Makubaliano ya kusitisha mapigano ni hatua ya mafanikio, lakini vita bado havijakwisha

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Huu ni ushindi mkubwa wa kidiplomasia

Na:Cantona Joseph|RFA

Mkataba wa kusitisha mapigano na kuachilia mateka kati ya Israel na Hamas, uliotangazwa baada ya mazungumzo makali nchini Misri, ni mafanikio yanayosubiriwa kwa muda mrefu ambayo yanawaleta karibu na kumaliza vita vilivyodumu kwa miaka miwili huko Gaza.

Lakini, licha ya kasi, hakuna uhakika kwamba hili litatokea.

Tofauti kuu katika juhudi hizi imekuwa ni ushiriki wa binafsi wa Rais Donald Trump, ambaye ameweka shinikizo sio tu kwa Hamas bali pia kwa Israel kwa makubaliano.

Huu ni ushindi mkubwa wa kidiplomasia kwa mtu ambaye anataka kuonekana kama mtu aliyemaliza vita na katika mchakato huo, atalipwa kwa hilo.

Israel ilianzisha vita huko Gaza kujibu mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba 2023, wakati karibu watu 1,200 waliuawa, wengi wao wakiwa raia wa Israeli, na 251 walichukuliwa mateka.

Mashambulizi ya kijeshi ya Israel yamewaua zaidi ya Wapalestina 67,000, wengi wao wakiwa raia na wakiwemo watoto zaidi ya 18,000, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas.

Takwimu zake zinaonekana kuwa za kuaminika na UN na mashirika mengine ya kimataifa.

Imeharibu sehemu kubwa ya eneo hilo na kusababisha janga kubwa la kibinadamu. Kilichokubaliwa ni awamu ya kwanza ya mpango ambao rais alitangaza katika Ikulu ya White House wiki iliyopita pamoja na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambaye ameshutumiwa kuhujumu juhudi za mapatano huko nyuma.

Wakati huu, Trump, ambaye ameripotiwa kutokuwa na subira na kukerwa na Netanyahu, anaonekana kutumia uwezo walionao Wamarekani pekee kuishawishi Israel, na kumuacha waziri mkuu huyo akiwa hana chaguo zaidi ya kujihusisha na mchakato huo.

Lakini Netanyahu bado anakabiliwa na vikwazo vya kisiasa.

Anategemea uungwaji mkono wa mawaziri wasiopenda siasa kali ambao wametishia kujiondoa katika muungano huo,”kujiondoa kwenye muungano iwapo kutakuwa na makubaliano.”ambayo yanaweza kusababisha kusambaratika kwa serikali, wasiwasi ambao wengi wanashuku umemsababisha kurefusha vita.

Ameahidi kupata “ushindi kamili” dhidi ya Hamas, na makubaliano yoyote yatalazimika kumruhusu kusema amefanikisha hilo.

“Netanyahu ameita tangazo hilo kuwa ‘ushindi wa kidiplomasia, kitaifa na wa maadili kwa Taifa la Israeli’. Cha kushangaza, tofauti na Hamas, taarifa yake haikusema kwamba vita vitakwisha.”

Rais wa Madagascar aomba mwaka mmoja kutatua matatizo akishindwa atajiuzulu

Maandamano

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ameomba muda wa mwaka mmoja kurekebisha changamoto za nchi hiyo, na kuahidi kuwa iwapo zitaendelea, atajiuzulu.

Alisema hayo wakati wa mkutano katika ikulu yake na makundi mbalimbali ya wafuasi wa serikali.

Wahudhuriaji wengi walipata fursa ya kumuuliza rais maswali au kuchangia maoni yao tu, ambapo alijibu.

“Sitaki kubembeleza nataka kusikia ukweli, ni watu waliokuwa wakiniambia kila kitu kiko sawa ndio wanahusika na hali yetu ya sasa,” alisema.

Vuguvugu la maandamano hayo, linalojulikana kama Gen Z Mada. limekuwa likitoa wito kwa rais kujiuzulu na kukataa mwaliko wa kuhudhuria mazungumzo hayo.

Wanasema kuwa hawawezi kushirikisha serikali ambayo imekuwa ikiwakandamiza kwani wanadai haki za msingi za binadamu.

Kundi hilo limeitisha maandamano mapya siku ya Alhamisi. “Tunakataa mwaliko wa rais kwenye mazungumzo. Hatutashiriki mazungumzo na utawala unaokandamiza, kuwashambulia na kuwadhalilisha vijana wake mitaani,” waliandika kwenye ukurasa wao wa Facebook.

Israel, Hamas, Trump wamesema nini?

Wakazi wa Gaza

Israel;

Ni siku nzuri kwa Israel,” Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema katika taarifa yake.

Aliwashukuru wanajeshi wa Israel na Rais wa Marekani Donald Trump na timu yake “kwa uhamasishaji wao kwa kazi hii takatifu ya kuwaachilia mateka wetu”, akimaanisha Waisraeli wanaoshikiliwa na Hamas huko Gaza kwa sasa.

“Kwa msaada wa Mungu tutawaleta wote nyumbani,” anaongeza

Trump;

Rais wa Marekani aliandika katika taarifa yake jana usiku kwamba: “Hii ni siku kubwa kwa Ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu, Israel, Mataifa yote yanayoizunguka, na Marekani, na tunawashukuru wasuluhishi kutoka Qatar, Misri na Uturuki, walioshirikiana nasi kufanikisha Tukio hili la Kihistoria na lisilokuwa na Kifani.

Baadaye aliiambia Fox News kwamba Gaza “itajengwa upya” baada ya awamu ya kwanza ya mpango huo kutekelezwa na kuongeza kuwa “itakuwa mahali salama zaidi” baadaye.

Hamas;

Kwa mujibu wa mshirika wa BBC wa shirika la habari la Marekani CBS, Hamas ilisema makubaliano hayo “yatamaliza vita dhidi ya Gaza, kuhakikisha uondoaji kamili wa vikosi vya uvamizi, kuruhusu kuingia kwa misaada ya kibinadamu, na kutekeleza kubadilishana wafungwa”

Watu wa Gaza “wameonesha ujasiri, heshima na ushujaa usio kifani”, iliongeza “Hatutaacha kamwe haki za kitaifa za watu wetu hadi uhuru upatikane,” ilisema.

Ulimwengu waguswa na hatua ya kwanza ya makubaliano ya amani ya Gaza

Wakazi wa Gaza

Viongozi wa dunia wamekaribisha kwa furaha habari kwamba Israel na Hamas wamekubaliana na awamu ya kwanza ya mpango wa amani wa Gaza.

Makubaliano hayo yanafungua njia ya kuachiliwa kwa mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina, kuondolewa kwa wanajeshi wa Israel kutoka Gaza na kuingia kwa misaada Gaza.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliyataja makubaliano hayo kuwa “siku kuu kwa Israel” na kusema serikali yake itakutana siku ya Alhamisi ili kuidhinisha.

Hamas ilisema mazungumzo hayo ni “ya kuwajibika na mazito” na kutoa wito kwa Marekani na wapatanishi wengine kuhakikisha kuwa Israel inatekeleza mapatano hayo “bila kukanusha au kuchelewa”.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alielezea mpango huo kama “fursa muhimu”, akiongeza kuwa Umoja wa Mataifa utaunga mkono “utekelezaji kamili” wa mpango huo, kuongeza utoaji wake wa misaada ya kibinadamu na kuendeleza juhudi zake za ujenzi mpya huko Gaza.

Guterres alizitaka pande zote kutii masharti ya mkataba huo, ikiwa ni pamoja na kuwaachilia mateka wa Israel, kutii usitishaji vita wa kudumu, na kuruhusu mara moja misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.

Nini kimekubaliwa kwenye mpango wa amani wa Gaza?

Athari za mashambulizi Gaza

Kama ambavyo tumekuwa tukiripoti, maelezo kamili ya mpango wa awamu ya kwanza wa kusitisha mapigano hayajafichuliwa rasmi.

Hivi ndivyo tunavyojua hadi sasa:

Chanzo cha habari cha Palestina kimeiambia BBC kwamba makubaliano hayo yanabainisha kuwa wafungwa 250 wa Kipalestina na Wagaza 1,700 wanaozuiliwa na wanajeshi wa Israel tangu vita hivyo kuanza wataachiliwa huru.

Chanzo hicho kilisema Hamas haijapokea orodha ya wafungwa wa Kipalestina ambao Israel inapanga kuwaachilia lakini suala hili linatarajiwa kutatuliwa ndani ya saa chache.

