Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei ameuawa, televisheni ya serikali imesema

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa: 01/03/2026

Vocalize Pre-Player Loader

Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi…

Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimethibitisha kwamba Kiongozi Mkuu Ali Khamenei ameuawa, katika mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran kutoka ambayo yalianza Jumamosi asubuhi (saa za ndani).

Haya hapa yaliyojiri kwa mukhtasari:

  • Taarifa ya Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran, iliyosomwa vyombo kadhaa vya habari vya serikali, imethibitisha kuwa Ayatollah Khamenei aliuawa ofisini kwake mapema Jumamosi asubuhi.
  • Mtangazaji mmoja, huku akitokwa na machozi, alisema nchi itaanza siku 40 za maombolezo.
  • Zaidi ya watu 200 wameuawa wakati wa mashambulizi hayo, kulingana na Red Crescent, CBS News, mshirika wa habari wa BBC ikiripoti kuwa maafisa 40 wa Iran wameuawa.
  • Kujibu mashamblizi hayo, Iran imeanzisha mashambulizi katika Mashariki ya Kati, dhidi ya mataifa washirika wa Marekani na ambapo Marekani ina kambi za kijeshi, ikiwa ni pamoja na Dubai, Doha, Bahrain, na Kuwait.
  • Uingereza inashiriki katika “operesheni zilizoratibiwa za ulinzi wa kikanda” kulinda raia wa Uingereza na washirika wa kikanda, Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer amesema.
  • Rais Donald Trump hapo awali alisema Khamenei alikuwa “mmoja wa watu waovu zaidi katika historia” na kwamba kifo chake kilikuwa “fursa kubwa zaidi kwa Wairan kurujirudishia nchi yao”. Alisema Marekani itaendelea kuishambulia Iran kwa mabomu – huku milipuko ikiendelea kusikika katika mji mkuu wake Tehran.
  • Marekani haiwezi kutangaza vita bila idhini ya bunge – na operesheni hii imegawanya wabunge, kwa kiasi kikubwa kulingana na vyama.
  • Umoja wa Mataifa pia umesema operesheni hiyo ya kijeshi inadhoofisha amani katika eneo hilo.

Awali, Trump alithibitisha kuwa Khamenei amefariki kupitia akaunti yake kwenye mtandao wa Truth Social.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei ameuawa, televisheni ya serikali imesema

.

Televisheni ya taifa ya Iran imethibitisha kuwa Ayatollah Ali Khamenei ameuawa.

Siku arobaini za maombolezo zatangazwa nchini Iran

Katika hotuba ya machozi, mtangazaji wa televisheni ya serikali ametangaza kifo cha Khamenei na kusema nchi itaingia katika siku 40 za maombolezo.

Jamaa za Khamenei pia waliuawa katika mashambullizi hayo.

Kulingana na Shirika la Habari la Fars ambalo lina mafungamano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kuna ripoti kwamba binti mmoja wa Khamenei ameuawa pia.

Mrithi wa Khamenei hakutajwa kwenye tangazo la kifo chake

.

Taarifa kutoka Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, vyombo kadhaa vya habari vya serikali nchini Iran vimethibitisha kifo cha Ayatollah Khamenei.

Rais wa Marekani Donald Trump saa chache zilizopita alisema Kiongozi Mkuu huyo aliuawa wakati wa shambulio la pamoja na Israel katika maeneo kadhaa kote Iran.

Katika taarifa hiyo, haikutajwa ni jinsi gani Khamenei mwenye umri wa miaka 86 alivyofariki, au ni nani anayeweza kuchukua nafasi ya kiongozi.

Jamaa wa Khamenei pia wameuawa katika mashambulizi hayo

Hapo awali, vyombo vya habari vya serikali vilisema kwamba binti wa Khamenei, mkwewe na mjukuu wake pia waliuawa katika mashambulizi hayo.

Kulingana na Shirika la Habari la Fars, ambalo lina uhusiano na Kikosi cha Revolutionary Guard, kuna ripoti kwamba mmoja wa mabinti wa Khamenei ameuawa pia.

‘Vigogo kadhaa’ wa utawala wa Iran wameuawa – Jeshi la Israel

Afisa wa jeshi la Israel anasema “maafisa kadhaa wenye ushawishi” wa utawala wa Iran “wameuawa” katika shambulioyala leo.

Afisa huyo anasema maeneo matatu ambapomaafisa wa serikali ya Iran walikuwa wamekusanyika yalishambuliwa kwa wakati mmoja wakati wa operesheni hiyo.

Shambulio hilo lilipangwa “kwa muda wa miezi kadhaa”, na ujasusi kubaini “fursa ya kuchukua hatua” wakati “maafisa wakuu wa serikali wangekutana”.

Wanaongeza kuwa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limekuwa kifanya kazi “kwa ushirikiano wa karibu” na Jeshi la Marekani ili kupanga orodha “ya thamani” ya shabaha.

“IDF iko tayari kushambulia Iran tena ikilazimika kufanya hivyo,” wanasema.

Televisheni ya taifa ya Iran: Khamenei aliuawa ofisini kwake

Vyombo vya habari kadhaa vya serikali vilitangaza kifo cha Khamenei kwa wakati mmoja
Maelezo ya picha,Vyombo vya habari kadhaa vya serikali vilitangaza kifo cha Khamenei kwa wakati mmoja

Tukiangazia tena maelezo zaidi taarifa ya Baraza Kuu la Usalama la Iran, iliyosomwa kwenye vituo vya Televisheni vya serikali hapo awali.

Baraza hilo limesema kuwa Ayatollah Khamenei aliuawa mapema Jumamosi asubuhi katika ofisi yake “alipokuwa akitekeleza majukumu yake”.

Kwa kutumia picha za satelaiti, BBC Verify hapo awali ilithibitisha uharibifu mkubwa wa sehemu za Jumba la Uongozi, ambalo ni ofisi ya Khamenei mjini Tehran.

Shirika la Habari la Tasnim linalohusiana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema kwamba kifo cha Khamenei ofisini mwake ni dhibitisho kwamba ripoti kwamba alikuwa akijificha zilikuwa “vita vya kisaikolojia vya adui”.

Jeshi la Israel lasema limekamilisha “shambulio kubwa” dhidi ya Iran

g

Jeshi la Israel lilitangaza kuwa limekamilisha “shambulio kubwa” dhidi ya utawala wa Iran.

Taarifa ya jeshi ilisema: “Moja ya mashambulizi haya yalifanywa kwenye mfumo wa ulinzi wa anga wa juu (SA-65) huko Kermanshah magharibi mwa Iran.”

Taarifa hiyo iliendelea kusema: “Mashambulizi haya yalifanywa kwa lengo la kuanzisha na kuimarisha uhuru wa vitendo wa Jeshi la Anga la Israel juu ya anga ya Iran, ili kudhoofisha uwezo wa Walinzi wa Mapinduzi na vitisho dhidi ya eneo la ndani la Taifa la Israel.”

Mashambulizi mapya yaripotiwa Iran huku nayo ikifanya mashambulizi ya kulipiza kisasi

.

Mtu mmoja ameiambia BBC Persian kwamba mlipuko mpya umesikika magharibi mwa Tehran.

Shirika la habari la AFP linaripoti kwamba waandishi wake wamesikia “mfululizo wa milipuko mipya” katika mji mkuu. Hapo awali shirika hilo lilisema shirika la habari la Iran Fars lilikuwa likiripoti kwamba vitongoji viwili katika mji wa Bushehr kusini mwa Iran – kuliko kiwanda cha nguvu za nyuklia – “vililengwa na makombora”.

Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu (IRNA) linaloendeshwa na serikali ya Iran pia linaripoti kuhusu milipuko mipya mjini Tehran.

Ingawa chanzo hakijajulikana mara moja, hii inakuja baada ya Marekani na Israel kuanzisha mashambulizi ya pamoja dhidi ya Iran mapema hii leo, na kusababisha mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka Iran dhidi ya maeneo lengwa kote Mashariki ya Kati.

Jeshi la Anga la Israeli pia limechapisha kwenye mtandao wa X, likisema “limeanzisha shambulio lingine la anga na linashambulia maeneo ya kurusha makombora na mifumo ya ulinzi katikati mwa Iran”.

