Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 27, 2026 16:52 (EAT)


Gazeti la Washington Post liliripoti siku ya Ijumaa, likinukuu vyanzo ambavyo havikutajwa jina, kwamba jeshi la Marekani limerusha zaidi ya makombora 850 ya kusafiri ya Tomahawk wakati wa vita vya wiki nne na Iran.
Ripoti hiyo ilisema kuwa utumiaji wa makombora hayo ambayo hulenga kwa usahihi shabaha zinazopigwa, ulikuwa wa kiwango cha juu, jambo ambalo lilizua wasiwasi miongoni mwa baadhi ya maafisa wa Pentagon na kusababisha mijadala ya ndani kuhusu jinsi ya kuongeza idadi ya silaha hizo.
Shirika la habari la Reuters lilisema bado halijaweza kuthibitisha ripoti ya gazeti hilo, huku Wizara ya Ulinzi ya Marekani na Ikulu ya Marekani hazikujibu ombi la Reuters la kutoa maoni yao.
Israel yaanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Iran

Picha: Vahid Salemi/AP Photo/dpa/picture alliance
Israel imeendelea na mashambulizi yake dhidi ya Iran, wakati mvutano ukiendelea kati ya Tehran na Marekani wa usitishaji vita.
Israel imesema imeshambulia maeneo ya Iran ya kutengeneza makombora na silaha nyengine pamoja na kushambulia maeneo ya Magharibi mwa Jamhuri ya kiislamu yanayotumika kurushia makombora.
Haya yanajiri wakati Iran na Marekani zikiendelea kuvutana kuhusu usitishaji vita hivyo vinavyoingia mwezi mmoja kesho Jumamosi (28.03.2026).
Marekani imekuwa ikiishinikiza Iran kuingia katika mazungumzo ya mpango wa nukta 15 wa usitishaji vita, lakini wakati huo huo imeamuru maelfu ya wanajeshi wake kupelekwa katika eneo hilo la Mashariki ya Kati kwa matayarisho ya kile kinachosemekana ni kujaribu kudhibiti mlango bahari wa Hormuz kutoka kwa Iran.
Rais wa Marekani Donald Trump ameipa Iran hadi Aprili 6 kuufungua mlango huo au miundombinu yake muhimu ya nishati ishambuliwe na kuharibiwa vibaya.
Iran kupitia waziri wake wa nje Abbas Araghchi imesema haijaingia katika mazungumzo yoyote ya kusitisha vita na wala haina mipango ya kufanya hivyo.
Marco Rubio akutana na mawaziri wenzake wa G7 kujadili Iran

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Marco RubioPicha: Kevin Wolf/AP Photo/dpa/picture alliance
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Marco Rubio amewasili leo Ijumaa nchini Ufaransa kuhudhuria mkutano wa kwanza rasmi wa kundi la mataifa saba yaliyoendelea kiviwanda duniani G7
Mkutano huo ni wa kwanza kufanyika, tangu Marekani ambae ni mwanachama wa G7 kuanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya Iran. Vita vya Iran vinatarajiwa kuchukua nafasi kubwa katika ajenda ya mkutano huo.
Rubio anatarajiwa kujibu maswali mazito kutoka kwa washirika wake wa Ulaya kuhusu mkakati wa Marekani katika Vita hivyo vilivyoanza Februari 28 ambayo tayari vimesababisha bei ya mafuta kupanda duniani kutokana na mlango bahari wa Hormuz kufungwa na Iran. Mlango huo unatumika kusafirishia asilimia 20 ya nishati ya mafuta duniani.
Uingereza: Uhusiano wa Urusi na Iran unatupa mashaka
Huku hayo yakiarifiwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza Yvette Cooper nchi yake na washirika wake wa G7 wanawasiwasi kuhusu mafungamano ya Urusi na Iran baada ya ya nchi za Magharibi kuituhumu Moscow kuisaidia Tehran kushambulia vituo vya Marekani katikaeneo la Ghuba.
“Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu uhusiano kati ya Urusi na Iran ambao ni wa muda mrefu – kama vile Iran inavyoipa Urusi droni zinazotumika kwenye vita vya Ukraine. Lakini pia tumeona jinsi Urusi inavyoisaidia Iran katika mzozo wa Mashariki ya Kati. Na ndiyo maana G7, tumekuja pamoja kujadili mambo haya na njia ya kuulinda uchumi wa dunia kutoka nchi zinazotaka kutumia silaha kuathiri uchumi wetu”
Urusi imekanusha vikali tuhuma hizo. Mkutano unaofanyika nje ya Paris utavijadili pia vita vya Urusi dhidi ya Ukraine, hali ya Mashariki ya Kati, pamoja na vitisho vinavyoikabili amani na utulivu wa duniani.
UN yataka haki itendeke baada ya shule ya Iran kushambuliwa

Mkuu wa Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, Volker Turk,Picha: DW
Umoja wa Mataifa umeitaka Marekani ikamilishe uchunguzi wake juu ya mauaji ya kutisha ya watoto 160 kwenye shule moja ya wasichana katika siku ya kwanza ya vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran, mnamo Februari 28.
Mkuu wa Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema kushambuliwa kwa shule hiyo ya msingi ya Shajareh Tayyebeh, kulibainisha ukatili usioelezeka dhidi ya watoto, na kwamba lazima kuwe na uwajibikaji kwa waliohusika.
Katika mkutano wa Baraza hilo mjini Geneva, Turk alisema mvutano ulioko kwa sasa dhidi ya mataifa yaliyovitani, hauwezi kusuluhishwa kwa mauaji ya wanafunzi.
Amesema mauaji hayo yamefungua dirisha kubwa la hofu duniani na kwamba haki lazima itendeke.
Turk ameitolea mwito Marekani kukamilisha haraka uchunguzi wa shambulizi dhidi ya shule hiyo akisema matokeo yake ni lazima yatangazwe hadharani.
Ukraine na Saudi Arabia zasaini makubaliano ya kiulinzi

Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman akiwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mjini JeddahPicha: SPA/Xinhua/picture alliance
Maafisa wawili wakuu Ukraine na Saudi Arabia wamesema nchi hizo mbili zimesaini makubaliano ya mifumo ya ulinzi wa anga.
Nchi hizo zimesaini makubaliano ya mifumo hiyo ya ulinzi wa anga wakati wa ziara ya Rais Volodymyr Zelensky katika nchi hiyo ya Ghuba, inayokabiliwa na mashambulizi ya droni kutoka kwa Iran.
Kulingana na maafisa waliozungumza na shirika la habari la AFP, makubaliano hayo yataiwezesha Ukraine kuisadia Saudi Arabia kuuunda mifumo ya ulinzi wa anga ambaypo nchi hiyo haina kwa sasa.
Zelensky alithibitisha hilo kwenye mtandao wake wa kijamii kwamba nchi hizo mbili zimefikia makubaliano muhimu kuhusu ushirikiano wa kiulinzi na kwamba alikutana na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman wakati wa ziara yake.
Waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi aapishwa Nepal

Balendra Shah aapishwa kuwa Waziri mkuu mwenye umri mdogo zaidi NepalPicha: Prakash Mathema/AFP
Balendra Shah ameapishwa hii leo kuwa waziri mkuu mpya na mwenye umri mdogo zaidi katika historia ya Nepal, baada ya chama chake kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.
Uchaguzi huo ulifanyika baada ya maandmano makubwa ya vijana kuuangusha utawala wa zamani mwezi Septemba mwaka jana.
Balendra Shah, aliye na umri wa miaka 35, anayejulikana sana kama Balen, aliteuliwa kuwa waziri mkuu na Rais Ram Chandra Paudel baada ya chama chake cha Rastriya Swatantra kushinda karibu theluthi mbili ya viti bungeni.
Shah, ambaye hana uzoefu wa muda mrefu kisiasa, anakabiliwa na jukumu la kurejesha imani ya wananchi waliokata tamaa kutokana na ufisadi na migogoro ya kisiasa iliyozoeleka katika vyama vya zamani.
Hafla ya kuapishwa kwake ilijumuisha taratibu za kidini za Kihindu na Kibudha. Shah alizaliwa Kathmandu lakini asili ya familia yake ni kutoka eneo la Terai, karibu na mpaka wa India.
Balendra Shah, ambaye ni mhandisi, aliyepata umaarufu kwa kuwa msanii, kabla ya kugeukia siasa, kwa kuwa meya wa Kathmandu alijipatia umaarufu zaidi wakati wa maandamano makubwa ya vijana mwezi Septemba yaliyosababisha kuanguka kwa serikali, ingawa hakushiriki moja kwa moja maandamano hayo, aliyaunga mkono kwa kiwango kikubwa.
UN: Mgogoro mashariki mwa DRC unaongezeka maradufu

Kaimu Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC Vivian van de Perre akihojiwa na waandishi wa habari alipotembelea Goma, mashariki mwa Kongo.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance
Kaimu Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa mgogoro katika eneo lenye utajiri wa madini mashariki mwa Kongo, unazidi kuongezeka.
Vivian van de Perre amesema licha ya waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda kuondoka mwezi Januari katika mji wa Uvira kufuatia shinikizo la kimataifa, mapigano yanazidi kuongezeka katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini kati ya kundi hilo na jeshi la Kongo, na kwamba matumizi ya silaha nzito na droni yanahatarisha kwa kiasi kikubwa maisha ya raia.
Mjumbe huyo ameendelea kutahadharisha kuwa hali huko Kivu Kusini bado ni tete na kwamba kumezuka uhasama mpya unaotanua mzozo huo katika maeneo mengine ikiwa ni pamoja na mkoa wa Tshopo na eneo la mpakani mwa Burundi, jambo linalozidisha hatari ya kuzuka kwa vita vya kikanda.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.