Wakimbizi wamenasa kwenye mduara wa migogoro na majanga

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Viongozi mbalimbali wa dunia wakishiriki vikao vya awali kuelekea Mkutano wa Kilele wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP30) unaofanyika mjini Belem nchini Brazil.Picha: Ludovic Marin/AFP

Umoja wa Mataifa umesema mamilioni ya wakimbizi wamekwama kwenye mduara wa papo kwa papo wa migogoro na majanga makubwa ya kimazingira.

Wakati washiriki wapatao 50,000 kutoka mataifa zaidi ya 190 wakianza mkutano mkubwa kabisa wa mabadiliko ya tabianchi, COP30, katika mji wa Belem nchini Brazil siku ya Jumatatu (Novemba 11), Umoja huo ulitowa wito kwa washiriki wamkutano wa kilele kutoa ufadhili kwa mataifa yaliyo hatarini zaidi.

Shirika la wakimbizi la Umoja huo, UNCHR, lilisema kwamba ndani ya kipindi cha miaka 15 ijayo, maeneo yanayowahifadhi takribani nusu ya wakimbizi duniani yatakuwa yamekabiliwa na hali mbaya kabisa kutokana na mabadiliko ya tabianchi.

Ripoti iliyotolewa na shirika hilo ilisema matatizo yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi “yanaongeza mahitaji ya kibinaadamu na hatari ya watu kuendelea kuwa wakimbizi.”

Shirika hilo liliongeza kuwa ufikia katikati ya mwaka 2025, watu milioni 117 walikuwa wamegeuzwa wakimbizi kutokana na vita, machafuko na mauaji, ambapo watatu katika kila wanne miongoni mwao wanaishi kwenye nchi zinazokabiliwa na majanga makubwa ya kimazingira. 

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment