Takriban watu 600 waliuawa katika ghasia za kusini mwa Syria, shirika la uangalizi Syria lasema

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Maelezo ya picha,Mapigano hayo yalichochewa na mzozo kati ya jamii ya Bedouin na Druze

Kundi la uangalizi wa haki za kibinadamu nchini Syiria linasema watu 594 wameuawa wakati wa ghasia za hivi majuzi kusini mwa Syria ambazo zilichukua mwelekeo wa kidini.

Shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Syria lenye makao yake makuu nchini Uingereza (SOHR) liliandika kuhusu kuzuka kwa ukatili katika mauaji ambayo yamelikumba jimbo la Suweida tangu Jumapili.

Wanachama mia tatu wa kikundi cha jamii ya walio chache cha kidini cha Druze waliuawa, wakiwemo wapiganaji 146 na raia 154, 83 kati yao “waliuawa kwa ufupi” na vikosi vya serikali, SOHR lilisema Alhamisi jioni.

Takriban wafanyakazi 257 wa serikali na wapiganaji 18 wa Bedouin pia waliuawa, huku raia watatu wa Bedouin wakiuawa kwa jumla na wapiganaji wa Druze, liliongeza.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment