Iran yasema itaendelea kujibu mashambulio ya Israel na Marekani

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa: 01/03/2026

Vocalize Pre-Player Loader

Marekani na Israel, zimetekeleza mashambulio ya kijeshi nchini Iran siku ya Jumamosi, ikimlenga kiongozi wa kiroho Ayatollah Ali Khamenei na rais Masoud Pezeshkian, huku Tehran ikilipiza kisasi kwa kurusha makombora katika nchi za eneo la Ghuba, ikiwemo Israeli.

Raia wakiondolewa kwenye jengo ambalo lilishambuliwa katika eneo la Tirat Hacarmel, karibu na Haifa, kaskazini mwa Israel, Jumamosi, Feb. 28.
Raia wakiondolewa kwenye jengo ambalo lilishambuliwa katika eneo la Tirat Hacarmel, karibu na Haifa, kaskazini mwa Israel, Jumamosi, Feb. 28. AP – Leo Correa

Na:Hillary IngatiFuata

Mashambulio hayo yamejibiwa na Iran, ambayo imerusha makombora yake nchini Israel na kulenga kambi za jeshi la Marekani katika nchi za Bahrain, Qatar, Falme za Kiarabu na Kuwait.

Jeshi la Iran linasema, litaendelea na mashambulizi kulenga kambi za jeshi la Marekani, katika eneo la Ghuba, kwa kile inachosema, hadi adui ambaye ni Marekani na Israeli, watakaposhindwa.

Shambulio la Israeli jijini Tehran
Shambulio la Israeli jijini Tehran Social Media via REUTERS – Social Media

Nchini Iran, shambulio katika shule moja lilitokelezwa na Israeli, limesababisha vifo vya watu 40, huku Falme ya Kiarabu ikisema mtu mmoja ameuawa kufuatia shambulio ya Iran.

Urusi  imelaani mashambulio ya Marekani na Israeli nchini Iran, ikisema ni kitendo hatari, kunachoweza kusababisha vita vya kikanda, na kuwataka raia wake kuondoka Iran na Israeli haraka.

Moshi ukionekana angani kufuatia shambulio la Israel na Marekani jijini Tehran.
Moshi ukionekana angani kufuatia shambulio la Israel na Marekani jijini Tehran. © Reuters/Majid Asgaripour

Naye rais wa UfaransaEmmanuel Macron, ametaka kufanyika kwa dharura kwa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kujadili mzozo huu.

Hatua hii ya Israel na Marekani imekuja, wakati wajumbe kutoka Washington na Tehran, wakikutana jijini Geneva, kujadili uwezekano wa kupatikana kwa mkataba wa kidiplomasia kuhusu mradi wa nyuklia wa Iran, ambao Marekani na Israeli zinasema, nchi hiyo inatengeneza silaha za maangamizi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply