Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na : Cantona Joseph|RFA

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa,Volker TürkPicha: Uncredited/AP/dpa/picture alliance
Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa,Volker Türk, hii leo amesema ni lazima uchunguzi ufanyike kuhusu mauaji na ukiukwaji mwingine uliofanywa wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29 nchini Tanzania. Turk ameyasema hayo wakati ripoti zikiibuka kwamba miili ya waliouawa inaweza kuwa ilichukuliwa na vikosi vya usalama hadi maeneo ambayo baado hayajafichuliwa.
Taarifa zilizopatikana na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kutoka vyanzo tofauti nchini Tanzania zinaonyesha mamia ya waandamanaji na watu wengine waliuawa na idadi isiyojulikana kujeruhiwa au kukamatwa. Ofisi hiyo lakini imesema imeshindwa kuthibitisha kwa uhuru takwimu za majeruhi kutokana na hali tete ya usalama na kufungwa kwa mtandao kufuatia kura.
Kamishna mkuu huyo amesema zipo ripoti za kufadhaisha kwamba vikosi vya usalama vilionekana vikiondoa miili kutoka mitaani na hospitalini na kuipeleka katika maeneo ambayo hayajafichuliwa kwa jaribio la kuficha ushahidi.
Turk amezitaka mamlaka za Tanzania kuchunguza madai haya ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, kikamilifu na kwa uwazi, na kuwawajibisha wale waliohusika.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.