Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Askari wa zimamoto wakipambana kuuzima moto uliotokona na shambulio la droni la UrusiPicha: State Emergency Service of Ukraine/REUTERS
Urusi imefanya mashambulizi ya droni katika mji wa kusini wa Ukraine wa Odesa na kufanya uharibifu kwenye miundombinu ya nishati na usafiri. Licha ya jitihada mbalimbali za kuvimaliza vita hivyo bado vinaendelea.
Urusi imefanya mashambulizi ya droni katika mji wa kusini wa Ukraine wa Odesa hivi leo na kufanya uharibifu kwenye miundombinu ya nishati na usafiri. Gavana wa mji huo Oleh Kiper amesema mashambulizi hayo pia yamemjeruhi mtu mmoja na kuwasha moto mkubwa katika vituo vingi vya nishati.
Katika upande mwingine, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa ya video kwamba vikosi vyake pia vimechukua udhibiti katika baadhi ya vituo vya treni kusini na katikati mwa mji wa Ukraine wa Kupiansk Vuzlovyi.
Taarifa hiyo ya Urusi imedai kwamba bado vikosi vyake vinaendelea kufanya mashambulizi katika maeneo hayo. Vita vya Urusi nchini Ukraine vyenye zaidi ya miaka mitatu bado vinaendelea licha ya jitihada mbalimbali za kuvimaliza vita hivyo.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.