FURSA YA BIASHARA YA GENGE.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Biashara ya genge ni biashara inayofanyika kila siku kwa sababu inahusiana moja kwa moja na mahitaji ya kila siku ya nyumbani.

Mtu akitaka kupika anakutafuta wewe…
Ni biashara yenye uhitaji mkubwa na inaweza kuanzishwa kwa mtaji mdogo tu.

Eneo la Biashara hii..
Unatakiwa kuchagua sehemu iliyo rahisi kufikika na yenye watu wengi au eneo lenye shughuli nyingi. Kadri watu wanavyopita zaidi, ndivyo nafasi ya kupata wateja wapya inavyoongezeka.

Wateja wakuu wa biashara hii ni wamama wa nyumbani, migahawa mahoteli nk.

Ili kupata wateja wa kudumu unahitaji:kutembelea majumbani ukiwasambazia bidhaa. Na wajulishe ulipo ili wakupate kwa urahisi

Pia tengeneza mazingira safi na yenye kuvutia ili kuvuta wateja wa aina zote.

Vitu vya Kuwa navyo ili uweze Kuanzisha biashara hii ni,
Kibanda (genge),Visu, ndoo, mizani,bahasha au vifungashio. nk.

Bidhaa za kuuza kwenye biashara hii..
Mbogamboga uza mchicha, spinach, chainizi. Matunda uza matikitiki, nanasi, maembe, machungwa, matango, parachichi.Viungo uza vitunguu, vitunguu saumu, pilipili hoho, limao. Vingine uza nazi, karanga, karoti, pilipili nk.

Mtaji wa kuanzia…
Unaweza kuanza na mtaji wa kuanzia laki 2 (au zaidi/chini kulingana na uwezo wako).

Anza na bidhaa chache, ongeza kadri soko linavyokua na wateja wanavyokuzoea.Kumbuka bidhaa nyingi zinaharibika, hivyo usianze na mzigo mkubwa.

Faida Kubwa ya biashara hii..
Unapopata bidhaa kutoka kwa wakulima moja kwa moja au masoko makubwa, faida yako huongezeka.

Kama wazo hili linakufaa anzisha sasa na kimbia nalo sokoni.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply