Gharika Nuhu akalima shamba la mizabibu.

Baada ya Gharika Nuhu akalima shamba la mizabibu,siku moja akanywa mzabibu akalewa,akawa uchi Shem na Yefeti wakamfunika nguo.
Neno hili lina maana na ni ufunuo
Nuhu ndiye aliyekuwa chaguo la Mungu kwa kipindi hicho aliposhuka ndani ya safina baada ya miaka kupita akaanza kuhubiri neno la Mungu,mzabibu unafananishwa kama mtu ndio maana kuna neno linasema nilikupanda mzabibu mwema umegeukaje kuwa mzabibu mwitu? (Yeremia 2;21)Neno linasema Nuhu alikunywa mzabibu akalewa,kulewa katika ulimwengu wa roho ni kuzidiwa na mambo mengi ukakosa majibu watu wakaanza kumhoji na kushindana na Nuhu juu ya Neno la MUNGU akachoka akalewa,tunaona tena kuna sehemu neno linasema akawa uchi,neno hilo lina maana Nuhu alitoka katika utukufu yawezekana watu walimkera sana akajikuta amekasirika na kugombana nao angali nyongeza kwenye kitabu cha mwanzo baada ya Adamu na hawa kula tunda wakajikuta uchi,Yesu alivulishwa nguo pale msalabani akawa uchi maana yake walimdhihaki na kumcheka wakautoa utukufu wake maneno haya ni ya kiroho,unaweza kukasirika mpaka ukafikia hatua ukapigana na mtu lakini baadae ukitulia unagundua nilifanya kosa hapo ndipo tunasema uliupoteza utukufu wako.Baadae sasa Yefeti na kaka yake wakaenda kumsitiri baba yao kwa kumfunika nguo hii ina maana kwamba walimfariji na kumpa moyo,kuna jambo anaweza kufanya ndugu yako,rafiki au jamaa yako likawa sio la kiungwana lakini ukaamua kumtetea na kuona kwamba atabadilika hiyo ndiyo tunasema kumfunika nguo amekosea mpe moyo sio kumtangaza amefanya jambo la aibu mfariji sio kumtangaza wakati anafanya hayo utukufu haukuwepo usimdharau mfunike nguo.
Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates All rights reserved©2019


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment