Ujerumani: Makombora ya Iran yanatishia sio Israel pekee bali hata Ulaya

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema nchi yake imejitolea kupata suluhu la kidiplomasia kati ya Marekani na Iran kuhusu mipango ya nyuklia na makombora ya Tehran.

Iran yakutana na viongozi wa Hamas na Houthi wakati wa ziara ya Netanyahu nchini Marekani

.

Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amekutana na kundi la viongozi wa Hamas katika ziara yake nchini Qatar akiwemo Khaled Meshaal, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas.

Bw. Larijani pia alikutana na msemaji wa Houthi nchini Qatar. Kikao cha Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran na viongozi wa makundi yanayoungwa mkono na Jamhuri ya Kiislamu katika eneo kilikwenda sambamba na ziara ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Washington na kukutana na Rais Donald Trump wa Marekani.

Bwana Netanyahu anatarajiwa kumtaka rais wa Marekani kutafuta mapatano na Iran ambayo sio tu kwamba yatasimamisha urutubishaji wa madini ya uranium nchini humo bali pia kupunguza mpango wake wa makombora ya balistiki na uungaji mkono wake kwa makundi yanayoungwa mkono na Tehran katika eneo kama vile Hamas na Hezbollah.

Hii ni licha ya Iran kusisitiza kila mara kuwa mazungumzo yake na Marekani yatahusu tu mpango wake wa nyuklia.

Polisi wamtambua kijana wa miaka 18 kama mshukiwa wa shambulio la Tumbler Ridge

.

Kijana wa miaka 18 ametajwa kuwa mshukiwa wa shambulio la risasi lililoua watu wanane na kujeruhi makumi ya wengine huko British Columbia, Canada.

Polisi walisema Jesse Van Rootselaar alipatikana amefariki katika eneo la tukio kutokana na kujipiga risasi.

Sababu ya shambulio hilo bado haijajulikana. Watu sita waliuawa na wengine 25 kujeruhiwa katika Shule ya Sekondari ya Tumbler Ridge.

Wengine wawili – mama wa mshukiwa, 39, na kaka wa kambo, 11 – walipatikana wamekufa katika nyumba iliyo karibu.

Mamlaka zilisema Van Rootselaar alizaliwa akiwa mwanamume wa kibaolojia lakini akatambuliwa kama mwanamke.

“Ninaweza kusema kwamba Jesse alizaliwa kama mwanamume wa kibaolojia ambaye takriban miaka sita iliyopita alianza kubadilika kuwa mwanamke,” Dwayne McDonald, naibu kamishna wa Polisi wa Kifalme wa Canada (RCMP), alisema.

Tukio la ufyatuaji risasi lilitokea katika nyumba iliyo karibu, kisha mshukiwa akaenda shule, McDonald alisema.

Waliouawa katika shule hiyo ni mwalimu wa kike mwenye umri wa miaka 39, wanafunzi watatu wa kike, wote wakiwa na umri wa miaka 12, na wanafunzi wawili wa kiume, mmoja wa miaka 12 na mwingine 13.

Trump baada ya kukutana na Netanyahu: Ninasisitiza kuendelea na mazungumzo na Iran

.
Maelezo ya picha,Trump na Netanyahu

Baada ya kukutana na Benjamin Netanyahu, Donald Trump aliandika kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii la Truth:

“Hakuna matokeo ya uhakika yaliyopatikana, isipokuwa nilisisitiza kuwa mazungumzo na Iran yanaendelea kuona ikiwa makubaliano yanaweza kufikiwa.” Bw. Trump pia aliandika: “Nilimfahamisha Waziri Mkuu [Netanyahu] kwamba mapendeleo yetu ni makubaliano.

Tutaona matokeo yatakuwaje. Mara ya mwisho Iran iliamua kutoshughulika na ikashambuliwa kupitia [Operesheni] Midnight Hammer. Natumai watachukua hatua kwa busara na kuwajibika zaidi wakati huu.” Bw.Trump pia aliandika kwamba amezungumza pia masuala ya Gaza na Waziri Mkuu wa Israel.

“Tulijadili maendeleo makubwa ambayo yamepatikana huko Gaza na kanda kwa ujumla,” aliandika. Baada ya kikao hicho, ofisi ya Benjamin Netanyahu pia ilitangaza kuwa Waziri Mkuu wa Israel alisisitiza katika kikao hicho kwamba katika mazungumzo ya Marekani na Iran, kipaumbele chake ni kuhakikisha usalama wa Israel.

Kwa mujibu wa AFP, Bw. Netanyahu alikubaliana na Rais wa Marekani “kuratibu na kuwasiliana” ili kuendeleza mazungumzo ya Iran na Marekani.

Bw. Netanyahu alikutana na Steve Whittaker, mjumbe maalum wa Donald Trump, na Jared Kushner, mkwe wa Bw. Trump, jana usiku baada ya kuwasili Washington.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, wawili hao “walishiriki ripoti na Netanyahu kuhusu duru ya kwanza ya mazungumzo na Iran Ijumaa iliyopita.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani: Makombora ya Iran yanatishia si Israel pekee bali hata Ulaya

.
Maelezo ya picha,Waziri wa masuala ya kigeni nchini Ujerumani Johann Wadful

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani amesema nchi yake imejitolea kupata suluhu la kidiplomasia kati ya Marekani na Iran kuhusu mipango ya nyuklia na makombora ya Tehran.

Akizungumza pambizoni mwa mkutano na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Asia ya Kati mjini Berlin, Johann Wadful amesema:

“Mbali na mpango wa nyuklia, mradi wa kutengeneza makombora ya balistiki ya Iran ni hatari kwa Israel na Ulaya.”

Alisisitiza kuwa “ni kwa manufaa yetu kwamba masuala haya yachunguzwe na kutatuliwa kwa mazungumzo.”

Katika wiki za hivi karibuni, Ujerumani imechukua msimamo mkali zaidi kati ya nchi za Ulaya dhidi ya mauaji ya waandamanaji nchini Iran.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply