Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Imechapishwa: March 21, 2026 13:19 (EAT)



Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Nathan Howard/REUTERS
Rais wa Marekani Donald Trump amesema utawala wake unafikiria kumaliza operesheni za kijeshi Mashariki ya Kati licha ya nchi hiyo kutangaza kutuma meli zaidi za kivita na jeshi la wanamaji katika eneo hilo.
Taarifa hizo za mkanganyiko za Marekani zinakuja baada ya kupanda tena kwa bei ya mafuta na hivyo kupelekea kushuka kwa soko la hisa la Marekani. Hayo yanafuatiwa pia na tangazo la utawala wa Trump kwamba utaondoa vikwazo dhidi ya mafuta ya Iran yanayopakiwa kwenye meli, hatua inayolenga kukabiliana na ongezeko hilo la bei ya mafuta.
Hata hivyo, vita hivyo havijaonyesha dalili za kupungua licha ya Iran kusherehekea hii leo sikukuu ya Eid el Fitr.
Israel imesema Iran imeendelea kufyatua makombora mapema leo Jumamosi, huku Saudi Arabia ikisema imedungua droni 20 ndani ya saa kadhaa katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo, ambalo ni makazi ya mitambo mikubwa ya mafuta.
Wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema hakukuwa na majeruhi wala uharibifu.
Guterres ashirikiana na Bodi ya Amani kwa ujenzi wa Gaza

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio GuterresPicha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres, amepongeza dhamira ya Bodi ya Amani iliyoanzishwa na rais wa Marekani ili kufadhili na kusimamia mpango wa ujenzi mpya wa Gaza.
Katika mahojiano, Guterres amesema kuna mpango uliofafanuliwa na kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kwamba wanashirikiana kikamilifu na Bodi hiyo ya amani ya Trump chini ya mifumo rasmi iliyowekwa.
Ameongeza kuwa hakuna haja ya bodi hiyo kutanua zaidi malengo yake mbali na ujenzi mpya wa Gaza kwa sababu hiyo sio njia sahihi ya kushughulikia changamoto zilizopo kwa sasa.
Guterres pia amesema wanahitaji kuwa wazi kuhusu sheria za kimataifa na maadili ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa ambayo ni muhimu katika mpango wowote wa amani.
Ruto na Museveni kukutana kuhusu upanuzi wa reli ya kisasa

Treni ya kisasa ya kubeba mizigo nchini KenyaPicha: Reuters/Stringer
Marais wa Kenya na Uganda wanatarajiwa kukutana leo mjini Kisumu karibu na mpaka kati ya nchi hizo mbili, kuzindua ujenzi uliocheleweshwa wa upanuzi wa reli yenye thamani ya mabilioni ya dola iliyojengwa na China.
Reli hiyo inapaswa kufika katika mpaka huo mnamo Juni mwakani ikiwa mpango huo utazingatiwa.
Reli hiyo ya kisasa maarufu kama “SGR” iliyojengwa kutoka mwaka 2013 hadi 2019, inaunganisha bandari ya Kenya ya Mombasa na mji mkuu Nairobi hadi mji wa Naivasha, lakini China ilikataa kutoa mkopo zaidi kabla ya reli hiyo kufikishwa Uganda kama ilivyopangwa.
Siku ya Alhamisi , Rais wa Kenya William Ruto, alizindua ujenzi wa awamu inayofuata katika kaunti ya Narok na kusema mradi huo utachochea ukuaji wa uchumi wa kikanda, na kuifanya Kenya kuwa kitovu kikuu cha usafirishaji Afrika Mashariki na Kati, huku ikizalisha nafasi za ajira na kupunguza msongamano barabarani.
Ukraine yarusha zaidi ya droni 280 kulekea Urusi

Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Ukrainian Presidential Press Service/AFP
Ukraine imevurumisha zaidi ya droni 280 kuelekea Urusi usiku wa kuamkia leo, hii ikiwa moja ya shambulizi kubwa zaidi la droni tangu kuanza kwa vita hivyo.
Katika chapisho kwenye mtandao wa Telegram, Gavana wa eneo la kusini la Rostov Yuri Slyusar, amesema takriban droni 90 zilidunguliwa katika eneo hilo.
Kwa upande wake, meya wa Moscow Sergei Sobyanin, ameripoti kuwa droni 27 zilizoelekezwa katika mji huo mkuu pia zilidunguliwa.
Gavana wa eneo la kusini magharibi la Saratov Roman Busargin, pia ameripoti kuuawa kwa watu wawili katika mashambulizi ya droni yalioharibu nyumba kadhaa.
Kulingana na wizara hiyo ya ulinzi, jumla ya droni 283 zimedunguliwa.
Katika kulipiza kisasi cha mashambulizi ya Urusi ambayo yamelenga eneo lake kila siku tangu mwaka 2022, Ukraine imekuwa ikishambulia mara kwa mara ndani ya Urusi, ikisema kimsingi inalenga miundombinu ya nishati na ya kijeshi.
Ujerumani yawaondoa wafanyakazi wake wa kidiplomasia Niger

Kikosi cha kupambana na makundi ya itikadi nchini Niger chafanya doria katika eneo la Tillaberi mnamo Juni 11, 2021Picha: Boureima Hama/AFP
Ujerumani imesema jana kwamba imewaondoa kwa muda wafanyakazi wake wa kidiplomasia kutoka Niger kwa sababu za kiusalama katika taifa hilo la Afrika Magharibi, ambalo limekumbwa na ghasia za makundi ya itikadi kali.
Ujumbe uliochapishwa kwenye tovuti ya wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani, umesema kutokana na hali tete ya usalama, wafanyakazi wa ubalozi wa Ujerumani mjini Niamey wamehamishwa kwa muda nje ya Niger na kwamba kwa sasa hawawezi kutoa huduma za kibalozi.
Wizara hiyo pia imesema kuwa raia wa nchi za Magharibi ni walengwa wakuu wa utekaji nyara unaofanywa na makundi ya wahalifu na yale ya kigaidi.
Mnamo mwezi Januari, Marekani pia iliamuru wafanyakazi wake wa kitengo kisichokuwa cha dharura kuondoka Niger kwasababu za kiusalama.
Niger ambayo inaongozwa na jeshi tangu mapinduzi ya Julai 2023, imekuwa ikikumbwa na ghasia za makundi ya itikadi kali yenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda pamoja na lile linalojiita dola la kiislamu IS.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.