Basi Mtu mmoja alitembelewa na rafiki yake usiku wa manane,rafiki huyo alikua na njaa alitaji usaidizi.Mtu huyo akatoka na kwenda kumgongea mlango rafiki yake jirani ili ampe angalau chakula ili akampe huyo aliye mtembelea,basi yule aliyekuwa anagongewa akasema unanisumbua mimi nimekwisha lala na watoto wangu,yule bwana akaendelea kugonga mlango akisihi na kusema rafiki yangu ana njaa tafadhali nipatie chochote kitu nimpe apate kula,ndipo yule aliyekuwa ndani akaamka na kumpa mkate ili akampe rafiki yake.Neno hili lina maana fulani
Unapokuja kwangu una shida fulani ili Mungu akusaidie ni mfano wa yule rafiki aliyemtembelea mwenzake usiku wa manane mimi huanza kumuomba Mungu kwaajiri ya hitaji lako hata kama Mungu akichelewa kujibu kwakua Mungu ana watoto wengi duniani na kila mmoja anamuomba nitaendelea kugonga mlango mpaka pale atakapo nipa jibu la tatizo lako nami nitakuja kwako na kusema neno ndipo na wewe utashiba kwa uponyaji,utashiba kiimani,utashiba na kupokea hatua mpya kwa Jina la Yesu.Mama yangu Elizabeth,nampenda saana kwa kusimama na familia nyingi.Ni mkarimu wakati tunakua nilishuhudia mgeni akija hata Wenda wazimu aliwakaribisha akawapa chakula ,akawatengea mahala pa kulala na kuwaombea wanapoondoka.Kipindi hicho alituadithia umuhimu wa kuwakaribisha wageni maana Mungu hutuma malaika wake kupitia njia Kama hiyo.Hatua hii,ilitupa baraka katika familia ambayo tunashuhudia hadi leo.Ukarimu ni baraka.
Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates All rights reserved©2019


Leave a Reply