Mussa Zungu: Spika mpya wa Bunge la Tanzania

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Spika mpya wa Bunge la Tanzania Mussa Azzan Zungu akiendesha shughuli za Bunge mara baada ya kuchaguliwa kuwa spikaPicha: Deo Kaji Makomba/DW

Bunge la nchi hiyo limempata Spika wake mpya atakayeongoza muhimili huo kwa kipindi cha miaka mitano, baada ya zoezi la uchaguzi lililofanyika hii leo bungeni jijini Dodoma.

Kwenye uchaguzi huo wa spika uliosimamiwa na mbunge mkongwe William Lukuvi, Zungu amewabwaga washindani wenzake watano kwa kujipatia kura 378 kati ya kura 383 na hivyo kuwa Spika wa Nane wa bunge hilo.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Zungu amewashukuru wabunge wote wateule kwa kuonyesha Imani kwake kumchagua yeye kuwa Spika na kwamba huo ni ushindi wa wote. Aidha Zungu ameahidi kushirikiana na viongozi wenzake wote kwa kuzingatia sheria na kanuni za bunge.

Baadhi ya wabunge wa Bunge la Tanzania wakiwa kwenye vikao vya bungePicha: Bunge Tanzania

Aliongeza “Nitatoa fursa sawa kwa waheshimiwa wabunge wote, na kwamba ofisi ya spika itakuwa wazi kwa kila mbunge kwa ushauri mbalimbali.”

Hatua ya wabunge wateule kumchagua Mussa Hassan Zungu kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokelewa kwa hisia mseto katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania. Wengi wanasema huo ni uamuzi mzuri kwa kuwa wabunge hao wanamjua vyema Zungu ambaye awali alikuwa Naibu Spika.

Uzoefu unaonyesha kuwa baada ya hatua hiyo ikiwemo viapo vya wabunge wote, Spika atapokea jina moja kutoka kwa Rais, la mtu atakayependekezwa kuwa Waziri Mkuu ili apigiwe kura na wabunge na siku itakayopangwa Rais Samia Suluhu Hassan atakwenda viwanja vya Bunge kulihutubia kwa ajili ya kulizindua rasmi.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply