku nchi 52 zikijizuia. Uingereza na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya walikuwa miongoni mwa wale waliojizuia.

Azimio hilo pia linahimiza kurejeshwa haraka na bila vikwazo katika nchi za asili kwa vitu vyote vya kitamaduni, ikiwa ni pamoja na kazi za sanaa, vifaa vya makumbusho, hati na kumbukumbu za kitaifa.

WHO: Zaidi ya watu milioni 2 hawana huduma za afya Darfur

Picha ya satelaiti ikionyesha eneo kuliko hospitali huko El FasherPicha: Airbus DS/AP Photo/picture alliance

Zaidi ya watu milioni 2 huko Darfur nchini Sudan wameachwa bila huduma muhimu za afya baada ya shambulio la droni la wiki iliyopita kupelekea kusitishwa kwa shughuli katika hospitali kubwa eneo hilo.

Hayo yameelezwa na Shirika la Afya Duniani WHO na afisa mmoja wa shirika la misaada. Shambulio hilo linalotajwa kuendeshwa na jeshi la Sudan, lilisababisha vifo vya watu 70 na kuharibu  Hospitali ya Al Daein,  ambayo ilikuwa ikiwahudumia watu kote katika jimbo la Darfur Mashariki.

Hayo yakijiri, mapigano yameendelea huku kundi la wanamgambo la RSF likitangaza kuuteka mji wa kimkakati wa Kurmuk, uliopo mpakani mwa Sudan na Ethiopia, huku mamlaka za Chad zikiwazuia wakimbizi wa Sudan kuvuka mpaka wa Al‑Tina, kutokana na sababu za kiusalama.

Zelensky:Marekani inatuwekea masharti kumaliza vita na Urusi

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akiwa katika mkutano kwa njia ya video na viongozi wa UlayaPicha: Ukrainian Presidential Press Service/AFP

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekosoa msimamo wa Marekani na kusema kuwa Washington iko tayari kuipatia Ukraine hakikisho la usalama kwa sharti kwamba Kyiv itakabidhi eneo lote la Donbas kwa Urusi.

Zelensky aliitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumzia kuhusu makubaliano ya amani wakati wa mahojiano na shirika la habari la Reuters na kuongeza kuwa wakati Marekani ikijikita zaidi katika mgogoro wake na Iran, Rais Donald Trump amekuwa akiishinikiza Ukraine kufikia makubaliano ya amani.

Rais huyo wa  Ukraine  amesisitiza kuwa hakikisho thabiti za usalama kutoka kwa washirika wa kimataifa zinahitajika ili kuzuia uwezekano wowote wa Urusi kuishambulia tena Ukraine baada ya kufikiwa kwa makubaliano ya amani.

Waziri Mkuu wa Denmark ajiuzulu kufuatia uchaguzi

Waziri Mkuu wa Dernmark aliyejiuzulu Mette FrederiksenPicha: Sergei Grits/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen amejiuzulu Jumatano na kufungua njia ya kuundwa kwa serikali mpya

Frederiksen anatarajia pia kuiongoza serikalihiyo mpya itakayoundwa kufuatia uchaguzi uliofanywa jana Jumanne ambapo alishindwa kupata wingi.

Katika taarifa, Mfalme Frederik X wa Denmarkamesema amepokea barua hiyo ya kujiuzulu kwa waziri mkuu huyo, siku moja baada ya chama cha Kisoshalisti kuibuka kama chama chenye nguvu zaidi baada ya kupata asilimia 22 ya kura.

Ingawa chama cha Frederiksen bado kinasalia kuwa nguvu kuu, haijawa wazi iwapo atapata mamlaka ya kuunda serikali mpya.

Kulingana na tamaduni za Denmark, baada ya serikali iliyopo kujiuzulu, mfalme huwapokea viongozi wa vyama vyote 12 katika kasri lake, viongozi hao wakielezea yule wanayemuunga mkono kuunda serikali.

Baada ya hapo mfalme huyo ndiye anayeamua ni kiongozi yupi atakayekuwa wa kwnaza kujaribu kuunda serikali ya muungano ambayo haikabiliwi na upinzani mkubwa.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

.

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply