Iran na Marekani zakamilisha mazungumzo bila mwafaka

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na  Cantona Joseph Imechapishwa : February 27, 2026 13:21 (EAT)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas AraqchiPicha: Dilara Senkaya/REUTERS

Wasuluhishi wa mzozo kati ya Marekani na Iran unaohusu mpango wa nyuklia wa Tehran wamesema mazungumzo yaliyofanyika Alhamisi mjini Geneva yamekamilika bila makubaliano, lakini yalipiga hatua kubwa.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi ameyasifu mazungumzo hayo akiashiria awamu nyingine ya majadiliano  yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Iran yaitaka Marekani iachane na matakwa yasiyotekelezeka

Licha ya hatua hiyo Araqchi amesema ili kupata makubaliano, Marekani haina budi kuachana na matakwa mengi yasiyotekelezeka. Amesisitiza kuwa ili mazungumzo yao yapate mafanikio, kunahitajika umakini na kuzingatia uhalisia.

Kongo, Marekani zasaini makubaliano ya dola bilion 1.2.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix TshisekediPicha: Fabrice Coffrini/AFP

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Marekani zimetiliana saini makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya afya yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 1.2. ayo ni kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa Alhamisi.

Chini ya makubaliano hayo, Marekani itaipa Kongo dola milioni 900 katika kipindi cha miaka mitano. Fedha hizo zitatumika kuisaidia Kongo kupambana na UKIMWI, Kifua kikuu, malaria, vifo vya mama na mtoto na magonjwa mengine ya kuambukiza.

Kongo yaahidi kuongeza bajeti yake ya Afya

Kongo kwa upande wake itaongeza bajeti yake ya afya kwa takriban dola milioni 300 ndani ya muda huo. Makubaliano hayo ni sehemu ya ushirika wa Marekani na nchi za Afrika katika sekta ya afya ambapo tayari mataifa 19 yameshasaini makubaliano ya aina hiyo. Mpango huo ni mbadala wa programu za afya zilizokuwa chini ya lililokuwa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani USAID ambalo limefungwa.

Pakistan yafanya mashambulizi ya anga dhidi ya Afghanistan

Maafisa wa usalama wa Taliban wakilinda doria karibu na mpaka wa Torkham karibu na mpaka wa AfghanistanPicha: Aimal Zahir/AFP

Pakistan imefanya mashambulizi makubwa ya anga yaliyoilenga miji kadhaa ya Afghanistan ikiwemo Kabul, Kandahar na Paktia usiku wa kuamkia Ijumaa. Mashambulizi hayo yaliilenga miundombinu ya serikali ya Taliban.

Mapigano yameripotiwa pia sehemu kadhaa kwenye eneo la mpaka wa mataifa hayo. Kwa upande wake Afghanistan imesema imefanya mashambulizi ya kulipa kisasi dhidi ya miundombinu ya kijeshi ya Pakistan. Kutokana na mashambulizi hayo, Waziri wa Ulinzi wa Pakistan ametangaza kuwa nchi hizo mbili sasa ziko katika “vita vya wazi. 

Uhusiano unaozidi kudorora

Uhusiano kati ya mataifa hayo umekuwa wa mashaka kutokana na mzozo wa muda mrefu ambapo Pakistan inaishutumu Afghanistan kwa kushindwa kuyadhibiti makundi ya wanamgambo yanayofanya mashambulizi ndani ya taifa hilo, madai ambayoTaliban inayakanusha.

UN yatangaza ukatili dhidi ya wanawake kuwa janga la dharura

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker TürkPicha: Uncredited/AP/dpa/picture alliance

Umoja wa Mataifa kupitia Kamishna Mkuu wa ofisi yake ya Haki za Binadamu Volker Turk umelaani vikali hali inayoongezeka ya kukiukwa haki za wanawake kote duniani.

Turk ameyasema hayo kwenye Baraza la Haki za Binadamu mapema leo mjini Geneva ambapo ameyagusia mauaji pamoja na unyanyasaji wa kutisha uliodhihirika kutokana na kesi ya Jefferey Epstein nchini Marekani.

Dharura kote duniani

Mkuu huyo wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameutangaza ukatili dhidi ya wanawake kuwa janga la dharura kote duniani. Aidha ameweka wazi kuwa takriban wanawake na wasichana 50,000 waliuwawa kote duniani mwaka 2024. Wengi wa waliowauwa ni sehemu ya familia zao.

UN: Zaidi ya wahamiaji 7,600 walikufa njiani mwaka 2025

Umoja wa Mataifa umebainishakuwa zaidi ya wahamiaji 7,600 walikufa njiani mwaka 2025Picha: Gianluca Chininea/AFP/Getty Images

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limebainisha kwamba zaidi ya wahamiaji 7, 600 wasio na vibali walifariki dunia au walipotea kote duniani wakiwa njiani mwaka uliopita.

Ripoti iliyotolewa na shirika hilo Alhamisi imeeleza kuwa idadi hiyo ni ya vifo vilivyoripotiwa rasmi. Idadi kamili inaaminika kuwa kubwa zaidi lakini haiwezi kufuatiliwa kutokana na uhaba mkubwa wa fedha unaolikabili shirika hilo.

Mwaka 2024 IOM iliripoti vifo vya wahamiaji 9,200 idadi ambayo ni kubwa zaidi tangu shirika hilo lilipoanza kufanya ufuatiliaji mwaka 2024.

Bahari ya Mediterania hatari zaidi kwa wahamiaji waio na vibali

Kulingana na ripoti hiyo, Bahari ya Mediterania ndiyo njia hatari zaidi ya uhamiaji. Kufikia Februari 24 mwaka huu, tayari mamlaka zimehifadhi kumbukumbu ya vifo 606 kwa mwaka huu pekee ongezeko ambalo ni kubwa ikilinganishwa nwa vifo 285 vilivyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2025.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply