Maandamano baada ya uchaguzi yaendelea kusambaa Tanzania

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na: Cantona Joseph|RFA

Waandamanaji nchini Tanzania wanaipinga serikali ya Rais Samia Suluhu HassanPicha: AP Photo/picture alliance

Mamia ya waandamanaji wamejitokeza kwenye miji kadhaa nchini Tanzania katika siku ya pili ya maandamano yaliyoibuka wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 29.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeripoti kuwa watu wawili wameuawa katika vuguvugu hilo wakati taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa zikisema watu wengi wameuawa. Amnesty limetoa wito wa kuanzishwa uchunguzi kuhusu matumizi ya nguvu kubwa yanayodaiwa kufanywa na polisi dhidi ya waandamanaji.

Risasi na mabomu ya machozi vyarindima

Awali Polisi jijini Dar es Salaam waliwafyatulia risasi na mabomu ya machozi waandamanaji. Duru za habari zinasema waandamanaji kadhaa wamejeruhiwa katika mji wa Namanga mpakani na Kenya. Katika uchaguzi wa Oktoba 29 uliotawaliwa maandamano na ghasia, Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, anawania kuiongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment