Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa : February 27, 2026 18:21 (EAT)

Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker TürkPicha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/dpa/picture alliance
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk, ametaka hatua za haraka zichukuliwe ili kuepusha vita vingine kamili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini.
Zaidi Turk amefafanua kuwa hatua hizo zinatakiwa kuchukuliwa ili kuyadumisha makubaliano ya amani na kuzuia migawanyiko pamoja na mwendelezo wa visasi vinavyoweza kuibua vita kamili.
Akilihutubia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, ameonya kuwa, maadili ya kijeshi yameporomoka kwenye pande zote za mzozo.
Mashambulizi yanayowalenga raia yaushtusha Umoja wa Mataifa
Turk ameelezea kushtushwa na mashambulizi ya mwishoni mwa Juma yaliyosababisha vifo vya raia 21 wasio na silaha wakiwemo wanawake na watoto. Ametahadharisha pia kuhusu hatari kubwa kwa wafanyakazi wa mashirika ya misaada Sudan Kusini na kuwa kwa mwaka uliopita, kulikuwa na mashambulizi 350 yaliyowalenga wafanyakazi hao na ofisi zao.
Pakistan iko ‘vitani’ na Afghanistan – Waziri wa ulinzi

Mashambulizi hayo yalitokea baada ya Taliban wa Afghanistan kutangaza shambulio kubwa dhidi ya vituo vya kijeshi vya Pakistan karibu na mpaka Alhamisi usiku.
Aliyekuwa mwanadiplomasia wa Marekani ahukumiwa kifungo cha maisha kwa unyanyasaji Burkina Faso

Raia mmoja wa Marekani amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwanyanyasa kingono wasichana wawili wa kike wakati akifanya kazi katika ubalozi wa Marekani nchini Burkina Faso.
Idara ya Sheria ya Marekani ilisema Fode Sitafa Mara mwenye umri wa miaka 41, kutoka Maryland, alihukumiwa siku ya Jumatano kufuatia kesi ya wiki mbili mnamo mwezi Oktoba 2025 katika Mahakama ya Wilaya ya shirikisho ya jimbo hilo.
Baraza la mahakama lilimpata na hatia ya makosa manne ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mtoto mdogo, pamoja na kujaribu kulazimisha na kumshawishi mtoto mdogo na kujaribu kuzuia haki kupatikana.
Mashtaka yaliwasilishwa kama sehemu ya Mradi wa ‘Safe Childhood,’ mpango wa kitaifa uliozinduliwa na Idara ya Sheria mwaka wa 2006 ili kupambana na unyanyasaji wa kingono kwa watoto.
Waendesha mashtaka walisema makosa hayo yalifanyika mwaka 2022 na 2023 huko Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso, ambapo Mara alikuwa ameajiriwa na ubalozi wa Marekani.
Kulingana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani, unyanyasaji huo ulitokea katika nyumba iliyokodishwa kwa wanadiplomasia huyo wa Marekani.
Kwa sababu jengo hilo lilitengwa kwa matumizi rasmi, iliangukia chini ya mamlaka ya Marekani, na hivyo kuruhusu mamlaka ya Marekani kushtaki kesi hiyo.
Ripoti zinasema waathiriwa hao wawili, ambao walikuwa na umri wa miaka 13 na 15 wakati unyanyasaji ulipoanza, na alitoka katika mazingira magumu. Waendesha mashtaka walisema Mara alitumia vibaya mazingira yao kwa muda wa takriban mwaka mmoja.A
“Uhalifu wake ulikuwa kitu kibaya. Ingawa hakuna hukumu ambayo ingeweza kuondoa madhara aliyosababisha, uamuzi wa leo unaonyesha kwamba wale wanaowanyanyasa watoto – ndani au nje ya nchi – watakabiliwa vilivyo na mfumo wa sheria Marekani,” alisema Naibu Mwanasheria Mkuu A Tysen Duva.
Alitumia ugonjwa unaohatarisha maisha wa mama wa wasichana huyo kama fursa ya kudai ngono, akiwaambia hangeweza kuwasaidia bila kupokea kitu kama malipo, ilisema Ofisi ya Masuala ya Umma.
Mara alikuwa amewapa wasichana hao simu ili aweze kuwapigia wakati mkewe ameenda kazini, iliongeza.
Pia alihukumiwa kwa kutuma jumbe chafu za ngono kwa mmoja wa wasichana na kujaribu kumshawishi mfanyakazi wa ndani kuwapotosha wachunguzi.
Kesi hiyo ilichunguzwa na mamlaka ya Marekani kwa usaidizi kutoka Burkina Faso.
Pakistan iko ‘vitani’ na Afghanistan – Waziri wa ulinzi

Waziri wa ulinzi wa Pakistan amesema nchi hiyo iko katika “vita vya wazi” na Afghanistan, baada ya kuanzisha mashambulizi ya anga huko Kabul kama sehemu ya wimbi la mashambulizi kote nchini humo.
“Uvumilivu wetu sasa umekwisha,” alisema Khawaja Muhammad Asif kufuatia mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo yalitokea baada ya Taliban wa Afghanistan kutangaza shambulio kubwa dhidi ya vituo vya kijeshi vya Pakistan karibu na mpaka Alhamisi usiku.
Mashambulizi ya hivi karibuni yanafuatia miezi kadhaa ya mapigano kati ya mataifa hayo mawili jirani, licha ya kukubaliana kusitisha mapigano mpango ambao ulikuwa dhaifu mnamo mwezi Oktoba.
Mazungumzo ya mwaka jana yalishindwa kufikia makubaliano mapana kukomesha kabisa uhasama, huku pande zote mbili zikilaumiana kwa kutochukulia mazungumzo hayo kwa uzito mkubwa.
Bill Clinton kutoa ushahidi wa kibinafsi kwa Bunge kuhusu Epstein

Rais wa zamani Bill Clinton anatarajiwa kutoa Ushahidi siku ya Ijumaa faraghani, kwa jopo la bunge kuhusu uhusiano wake na marehemu Jeffrey Epstein, mhalifu wa kingono.
Ushahidi wa Clinton, uliopangwa kufanyika saa tano asubuhi ET (16:00 GMT), unafuata ule wa mkewe, Katibu wa zamani wa Mambo ya Nje Hillary Clinton, ambaye aliiambia Kamati ya Uangalizi ya Baraza la Bunge la Wawakilishi siku ya Alhamisi kwamba hakumbuki kukutana na Epstein na hakuwa na chochote cha kushirikisha kuhusu sakata ya uhalifu wa kingono ya Epstein.
Bill Clinton alisafiri kwa ndege ya Epstein mara kadhaa mwanzoni mwa miaka ya 2000 baada ya kuondoka madarakani, na sehemu ya mamilioni ya nyaraka zilizotolewa na Idara ya Sheria zinajumuisha picha zake akiwa na wanawake ambao nyuso zao zimefutwa. Amekana kufanya makosa na ameelezea kujutia uhusiano wake na Epstein.
Mwenyekiti wa jopo la Republican, Mwakilishi James Comer wa Kentucky, anasema Bill Clinton na mkewe hawashutumiwi kwa makosa lakini lazima wajibu maswali kuhusu uhusiano wao na Epstein katika shirika lao la hisani.
Walikubali kutoa ushahidi karibu na makazi yao makuu ya Chappaqua, New York, baada ya Baraza la Bunge la Wawakilishi kutishia kuwachukulia hatua kwa kukataa kutoa ushirikiano. Baadhi ya Wademocrats waliunga mkono hatua hiyo.
Waghana takriban 55 wameuawa katika vita vya Urusi na Ukraine, Waziri asema

Takriban Waghana 55 wameuawa wakipigana vitani nchini Ukraine, huku wengine wawili wakishikiliwa kama wafungwa wa kivita, waziri wa mambo ya nje wa Ghana amesema.
Katika safari yake kwenda Kyiv, Samuel Okudzeto Ablakwa alisema kwamba takriban Waghana 272 wanaaminika kushawishiwa kuingia katika mzozo huo tangu 2022, akirejelea mamlaka ya Ukraine.
Ablakwa alielezea takwimu hizo kama “zinazohuzunisha na kutisha,” akisema Ghana “haiwezi kufumbia macho takwimu hizi za kuvunja moyo”.
Hakusema ni upande gani ambao Waghana walikuwa wakipigana lakini waziri wa mambo ya nje wa Ukraine alisema Jumatano kwamba zaidi ya watu 1,700 kutoka nchi 36 barani Afrika wamesajiliwa kupigania Urusi.
Waghana 55 ndio idadi kubwa zaidi ya majeruhi kutoka nchi moja ya Afrika kuthibitishwa rasmi katika vita vya Ukraine na Urusi.
Vyombo vya habari vya ndani nchini Cameroon vimeripoti kwamba raia wake 94 wamekufa katika mzozo huo, lakini mamlaka hazijatoa maoni yoyote kuhusu takwimu hizi.
Waafrika Kusini wawili na takriban Mkenya mmoja wamefariki katika mzozo huo.
Ablakawa alisema takwimu za majeruhi “sio tu idadi, zinawakilisha maisha ya binadamu, matumaini ya familia nyingi za Ghana na taifa letu”.
Alisema serikali ya Ghana imejitolea “kufuatilia na kusambaratisha mipango yote ya usafirishaji watu kwa njia haramu” pamoja na kuanzisha kampeni kali za uhamasishaji umma ili kuzuia vijana wa nchi hiyo kuingizwa kwenye mzozo huo.
“Hii si vita yetu na hatuwezi kuruhusu vijana wetu kuwa ngao za kibinadamu kwa wengine,” aliongeza.
Siku ya Alhamisi, raia wa Kenya alishtakiwa kwa tuhuma za kuwashawishi vijana wa kiume kwenda Urusi na ajira za kazi, lakini wakaishia kupigana nchini Ukraine. Festus Arasa Omwamba alikana mashtaka hayo.
Jumla ya Wakenya 1,000 wamesajiliwa kupigania Urusi katika vita vyake vya miaka minne dhidi ya Ukraine, ilisema ripoti kutoka kwa Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi ya Kenya (NIS), iliyotolewa wiki iliyopita.
Ubalozi wa Urusi nchini Kenya umekanusha madai kwamba ulihusika katika kuwasajili watu kupigana vitani.
Hata hivyo, ilisema kwamba sheria ya Urusi iliwaruhusu raia wa kigeni waliopo nchini humo kisheria kujiunga na jeshi kwa hiari.
Siku ya Jumatano, waziri wa mambo ya nje wa Ghana alimhimiza Rais Volodymyr Zelensky kuwaachilia huru wafungwa wawili wa kivita wa Ghana waliokamatwa wakipigania Urusi.
“Wao ni waathiriwa wa udanganyifu, taarifa za uongo, taarifa potofu, na mitandao ya biashara haramu ya wahalifu,” alisema.
Aliishukuru Ukraine kwa kuhakikisha sheria za kimataifa zinaheshimiwa katika kuwashughulikia wafungwa.
“Tumepokea ripoti kwamba wako katika afya njema,” alisema. “Hawajateswa. Hawajatendewa ukatili tangu walipokamatwa.”
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andriy Sybiga alisema pande zote mbili zilijadili “kwa uwazi” kuhusu uwezekano wa kuwarudisha wafungwa hao Ghana.
Pakistan yazuia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika miji muhimu – Waziri wa Habari

Waziri wa Habari wa Pakistani Atta Tarar ameandika kwenye Twitter kwamba Pakistan imezuia majaribio ya Taliban wa Afghanistan ya kurusha ndege ndogo zisizo na rubani kushambulia maeneo yao lengwa huko Abbottabad, Swabi na Nowshera.
“Mifumo ya Kupambana na Ndege Zisizo na Rubani imedondosha ndege zote zisizo na rubani. Hakuna aliyepoteza maisha,” ujumbe wake wa Twitter uliongeza.
Abbottabad ni mji wa kijeshi wenye chuo cha kijeshi cha Jeshi la Pakistani.
Kauli ya Tarar inakuja baada ya msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Taliban, Zabihullah Mujahid, kudai kuwa ameanzisha “mashambulizi ya anga” kulenga kambi ya kijeshi karibu na Faizabad huko Islamabad, kambi ya kijeshi huko Nowshera, maeneo ya kijeshi huko Jamrud, na maeneo mengine huko Abbottabad.
Taarifa ya Taliban iliongeza kuwa “operesheni ya angani ilitekelezwa kwa mafanikio, ikilenga kambi muhimu za kijeshi za Pakistani, vituo vya kutoa amri, na vifaa vya kimkakati. Mashambulizi hayo yalifanywa kujibu mashambulizi ya angani yaliyofanywa jana usiku na vikosi vya Pakistani huko Kabul, Kandahar na Paktia.
Afghanistan yasema ilitumia ndege zisizo na rubani kushambulia Pakistan

Awali, Wizara ya ulinzi na msemaji wa serikali wa Afghanistan walisema kuwa “wamefanikiwa kufanya” mashambulizi ya angani kwa kutumia ndege zisizo na rubani kushambulia maeneo ya kijeshi nchini Pakistan.
Mashambulizi ya Pakistan katika majengo ya serikali yapitisha ujumbe mzito – Mtaalam

Wakati huohuo, mashambulizi ya Pakistan ya safari hii yamelenga vituo vya serikali vya Taliban badala ya maeneo ya kigaidi nchini Afghanistan, Michael Kugelman, mjumbe mwandamizi wa Asia Kusini katika Baraza la Atlantiki, aliambia kipindi cha Newsday cha BBC.
Hii ina maana kwamba “sasa inalenga utawala wenyewe”, alisema.
Pakistan inadai kwamba Taliban wa Afghanistan wanawahifadhi magaidi ili kufanya mashambulizi dhidi ya Pakistan. Ingawa kumekuwa na hatua za kidiplomasia zilizochukuliwa ili kupunguza mvutano huo, hazijaleta suluhisho la kudumu.
Wakati huo huo kauli mbiu kutoka kwa Taliban zinaonyesha kuwa imejitolea “kufanya mashambulizi yasiyokoma” upande wa mpaka wa Pakistan, alisema, akiongeza kuwa hii ilikuwa “hatari” na inaweza kusababisha mzozo huo kutanuka.
Katika Picha: Kadinali Pengo aagwa Dar es Salaam Tanzania

Waumini wa Kanisa Katoliki, jamaa na waombolezaji kwa jumla wanahudhuria misa ya kuuaga mwili wa Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu jijini Dar es Salaam Tanzania.
Marehemu Kardinali Pengo atazikwa huko Pugu Jumamosi Februari 28, 2026.





Melezo zaidi:
Wairan wengi wanakabiliwa na adhabu ya kifo kwa maandamano – Mkuu wa haki za binadamu wa UN

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk siku ya Ijumaa ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa matumizi ya adhabu ya kifo nchini Iran, akionya kwamba watu wengi zaidi wako hatarini kunyongwa baada ya hukumu ya kwanza ya kifo inayohusishwa na maandamano makubwa ya Januari kutolewa wiki hii.
“Nimeshtushwa na ripoti kwamba takriban watu wanane, wakiwemo watoto wawili, wamehukumiwa kifo kutokana na maandamano hayo,” Turk alisema katika hotuba yake kwa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva, akiongeza kuwa watu wengine 30 walionekana kuwa katika hatari ya kuhukumiwa kifungo hicho.
Mahakama ya mapinduzi mjini Tehran ilitoa hukumu ya kifo kwa mwanamume mmoja wa Iran anayetuhumiwa kwa “uadui dhidi ya Mungu” ambayo ikithibitishwa itakuwa hukumu ya kwanza kama hiyo inayohusishwa na maandamano makubwa ya mwezi Januari, chanzo kilicho karibu na familia ya mwanamume huyo kilisema.
Makundi ya haki za binadamu yanasema maelfu ya watu waliuawa katika msako mkali dhidi ya maandamano hayo, machafuko mabaya zaidi ya ndani nchini Iran tangu enzi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979. Wakati wa machafuko hayo, Rais wa Marekani Donald Trump aliionya Tehran kwamba anaweza kuagiza hatua za kijeshi ikiwa itatekeleza mauaji.
“Nina wasiwasi sana kuhusu uwezekano wa kuongezeka kwa jeshi la kikanda na athari zake kwa raia, na natumai sauti ya mantiki itashinda,” Turk alisema katika hotuba hiyo hiyo.
Oman ambayo ni mpatanishi ilisema mazungumzo mjini Geneva siku ya Alhamisi kati ya Marekani na Iran yalipiga hatua kuhusu mpango wa nyuklia wa Tehran, lakini hakukuwa na dalili yoyote ya mafanikio ambayo yangeweza kuzuia mashambulizi ya Marekani huku kukiwa na ongezeko kubwa la kijeshi.
Afghanistan na Pakistan lazima zifuate sheria za kimataifa – UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, pamoja na Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, wameeleza msimamo wao kuhusu hali ya hivi karibuni ya mvutano na mapigano kati ya Pakistan na Afghanistan.
Guterres amezihimiza nchi hizo mbili kuzingatia kikamilifu wajibu wao chini ya sheria za kimataifa, hususan sheria za kimataifa za haki za binadamu.
Kwa upande wake, Volker Turk ametoa wito kwa Afghanistan na Pakistan kufanya mazungumzo ya pamoja ili kutatua matatizo yaliyotokana na mapigano ya mpakani na mashambulizi mabaya ya anga yaliyoleta vifo.
Inafaa kufahamika kuwa Pakistan imedai kwamba baada ya mashambulizi “yasiyochokozwa” kutoka kwa Taliban wa Afghanistan, ililenga vituo vya ulinzi vya Taliban katika miji ya Kabul, Paktia na Kandahar, na kuua wanachama 133 wa utawala wa Taliban wa Afghanistan pamoja na kuwajeruhi zaidi ya 200.
Hata hivyo, BBC haijaweza kuthibitisha madai hayo kwa njia huru.
Iran yajitolea kupatanisha Pakistan na Afghanistan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, amesema kuwa Iran iko tayari kuwezesha mazungumzo kati ya Pakistan na Afghanistan.
Katika taarifa aliyochapisha kwenye mtandao wa X, alisema: “Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambao ni mwezi wa kujizuia na kuimarisha mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu, inafaa Afghanistan na Pakistan kushughulikia na kutatua tofauti zao za sasa kwa kuzingatia ujirani mwema na kupitia mazungumzo.”
Alisema Iran iko tayari kutoa kila aina ya msaada ili kuwezesha mazungumzo kati ya nchi hizo mbili na kuimarisha uelewano pamoja na ushirikiano.
Iran tayari ilikuwa imewahi kujitolea kupatanisha nchi hizo mbili hapo awali wakati mvutano wa mpakani ulipokuwa unaongezeka.
China yataka Pakistan na Afghanistan kumaliza mzozo kupitia mazungumzo

China imezitaka Afghanistan na Pakistan kutatua mgogoro wao kwa njia ya mazungumzo, ikisema kumaliza uhasama ni kwa maslahi ya wananchi wa nchi zote mbili.
Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema inaeleza “wasiwasi mkubwa” kuhusu kuongezeka kwa mvutano katika mpaka wa Afghanistan na Pakistan, na kuzipa wito nchi hizo “kutatua tofauti na migogoro yao kupitia mazungumzo na majadiliano.”
Wizara hiyo iliongeza kuwa China “inafanya juhudi za upatanishi kwa kutumia rasilimali zake yenyewe katika mgogoro huo, na iko tayari kuchukua jukumu la kujenga katika kupunguza mvutano na kuboresha uhusiano wa pande mbili.”
“Kama jirani na rafiki, China ina wasiwasi mkubwa kuhusu mvutano huu na inasikitishwa na vifo vilivyotokea katika mzozo huu. Ongezeko lolote la hali ya taharuki litaleta madhara na hasara kwa pande zote,” alisema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa kumaliza mapigano ni “kwa maslahi ya msingi ya nchi zote mbili na wananchi wake, na kutasaidia kudumisha amani na utulivu katika eneo hilo.”
Taliban wa Afghanistan wadai kuwaua askari 50 wa Pakistan

Mamlaka ya Taliban nchini Afghanistan imesema kuwa imefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya vituo vya mpaka vya Pakistan mashariki na kusini-mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa serikali ya Taliban, Zabiullah Mujahid, aliliambia Shirika la Utangazaji la BBC kwamba vikosi vya Afghanistan viliharibu vituo 19 vya mpaka vya Pakistan na kuwakamata wanajeshi kadhaa wa Pakistan.
Aidha, alidai kuwa zaidi ya wanajeshi 50 wa Pakistan waliuawa.
Hata hivyo, hakuna uthibitisho huru uliotolewa kuthibitisha takwimu hizo.
Kwa upande wake, Pakistan imedai kuwa imeharibu vituo 27 vya mpaka vinavyomilikiwa na Taliban wa Afghanistan, na kusema kuwa imewasababishia hasara kubwa wanamgambo wa Taliban.
Africa CDC yaonya kuhusu usalama wa takwimu katika mikataba ya afya kati ya Afrika na Marekani

Kuna masuala makubwa katika makubaliano ambayo Marekani inafanya na nchi za Afrika kuhusu namna ufadhili wake wa kimataifa wa afya utakavyotekelezwa kuanzia sasa, amesema Mkuu wa Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) Alhamisi.
“Kuna wasiwasi mkubwa kuhusu matumizi ya takwimu na kuhusu ushirikishwaji wa vimelea vya magonjwa,” alisema Mkurugenzi Mkuu Jean Kaseya katika mkutano na wanahabari uliofanyika kwa njia ya mtandao.
Jumatano, Zimbabwe ilijiondoa katika mazungumzo na Marekani kuhusu makubaliano yenye thamani ya dola milioni 367 kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, ikieleza wasiwasi kuhusu usalama wa taarifa nyeti na kudai kuwa makubaliano hayo hayakuwa ya usawa. Serikali ya Zambia nayo ilisema imepinga kipengele fulani katika makubaliano yake.
Makubaliano hayo ni sehemu ya mfululizo wa mikataba ya nchi mbili inayobadili namna utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump unavyotoa mabilioni ya dola za ufadhili wa afya duniani. Hatua hizo zinafuatia kuvunjwa kwa shirika la misaada la Marekani mwaka jana, kupunguzwa kwa ufadhili na mikataba duniani kote, pamoja na ahadi ya kuweka “Marekani Kwanza” katika mkakati wake wa afya ya kimataifa.
Hata hivyo, Kaseya alisema taasisi hiyo imekuwa ikiunga mkono nchi wanachama pale zinapoomba msaada, na itaendelea kutoa ushauri iwapo zitahitaji kujadiliana upya na Marekani, pamoja na kuzisaidia kutekeleza makubaliano yoyote zitakayokubaliana nayo.
“Niliambia nchi zangu zote, mnaungwa mkono kikamilifu na Africa CDC. Hata kama mnataka kutathmini upya mikataba na Marekani… mkihitaji Africa CDC iwepo, tutakuwepo,” alisema.
Kwa mujibu wa ubalozi wa Marekani, tayari nchi 16 za Afrika zimesaini mikataba kama hiyo yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 18.3.
Epstein alijaribu kununua jumba la kifahari huko Morocco siku chache kabla ya kukamatwa kwake 2019