Iran yaonya kuhusu ‘mashambulizi mabaya’

Tumepokea taarifa hivi punde kutoka kwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ikionya kwamba watashambulia kambi za Marekani na Israel.

“Operesheni mbaya zaidi ya katika historia ya vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaanza kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na vituo vya kigaidi vya Marekani muda mfupi ujao,” inasema.

Dalili zinaonyesha kuwa kiongozi mkuu wa Iran ‘ameuawa’ – Netanyahu

.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amezungumzia shambulizi dhidi ya eneo la Iran la kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ambalo tuliliripoti mapema.

‘Kuna dalili zinazoongezeka zinazoonyesha kuwa “dikteta huyu” “ameuawa”’, Netanyahu amesema.

Katika hotuba yake, Netanyahu amewaambia Wairan kuwa mashambulizi hayo yatawasaidia “kujiondoa katika udhalimu” na kuongeza kuwa wana “fursa moja tu” ya kupindua utawala wa Iran.

“Nendeni mitaani kwa wingi mumalize kazi hii,” Netanyahu amesema.

Ni “wakati muafaka wa kuungana pamoja kwa ajili ya misheni ya kihistoria”, Netanyahu ameongeza.

Amemalizia hotuba yake kwa kuwataka raia wa Israeli kusikiliza ushauri wa usalama kutoka kwa Kamandi ya Nchi baada ya kupendekeza kwamba operesheni dhidi ya Iran itaendelea “kadiri itakavyohitajika”.

Ripoti ambazo hazijathibitishwa zasema kuwa kiongozi mkuu wa Iran “ameuawa

.

Kufuatia Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu kusema “kuna dalili zinazoongezeka” zinazoonyesha kuwa kiongozi mkuu wa Iran “ameuawa”’, tunaona ripoti ambazo hazijathibitishwa kwamba ameuawa na mashambulizi ya Marekani na Israeli.

Shirika la habari la Reuters, limemnukuu afisa mkuu wa Israeli, na kusema kuwa mwili wa Ayatollah Ali Khamenei umepatikana.

Axios, imenukuu chanzo, na kusema balozi wa Israeli nchini Marekani Yechiel Leiter amewafahamisha maafisa wa Marekani kwamba Khamenei aliuawa katika shambulio lililofanyika kwenye makazi yake huko Tehran.

Na vyanzo vingi vya Israeli, ikiwa ni pamoja na News 12 na Times of Israel, vinanukuu maafisa wa Israeli pia wakidai kwamba kiongozi huyo mkuu amefariki.

Trump asema Kiongozi Mkuu wa Iran amekufa

.

Khamenei, mmoja wa watu waovu zaidi katika Historia, amekufa,” Rais wa Marekani Donald Trump ameandika kwenye Truth Social.

‘Haki si kwa watu wa Iran pekee, bali kwa Wamarekani wote Bora’ – Trump

Katika akaunti yake kwenye mtandao wa Truth Social, Rais wa Marekani Donald Trump ameandika.

“Hii si haki kwa watu wa Iran pekee, bali kwa Wamarekani wote Bora,” amesema.

“Hakufanikiwa kukwepa Majasusi wetu na Mifumo yetu ya Ufuatiliaji ya Kisasa, na, kwa ushirikiano wa karibu na Israeli, hakukuwa ambalo yeye, au viongozi wengine awaliouawa pamoja naye, wangeweza kufanya.”

“Hii ndiyo fursa kubwa zaidi kwa watu wa Iran kuirudisha Nchi yao,” ameongeza.

Awali, Rais Donald Trump wa Marekani alizungumza na NBC News kwa njia ya simu – na wamemuuliza kuhusu ripoti kwamba kiongozi mkuu wa Iran ameuawa na mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel.

“Nimezungumza na watu wengi, tunahisi huu ni ukweli,” Inaripotiwa Trump amemwambia mtangazaji wa Marekani.

“Idadi kubwa ya viongozi wao pia wameuawa,” aliongeza, akirudia kile alichoambia ABC News.

Pia aliambia NBC News kwamba operesheni ya Marekani nchini Iran “tayari imefanikiwa”.

Trump asema ‘viongozi wengi wa Iran wameuawa

Awali, Rais Trump alizungumza na ABC News na kusema kwamba mashambulizi ya Marekani “tayari yamesababisha uharibifu mkubwa” na kuwa viongozi “wengi” wa Iran wameuawa.

“Hatujui yote, lakini mengi yanajulikana,” Trump amesema katika mahojiano ya simu. Rais pia ameongeza kuwa Marekani “ina maono mema” juu kundi lijalo la viongozi wa Iran.

Alipoulizwa kuhusu ni nani atakayechukua nafasi ya Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei, Trump kisha ameiambia NBC: “Sijui, lakini wakati fulani watanipigia simu kuuliza ni nani ningependa.”

“Ninakuwa na mzaha kidogo ninaposema hivyo,” Trump ameongeza:

Trump alipoulizwa ikiwa ana ‘uhakika’ kiongozi mkuu wa Iran ameuawa

Rachel Scott, mwandishi mkuu wa habari za kisiasa katika shirika la ABC News, amesema Donald Trump amemwambia tu kwamba “anaamini” kiongozi mkuu wa Iran amekufa.

Alipoulizwa kama ana “uhakika”, Trump inasemekana alisema: “Sitaki kusema chochote kwa uhakika hadi nitakapoona kwa maco yangu lakini tunaamini amekufa.”

“Na viongozi wao wengi wameuawa. Sio tu kutoka kwenye eneo moja bali pia kutoka kwenye maeneo mengine mawili ambayo pia tumeshambulia. Tulikuwa na taarifa nyingi za ujasusi hivyo basi, tunaamini viongozi wengi wameuawa.”

UAE yalaani shambulio la Iran

Umoja wa Falme za Kiarabu umelaani mashambulizi ya Iran dhidi ya eneo lake, ukiita ni “ukiukaji wa uhuru wa kitaifa na sheria za kimataifa”.

Katika chapisho kwenye mtandao wa X, UAE inaita hatua ya kulipiza kisasi ya Iran kuwa kuongeza hatari na “kitendo cha uwoga” kinachotishia usalama wa raia na kudhoofisha utulivu.

Wizara yake ya ulinzi inasema iko ” katika tahadhari ya juu” na tayari kukabiliana na vitisho vyovyote.

Inaongeza kuwa vikosi vyake vya ulinzi vimezuia makombora 137 ya balestiki na ndege zisizo na rubani 209 zilizorushwa kuelekea nchini.

Kumi na nne kati ya ndege zisizo na rubani zilizoanguka ndani ya maeneo na maji ya nchi hiyo zilisababisha “uharibifu fulani”, inasema.

CBS yasema maafisa 40 wa Iran wauawa katika shambulizi

Chanzo cha habari cha kijasusi na chanzo cha kijeshi kimeambia mshirika wa vyombo vya habari wa BBC, CBS News, kwamba takriban maafisa 40 wa Iran wameuawa katika mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

Haijulikani wazi kama maafisa hao walikuwa katika eneo moja au tofauti.

Walidai kwamba kiongozi mkuu wa Iran, Ali Khamenei, alikuwa miongoni mwa waliofariki, pamoja na kamanda wa Kikosi cha Revolutionary na waziri wa ulinzi.

Iran bado haijathibitisha ripoti zilizoenea kuhusu kifo cha Khamenei.

Kuanzia Dubai hadi Doha, Iran yafanya mashambulizi Mashariki ya Kati

.

Baada ya mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, hatua ya kulipiza kisasi ya Iran imeshuhudiwa kote Mashariki ya Kati – hasa katika maeneo yenye kambi za kijeshi za Marekani, au ambayo ni washirika wa Marekani:

  • Huko Dubai, UAE, mlipuko umeshuhudiwa katika hoteli ya Fairmont The Palm. Mamlaka ya Dubai imesema watu wanne wamejeruhiwa baada ya “jengo la eneo la Palm Jumeirah” kushambuliwa
  • Wizara ya ulinzi ya UAE pia ilisema imezuia wimbi jipya la makombora na ndege zisizo na rubani za Iran, baada ya kusema hapo awali kwamba nchi hiyo imekabiliwa na “shambulizi baya linalohusisha makombora ya Iran”.
  • Huko Doha, Qatar, milipuko imeonekana kulenga kambi ya jeshi la anga ya al Udeid, kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani katika eneo hilo.
  • Kambi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani huko Bahrain ” imeshambuliwa kwa kombora”, kulingana na taarifa iliyonukuliwa na Shirika la Habari la Bahrain linaloendeshwa na serikali.
  • Milipuko ilisikika nchini Kuwait, na shirika la habari la eneo hilo Kuna, lilisema kwamba ndege isiyo na rubani iliyolenga uwanja wa ndege wa kimataifa ilisababisha “majeraha madogo kwa wafanyakazi kadhaa” huku uharibifu “mdogo” ukitokea kwenye kituo cha uwanja wa ndege.
  • Reuters imeripoti kwamba ulinzi wa anga wa Marekani ulidungua ndege isiyo na rubani juu ya kambi ya kijeshi ya Marekani karibu na Erbil, Iraq
  • Jordan – ambayo inapakana na Israeli – inasema kwamba vikosi vyake vya kijeshi vilidungua makombora mawili ya masafa marefu na kwamba vifusi vilianguka katika maeneo mbalimbali
  • Israel pia imeripoti wimbi la makombora ya Iran, huku ving’ora vikilia kote nchini. Jeshi la Israel linasema Iran inataka “kuwatisha raia na kuharibu maeneo yaliyo jirani”

Waandamanaji wakusanyika nje ya ubalozi wa Iran London kuunga mkono mashambulizi ya Marekani na Israel

f

Katika eneo la katikati mwa London, umati wa watu na misafara ya pikipiki walikusanyika nje ya ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuonyesha uungwaji mkono wao kwa mashambulizi ya Marekani na Israel.

Waandamanaji hao, wakiwa wamebeba picha za Reza Pahlavi, walikuwa wakipiga kelele za kauli mbiu kama “Iran idumu, Israel idumu.”

Mwandishi wa habari wa BBC News, Winnie O’Dowd, aliyekuwepo katika mkusanyiko huo, amesema kuwa mapema alasiri kwa saa za eneo hilo, kundi la watu na msafara wa waendesha pikipiki walikusanyika nje ya ubalozi wa Iran kusherehekea na kucheza. Mlio wa pikipiki na kauli mbiu za “Iran idumu, Israel idumu” zilisikika kutoka kwa Wairani waliokuwa na shauku, wakiwa wamebeba picha za Reza Pahlavi, mwana wa Shah wa mwisho wa Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi huyo wa BBC, Davoud Pahlavi, binamu wa aliyekuwa mrithi wa ufalme, alikuwa miongoni mwa waliokuwapo katika sherehe hizo. Umati uliokuwepo ulionekana kwa kiasi kikubwa kumuunga mkono Pahlavi.

Baadhi ya waliohudhuria walikuwa wakinywa kinywaji cha kienyeji cha Iran kiitwacho sagi, aina ya pombe inayotengenezwa kwa zabibu nyeusi au nyeupe za Shiraz.

Wengine walionekana kuwa na wasiwasi kuhusu ndugu na jamaa zao ambao hawakuweza kuwasiliana nao tangu jioni ya siku iliyotangulia.

Watu wanne wajeruhiwa katika shambulio lililofanywa Dubai

f

Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Dubai imesema “tukio limetokea katika jengo lililopo eneo la Palm Jumeirah.”

Kwa mujibu wa ofisi hiyo, vikosi vya uokoaji vilitumwa mara moja katika eneo la tukio na moto uliotokana na tukio hilo sasa “umedhibitiwa.” Watu wanne wamejeruhiwa na wamepelekwa hospitalini kwa matibabu.

Taarifa hiyo inafuatia ripoti ya awali ya shahidi wa tukio, iliyosambazwa pamoja na picha inayoonyesha moshi katika eneo hilo, baada ya vyombo vya habari vya serikali ya Iran kudai kuwa shambulio lilikuwa limeanzishwa dhidi ya Dubai.

Haijabainika wazi Iran inalenga nini hasa, ingawa kuna uwepo wa kijeshi wa United States katika nchi hiyo.

Palm Jumeirah ni visiwa bandia vinavyojulikana kwa hoteli za kifahari na makazi ya hali ya juu.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply