Kipawa ni ramani yako

Lakini yule mtunza bustani akasema naomba unipe mwaka mmoja tena nitauwekea mbolea na kuumwagilia
Nini maana yake ; nikasema Bustani ni mfano Mwenye bustani ni Yesu
Mtunza bustani ni mtumishi anaeongoza kanisa yaani mchungaji
Mti aina ya mtini ni moja kati ya muumini ambaye yeye husikia neno wala halifanyii kazi
Mungu anataka baada ya kuokoka ufundishwe neno na baada ya kulijua wewe nawe uwe sasa mwalimu wa kulisema na kulitenda neno
Usiwe mbinafsi
Usiwe mchoyo
Usiwe mgumu kutoa mbele za Bwana
Nimeanza na kukumbusha hilo kwakua somo la leo liko pia hapo
Mtu anaweza kuniuliza nitatoaje wakati sina cha kutoa?
Nakuja sasa kwenye somo
Mungu alipo muumba mwanadamu aliweka kipawa ndani mwako Lkn leo hii mambo yamekuwa tofauti kwa watu wengi wamekua wakiwaza kusoma na kutumia mbinu ambazo si mkakati wa kiMungu na ndio maana wengi hamfanikiwi
Sikiliza nikwambie wote matajiri duniani ni watu wenye vipawa
Kipawa ndio uthamani wako
Kama ni Elimu kila mmoja anaweza akasoma lkn kipawa sio tena kusoma kipawa ni kitu cha tofauti ambacho hakifanani na mtu mwingine wala hakisomewi sehemu yoyote bali ni zawadi ambayo Mungu humpa kila mmoja
Unaweza ukawa na kipawa cha kuimba ukakizarau na kuona hakiwezi kukufikisha mahali lkn Mungu ndie alikupa hicho kama ramani ya maisha yako
Una kipawa cha uandishi,ualimu,uhandisi,ukulima na vingine vingi sana kila mmoja na cha kwake
Utakapo kifanya wewe sivyo kama atakavyo fanya mwingine ww ni zaidi ya kila mmoja . Mungu alimuumba mwanadamu ili aje kuwa ni suruhisho kwa maisha ya mwingine
Yaani wewe unategemewa na mtu mwingine ili maisha yake yaende
Waliamua kumjaribu Mungu kwa kidogo walichonacho
Sikiliza Mungu anapenda watu wenye imani watu ambao hawaogopi watu wanaoamua kufanya kwa moyo. Kama wewe ni muoga maendeleo utayasikia kwa wenzako.


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment