Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 30, 2026 07:37 (EAT)



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO), Ngozi Okonjo-Iweala, anasema Marekani na Brazil zinatakiwa kumaliza tafauti zao.Picha: DW
Mkutano wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) umemalizika nchini Kameruni bila ya makubaliano kwenye masuala muhimu ya mageuzi, kilimo na biashara ya mtandaoni kutokana na mgongano baina ya Marekani na Brazil.
Waziri wa Biashara wa Kameruni, Mbarga Atangana, alisema baada ya siku nne za mkutano huo mjini Yaoundé, wameona muda hautoshi kufikia makubaliano kwenye masuala hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa WTO, Ngozi Okonjo-Iweala, alisema anatumai nchi hizo “zitaweza kuurejesha mkataba wa kusitishwa kwa biashara ya mtandaoni ambao umemalizika muda wake, na kuziwezesha kutoza ushuru wa forodha kwenye utumaji wa kielektroniki kama vile kupakua na kutangaza.”
Majadiliano hayo yalikwama baada ya Marekani na Brazil kutafautiana juu ya kuongezwa muda huo kwa miaka miwili mingine.
Hata hivyo, mkurugenzi mkuu huyo wa WTO aliongeza kuwa Marekani na Brazil zilikuwa zinafanya mazungumzo baina yao kuukwamua mkwamo huo.
Meli ya mafuta ya Urusi kuwasili Kuba kusaidia umeme

Meli ya mafuta kando ya eneo la viwanda kwenye mji mkuu wa Kuba, Havana.Picha: Adalberto Roque/AFP
Meli ya mafuta ya Urusi inatazamiwa kutia nanga nchini Kuba muda wowote kutokea sasa, ikiwa na matangi 730,000 ya mafuta ya dizeli yanayotosha kuzalisha umeme kwa angalau mwezi mmoja.
Taifa hilo la visiwa limekosa umeme kwa muda mrefu sasa kutokana na vikwazo vya Marekani.
Ingawa meli iitwayo Anatoly Kolodin imewekewa vikwazo vya kimataifa kutokana na vita vya Urusi nchini Ukraine, Rais Donald Trump wa Marekani amesema ameiruhusu kufikisha mafuta hayo.
Kuba imekuwa ikikabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kutokana na mbinyo mkali inaowekewa na Marekani inayoilazimisha kubadili mfumo wake wa utawala.
Tangu kurudi tena madarakani, Trump amezidisha vikwazo hivyo maradufu, ambavyo sasa vinaathiri hata huduma za kila siku, zikiwemo hospitali na chakula.
Trump adai mabadiliko ya utawala yamefanikiwa Iran

Rais Donald Trump wa Marekani anadai lengo la kubadilisha utawala nchini Iran limefanikiwa kutokana na vita alivyoshirikiana na Israel dhidi ya Jamhuri hiyo ya Kiislamu.Picha: Mark Schiefelbein/AP Photo/dpa/picture alliance
Rais Donald Trump wa Marekani amedai kwamba vita vilivyoanzishwa na nchi yake na Israel vimeshafanikiwa kuleta mabadiliko ya utawala nchini Iran, huku akihakikisha kuwa ataweza kufikia makubaliano na Wairani.
Akizungumza na waandishi mjini Washington siku ya Jumatatu (Machi 30), Trump aliyataja majina ya viongozi kadhaa wa Iran waliokwishawauwa kwenye vita hivyo ambavyo vimetimia mwezi mzima sasa.
Rais huyo wa Marekani alisema kwa sasa wanashughulika na viongozi tafauti kabisa, jambo ambalo linamfanya aone kuwa “tayari kuna mabadiliko ya utawala.”
Kauli hiyo ya Trump ilitolewa wakati mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Saudi Arabia na Misri wakirejea nyumbani baada ya mkutano wao nchini Pakistan uliojadili hatua zilizopigwa katika juhudi za kuzileta Iran na Marekani kwenye meza ya mazungumzo kukomesha vita hivyo.
Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Pakistan haikutowa undani wa majadiliano hayo, lakini Spika wa Bunge wa Iran, Mohammad Bagher Qalibaf, ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba vikosi vya nchi yake vinangojea kuwakabili wanajeshi wa Marekani kuwasili nchini humo wakati wowote.
Tayari kikosi cha wanajeshi wa Marekani 2,500 wa ziada kimewasili kwenye eneo la Mashariki ya Kati, ikikhofiwa kuwa ni kwa ajili ya kuivamia Iran kupitia ardhini.
Amnesty yaonya Kombe la Dunia kuwa ‘jukwaa la ukandamizaji’

Mechi ya kirafiki kuelekea michuano ya Kombe la Dunia 2026 kati ya Ujerumani na Uswisi iliyochezwa tarehe 27 Machi 2026.Picha: Heiko Becker/HMB Media/picture alliance
Ripoti mpya ya shirika la haki za binaadamu iliyotolewa leo imeonya kwamba mashindano ya Kombe la Dunia mwaka huu yanaweza kugeuka kuwa jukwaa la ukandamizaji na matendo ya kidikteta.
Ripoti ya shirika hilo yenye kurasa 36 iliyopewa jina “Ubinaadamu Lazima Ushinde: Kulinda haki, kukabiliana na ukandamizaji kwenye Kombe la Dunia la FIFA 2026” inachambuwa kwa kina matukio yanayoweza kuhatarisha haki za mashabiki, wachezaji, waandishi wa habari, wafanyakazi na jamii za wenyeji kwenye mataifa hayo matatu.
Ikiwa ni miezi michache kuelekea michuano hiyo, Marekani bado imeweka marufuku ya kuingia nchini humo kwa baadhi ya nchi ambazo zimefaulu kushiriki kombe hilo litakalokuwa na mechi 48.
Michuano hiyo inayotazamiwa kuhudhuriwa na mamilioni ya mashabiki wa soka inaanza mnamo Juni Mosi kwa maechi kati ya Meksiko na Afrika Kusini.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, republic-of, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands, wallis-and-futuna-islands, wallis-et-futuna, washington-dc, western-sahara, yemen, zambia, zambie, zimbabwe
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.