
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 31, 2026 13:17 (EAT)


Machafuko ya magenge yanayoendelea HaitiPicha: Arte France
Polisi nchini Haiti inasema watu 16 wameuwawa katika shambulizi la genge mwishoni mwa wiki wakati ambapo Umoja wa Mataifa umesema kuwa huenda hadi watu 80 waliuwawa.
Shambulizi hilo lilifanyika katika mji wa Petite Riviere, mji ulioko katikati mwa Haiti.
Mwanaharakati katika eneo hilo amesema wanachama wa genge la Gran Grif walichoma nyumba na kusababisha vifo vya watu kadhaa huku mashambulizi zaidi yakifanyika jana Jumatatu.
Mwakilishi wa Mtandao wa Kitaifa wa Ulinzi wa Haki za BinadamuPierre Esperance, amewaambia waandishi wa habari wa shirika la Ufaransa AFP kuwa washambuliaji hao walikuwa wanawapiga risasi watu waliokuwa wanakimbia baada ya kuchomwa kwa nyumba zao huku wengine wakiuwawa kwa karibu.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema shambulizi hilo linaonesha wazi jinsi hali ilivyo mbaya nchini humo.
Wanadiplomasia wa EU wako Kyiv kuadhimisha mauaji ya Bucha
Mwanadiplomasia mkuu wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas na mawaziri wengine wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wamewasili mjini Kyiv kuhudhuria kumbukumbu ya mwaka wa nne tangu mauaji ya Bucha.

Maadhimisho ya mauaji ya Bucha huko UkrainePicha: Evgeniy Maloletka/AP Photo/picture alliance
Mawaziri hao wa mambo ya kigeni pia wanaonesha uungwaji mkono wa nchi hiyo huku kukiwa na mivutano ndani ya Umoja wa Ulaya kuhusiana na msaada kwa Ukraine.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine Andrii Sybihaamesema uwepo wa ujumbe huo wa Umoja wa Ulaya unaonesha kuwa ni lazima haki ipatikane kwa ukatili uliofanywa na Urusi.
Vikosi vya Urusi miaka minne iliyopita viliwauwa zaidi ya watu 400 katika mji huo ulio kilomita 25 kutoka Kyiv.
Urusi ilikanusha kwamba vikosi vyake vilifanya mauaji hayo ikidai kuwa Ukraine ilibuni tukio hilo.
Mashambulizi ya Marekani na Israel yaharibu eneo la kidini
Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kukiharibu kabisa kituo kikuu cha mafuta cha Iran cha Kisiwa cha Kharg pamoja na viwanda vya umeme na kusafisha maji, iwapo Tehran haitokubali kufikia makubaliano.

Uharibifu katika jengo baada ya shambulizi la IsraelPicha: Sobhan Farajvan/Pacific Press/picture alliance
Trump ametoa kitisho hicho licha ya kusema kuwa juhudi za kidiplomasia zinapiga hatua.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Israel ambaye ndiye mshirika wa Trump katika mashambulizi hayo amesema zaidi ya nusu ya malengo ya jeshi lake yametimizwa, huku viongozi wote wawili wakikataa kutoa muda ambao operesheni hiyo iliyosababisha vita vya kikanda na bei za mafuta kupanda, itakapokwisha.
Hayo yakiarifiwa mashambulizi ya Marekani na Israel Jumanne yamesababisha uharibifu katika eneo la kidini la Waislamu wa Kishia kaskazini magharibi mwa Iran.
Vyombo vya habari nchini Iran vimeripoti kuwa jengo la Grand Husseinya, ambao ni ukumbi unaotumiwa kwa mikusanyiko na shughuli za maombolezo za Washia, limeharibiwa kufuatia shambulizi katika mji wa Zanjan.
Kwengineko waandishi wa habari wa shirika la AFP wameripoti milipuko hii leo huko Dubai huku Saudi Arabia ikisema watu wawili wamejeruhiwa kusini mashariki mwa Riyadh kufuatia kuzuiliwa kwa shambulizi la droni.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, republic-of, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands, wallis-and-futuna-islands, wallis-et-futuna, washington-dc, western-sahara, yemen, zambia, zambie, zimbabwe
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.