Mungu alipoumba ulimwengu alichagua watu wake na kuwapa urithi.Watu hao ndio hupigwa vita na njia yao kuwa ngumu sana kufanikiwa.Watu hao ni wewe unae waza mambo makubwa lakini huoni ni wapi pakuanzia,ni wewe ambaye vita vyako haviishi una dhulumiwa unasingiziwa na kuonewa,ni wewe ambaye magonjwa yamekuandama kila siku hayaishi,ni wewe ambaye umekata tamaa ya kuishi na kuona kama huwezi tena kufanikiwa ukidhani umechelewa sana.Sikiliza nikwambie shetani humlenga yule mwenye kitu yule ambaye Mungu ameweka jambo kubwa ndani yake hiyo misuko suko ni lengo la shetani ukate tamaa,kuna mtu mmoja anaitwa Nabothi alikua na shamba la mizabibu lakini ahabu mfalme alilitaka ili alime mboga lakini Nabothi akakataa akisema siwezi kukupa urithi wa baba zangu.Ahabu akachukia mpaka akashindwa kula wala kupata usingizi,ndivyo ilivyo na kwako shetani amechukia sana kuona Mungu amekupa baraka kubwa kiasi hicho lakini kwa kua huoni rohoni unazidharau na ndio maana unakata tamaa iyo ni roho ameweka kwako ili ulicho nacho akiibe,natamka kuanzia sasa Roho hiyo iondoke na kukuacha huru ufikie malengo yako kwa Jina la Yesu.Acha kuwa na mashaka na maombi yako.Dai urithi wako
#Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates
All rights reserved©2019

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.