Jeffrey Epstein alijaribu kununua jumba la mamilioni ya dola huko Morocco siku moja kabla ya kukamatwa kwake mnamo 2019, kulingana na hati zilizotolewa na Idara ya Sheria ya Marekani mwezi uliopita.
Epstein alitaka kumiliki Bin Ennakhil tangu 2011, lakini mizozo na muuzaji kuhusu bei na mpangilio wa ununuzi iliendelea kwa miaka kadhaa.
Jumba la kifahari katika kitongoji cha kifahari cha Palmeraie cha Marrakech limefafanuliwa kuwa kazi bora ya usanifu, iliyojengwa na mafundi 1,300 na kuangazia nakshi na vinyago vya kupendeza.
Epstein alitia saini uhamisho wa kielektroniki wa $14.95m (£11m) tarehe 5 Julai 2019, siku moja kabla ya kukamatwa kwake, kufuatia makubaliano ya kununua kampuni ya kigeni iliyomiliki mali hiyo kwa €18m (£13.3m).
Kulingana na hati zilizotolewa, uhamisho huo ulikuwa shughuli kuu ya mwisho ya kifedha ya Epstein katika kipindi hicho kabla ya kukamatwa kwake na mamlaka ya Marekani kwa mashtaka ya biashara ya ngono aliporejea New York.
Siku tatu baada ya kukamatwa, mhasibu wa Epstein Richard Kahn alighairi uhamisho wa kielektroniki na ununuzi wa jumba hilo la kifahari haukukamilika .
Ukraine: Zaidi ya waafrika 1,700 wanapigana kwa niaba ya Urusi

Zaidi ya Waafrika 1,700 wanapigana upande wa Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Andrii Sybiha, alisema Jumatano, akiongeza kuwa Moscow inatumia udanganyifu kuwashawishi kujiunga na mapigano hayo.
Akizungumza pamoja na mwenzake wa Ghana, Sybiha alisema mazungumzo yanaendelea na serikali mbalimbali barani Afrika ili kuzuia raia wao kuhadaiwa katika mipango hiyo. Ghana itakuwa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mwaka ujao.
“Tunaona wazi kuwa Urusi inajaribu kuwahadaa raia wa Afrika kuingia katika vita vya maangamizi,” Sybiha aliambia mkutano na wanahabari. “Kwa mujibu wa takwimu zetu, kwa sasa kuna zaidi ya raia 1,780 kutoka bara la Afrika wanaopigana katika jeshi la Urusi.”
Aliongeza kuwa wapiganaji hao wanatoka katika nchi 36 tofauti za Afrika.
Mamlaka za Urusi zimekanusha madai ya kuwaajiri kinyume cha sheria raia wa Afrika kujiunga na majeshi yake.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Samuel Okudzeto Ablakwa, alisema wengi wa Waafrika wanaopigana kwa niaba ya Urusi ni waathiriwa waliotapeliwa, wakihadaiwa kupitia mtandao wa siri (dark web) kwa ahadi za ajira za kawaida.
“Hawana historia ya kiusalama. Hawana uzoefu wa kijeshi. Hawajapata mafunzo,” alisema Ablakwa. “Walishawishiwa na kudanganywa, kisha wakawekwa mstari wa mbele vitani.”
Ablakwa alionesha mshikamano wake na Ukraine na akatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano ili kumaliza vita hivyo, ambavyo vilitimiza miaka minne tangu kuanza kwake Jumanne. Alisema atamwomba Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, kuwaachilia huru raia wawili wa Ghana waliotekwa wakiwa wanapigana upande wa Urusi.
Aidha, Ablakwa alisema Ghana itahamasisha kampeni za uelimishaji wa umma kuhusu mitandao ya usafirishaji haramu wa watu inayowadanganya Waafrika kujiunga na majeshi ya Urusi, wakati wa uongozi wake katika Umoja wa Afrika.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.