Afisa mkuu wa Palestina pia ameiambia BBC kuwa chini ya makubaliano hayo, Israel itaruhusu malori 400 ya misaada kuingia Gaza kila siku, na idadi hiyo ikiongezeka polepole katika hatua za baadaye.

Kwamujibu wa afisa wa Ikulu, Hamas itawaachilia mateka 20 walio hai wakati wa awamu ya kwanza ingawa ni mafanikio makubwa, mpango wa awamu ya kwanza ni mwanzo tu, sio mwisho.

Ni usitishaji vita, sio mpango wa amani, anaandika mwandishi wetu mkuu wa kimataifa Lyse Doucette.

Ethiopia yaishutumu Eritrea kwa kujiandaa kwa vita huku mvutano wa Bahari ya Shamu ukiongezeka

Gari la kivita

Ethiopia imeishutumu Eritrea kwa kujiandaa kuanzisha vita dhidi yake kwa kushirikiana na kundi la upinzani, katika ishara ya hivi punde ya kuongezeka kwa mvutano kati ya majirani hao wawili kuhusu udhibiti wa Bahari ya Shamu.

Tuhuma za Ethiopia zimo katika barua iliyotumwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje Gedion Timothewos kwa mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akionya kwamba njama hiyo imekuwa “dhahiri zaidi katika miezi michache iliyopita”.

Eritrea bado haijatoa maoni yoyote kuhusu barua hiyo, lakini uhusiano wake na Ethiopia umezidi kuwa mbaya katika miezi ya hivi karibuni.

Ethiopia imekuwa ikikusanya usaidizi ili kurejesha ufikiaji wa Bahari ya Shamu, na kusababisha hofu nchini Eritrea ilipochukua udhibiti wa ukanda wa pwani wakati wa uhuru mnamo 1993.

Ikiwa madai ya Gedion ni ya kweli, ina maana kwamba Eritrea inaendesha vita vya wakala dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ili kuizuia isifanye uvamizi wa kijeshi nchini Eritrea ili kukamata bandari zilizo kando ya Bahari ya Shamu.

Ethiopia na Eritrea zilipigania udhibiti wa mji wa mpaka wa Badme kutoka 1998 hadi 2000, na kusababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu.

Baada ya Abiy kuchukua madaraka mwaka wa 2018, alimaliza mvutano kwa kujenga muungano imara na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki.

Katika barua hiyo iliyoonwa na shirika la habari la AFP, Gedion alidai kwamba Eritrea na kundi lenye msimamo mkali la Tigray People’s Liberation Front (TPLF) walikuwa “wakifadhili, wakihamasisha na kuongoza makundi yenye silaha” katika eneo la Amhara nchini Ethiopia, ambako wanamgambo wanaojulikana kama Fano wamekuwa wakipambana na serikali ya shirikisho.

Trump asema awamu ya kwanza ya makubaliano ya amani ya Gaza yakubaliwa

Trump

Rais wa Marekani Donald Trump anasema awamu ya kwanza ya mkataba wake wa amani wa Gaza, kunamaanisha “Mateka wote wataachiliwa hivi karibuni.”

Kulingana na afisa mkuu wa Ikulu ya White House akizungumza na mshirika wa BBC wa Marekani, habari za CBS, mpango huo unakwenda kwa baraza la mawaziri la Israel siku ya Alhamisi.

Iwapo wataidhinisha rasmi mpango huo, Israel lazima iondoe wanajeshi wake kutoka Gaza hadi kwenye mstari uliokubaliwa, ambao afisa huyo anasema huenda ukachukua chini ya saa 24.

Mateka wanaoshikiliwa na Hamas huenda wataanza kuachiliwa kutoka Gaza siku ya Jumatatu, afisa mkuu wa Ikulu ya White House anaeleza.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema Umoja wa Mataifa utaunga mkono “utekelezaji kamili” wa makubaliano hayo pamoja na kuongeza utoaji wake wa misaada ya kibinadamu na kuendeleza juhudi zake za ujenzi mpya huko Gaza.

Guterres pia anazitaka pande zote kutii masharti ya mkataba huo ikiwa ni pamoja na kuwaachilia mateka wa Israel, kutii usitishaji vita wa kudumu, na kuruhusu mara moja misaada ya kibinadamu kuingia Gaza. “Mateso lazima yaishe,” Guterres anasema.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment