Trump asema Marekani inaweza ‘kuchukua mafuta nchini Iran’ na kukiteka Kisiwa cha Kharg

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 30, 2026 07:37 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader
Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ameliambia gazeti la Financial Times kwamba anaweza “kuchukua mafuta nchini Iran” na ikiwezekana akakiteka Kisiwa cha Kharg ambacho ni kitovu kikuu cha mafuta nchini humo.

“Kusema ukweli, jambo ninalotaka zaidi ni kuchukua mafuta nchini Iran lakini baadhi ya watu wajinga huko Marekani wanasema: ‘Kwa nini unafanya hivyo?’ Lakini ni watu wajinga,” alisema.

Trump alipendekeza hatua hiyo inaweza kumaanisha kuchukua kisiwa cha Kharg. “Pengine tuchukue Kisiwa cha Kharg, au tuachane nacho. Tuna chaguzi nyingi,” Trump aliambia Financial Times. “Inamaanisha pia kuwa tulipaswa kuwa huko [katika Kisiwa cha Kharg] kwa muda.”

Alipoulizwa kuhusu ulinzi wa Iran katika kisiwa hicho alisema: “Sidhani kama wana utetezi wowote. Tunaweza kukichukua kwa urahisi sana.”

Kauli hiyo ya rais inakuja huku wanajeshi 3,500 zaidi wa Marekani wakiwasili Mashariki ya Kati, hofu ya wanajeshi wa Marekani kijiunga na mashambulizi ya Iran ikiongezeka.

Trump aliongeza kuwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran kupitia “mabalozi” wa Pakistan yalikuwa yanaendelea vizuri, lakini hakugusia suala makubaliano ya kusitisha mapigano yanaweza kufikiwa hivi karibuni.

“Mkataba unaweza kufikiwa haraka,” alisema.

Mafuta yapanda zaidi ya $115 huku hisa za Asia zikishuka thamani

.

Bei ya mafuta duniani imepanda na hifadhi kushuka kwa kasi Jumatatu asubuhi huko Asia huku vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vikiongezeka.

Bei ya mafuta ghafi ya Brent ilipanda kwa zaidi ya 3% hadi zaidi ya dola 115 (£86.77) kwa pipa, huku mafuta yanayouzwa Marekani yakipanda hadi dola 103 baada ya kuimarika kwa 3.5%. Inaiweka Brent kwenye mstari kwa faida yake kubwa zaidi ya kila mwezi.

Masoko ya hisa barani Asia yalishuka thamani, huku Nikkei 225 ya Japani ikishuka kwa 4.5% na Kospi ya Korea Kusini 4% chini.

Haya yanajiri baada ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen kujiunga na vita kwa kuishambulia Israel mwishoni mwa juma na Iran kutishia kupanua mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya vyuo vikuu na nyumba za maafisa wa Marekani na Israel.

‘Mikono iliyojaa damu’: Papa Leo ‘awakosoa’ wale wanaohusika katika vita

Papa Leo XIV

Huku mzozo katika Mashariki ya Kati ukiendelea, Kiongozo wa Kanisa Katoliliki Duniani Papa Leo XIV ameonekana kuwakosoa wale wanaohusika na vita hivyo.

Akiwahutubia waumini wa kanisa hilo mjini Vatican wakati wa maadhimisho ya Jumapili ya Mitende, Papa alisema Mungu anakataa maombi ya viongozi wanaoanzisha vita na kuwa na “mikono iliyojaa damu”, katika kile ambacho kimetafsiriwa kuwa ukosoaji wa wale waliohusika katika vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

“Huyu ndiye Mungu wetu: Yesu, mfalme wa amani, anayekataa vita, ambaye hakuna mtu anayeweza kumtumia kuhalalisha vita,” anasema Papa.

“Hasikii maombi ya wapiganaji, lakini anakataa.” Akinukuu kifungu fulani cha Biblia, anasema: “‘Hata mjaposali sala nyingi, sitasikiliza: mikono yenu imejaa damu’.”

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply