Toka ulipo zaliwa Mungu alikuandalia maisha yenye baraka na mafanikio.Baraka zako zimefichwa gizani.Kuna mtu kazificha gizani na ndio maana neno linasema nitakupa hazina zilizofichwa gizani.Ukisimama kwa Mungu usiangalie umeshindwa mara ngapi,Tazama Ayubu wote walimkimbia akasema nimebakiza mmoja tu mtetezi wangu yu hai na ataniokoa.
Mungu aliye hai akakupe hazina zako na kukutoa kwenye taabu na shida zako kwa Jina la Yesu.
Maneno ya watu yanaweza kufanya ukachoka kabisa na kukutisha ukaona haiwezekani tena kutoka kwenye shida uliyo nayo,Yupo Mungu anayeishi yeye huondoa udhaifu wote na atakutenga mbali na kuonewa. Kuanzia leo uwe huru,neno hili likawe mkate na maji likakupe nguvu ya kuanza na kusonga mbele.Ni maombi yangu kwako hakuna wa kukushinda tena.
#Iposiku #Getinspired #CantonaJosephMotivates All rights reserved©2019

Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.