Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Maelezo kuhusu taarifa
Dalitso Lungu, mwana wa rais wa zamani Edgar Lungu ameamriwa na mahakama ya Zambia arejeshe magari 79 na vipande 23 vya ardhi pamoja na majengo, ikiwemo kituo cha biashara, kituo cha mafuta, “ghorofa za kifahari na makazi ya hadhi ya juu” katika mji mkuu, Lusaka. Kisa?, ameshindwa kueleza alikotoa utajiri huo. Haya yanajiri baada ya babake mzazi aliyekuwa rais wa nchi hiyo kustaafu na kisha kufariki dunia mwaka jana.
Kuzaliwa katika familia ya kiongozi mkuu serikalini sio kuzaliwa tu; La hasha! Ni kuzaliwa ndani ya hadithi ambayo tayari imeandikwa kwa macho ya umma.
Mtoto anakuwa nembo, ishara, na wakati mwingine shabaha. Wakati baba au mama yuko madarakani, mlango wa dunia hufunguka kwa urahisi. Lakini mlango huo huo unaweza kujifunga kwa kishindo.
Kwa baadhi yao, dhoruba haishii kwenye kuondoka madarakani. Wazazi wao wanapoondoka kwa kun’golewa, kushindwa uchaguzi, au kifo, ndiyo safasi ya misukosuko ya maisha yao huanza.
Wanapojifurukuta kuanza upya, huandamwa na kesi za ufisadi au hata wengine kuozea jela.
Historia ya kisiasa ya dunia imejaa mifano ya familia zilizotoka kileleni hadi ukingoni.
Makala haya yanaorodhesha watoto wa marais walioshindwa kuikimbia historia na jina la familia limewasakama kila mahali wanakokwenda ni huyu ni ”mtoto wa fulani”.
Dalitso Lungu- Mtoto wa rais wa zamani wa Zambia
Wa hivi karibuni ni mtoto wa kiume wa aliyekuwa rais wa zamani wa Zambia ambaye anaandamwa na kesi chungu nzima.
Alichokivuna wakati babake alipokuwa madarakani kinamsakama kooni baada ya kushindwa kuelezea alifanya biashara gani halali hadi kupata mali zenye thamani ya zaidi ya dola milioni 1.3 za Marekani (£923,000).
Mawakili wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 39 wamedai kuwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kitengo cha Uhalifu wa Kiuchumi na Kifedha katika Mahakama Kuu.
Na upande wa mahakama kuu umeeleza hukumu hiyo imetokana na kugundua kuwa licha mtoto huyo wa aliyekuwa rais kufanya kazi katika kampuni ya vinjwaji na kuhamia katika Mamlaka ya ushuru Zambia ujumla wa mshahara amepokea hauwezi kumtajirisha kiasi hicho.
Edgar Lungu, aliyeiongoza Zambia kwa miaka sita kuanzia mwaka 2015, alifariki dunia nchini Afrika Kusini mwezi Juni mwaka jana, lakini bado hajazikwa kutokana na mvutano wa kisheria unaoendelea kati ya familia yake na serikali ya sasa.
Saif al-Islam Gaddafi (Libya)

Baada ya kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, mtoto wake wa kiume Saif al- Islam Gaddafi alichagua ukimya, lakini jamii bado haikumshahau.
Saif al-Islam aliyesomea nchini Uingereza alihudumu kama mwanadiplomasia, lakini sifa yake iliharibiwa wakati wa maasi ya 2011, alipoapa kwamba Libya itageuka “mito ya damu” ikiwa maandamano dhidi ya utawala wa baba yake yataendelea.
Baada ya kuporomoka kwa serikali, alikamatwa na wanamgambo wakati alipokuwa akijaribu kutoroka nchini, kulingana na ripoti.
Alizuiliwa kwa miaka sita huko Zintan, na mwaka 2015 na hatimaye hukumiwa kifo mahakama ya Tripoli – uamuzi ambao baadaye ulibatilishwa chini ya msamaha.
Maisha ya Saif yaligeuka uwanja wa mapambano.
Mnamo mwaka wa 2015, mahakama ya Libya ilitoa hukumu kifo dhidi ya Saif al-Islam kwa tuhumu za uhalifu wa kivita wakati wa mapinduzi ya 2011.
Pia alishtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai ICC, kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya ubinadamu. Juhudi za mawakili wake kufuta kesi hiyo hazikufua dafu na hivyo kuacha mashtaka hayo bila kutatuliwa kwa miaka mingi.
Vita hivi vya kisheria vilimweka Seif al-Islam katika uangalizi wa kimataifa, licha ya kuishi maisha ya kutoonekana ndani ya Libya.
Saif ameng’angana kurejea mamlakani na kuhuisha utawala wa babake walakin amefariki dunia Februari 04 2026 katika hali tatanishi na kuondoa moja ya alama za mwisho za enzi ya utawala wa Gaddafi.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.