Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Ila tunatofautiana tu Viwango.
Kisaikolojia Ni Kuwa Kila Mwanadamu Ni MBINAFSI…
Ila tunatofautiana tu Viwango.
Ukitaka kuelewa hili angalia mkipiga picha ya pamoja (Group Photo)…
…Ukiipata unajiangalia wewe kwanza umetokeaje.
Kama umetokea vizuri hautajali kuna ambaye alifumba macho.
Au mdomo uko pembeni, UTAIPOST TU.
Kwenye maisha kuna watu wengi sana watakupush kufanya MAAMUZI ambayo yanawasaidia wao ila YAKUUMIZA WEWE.
Uwe makini sana na jambo hili.
Wengine ni watu wa karibu yako sana.
Watu ambao kila watakachokuwa wanataka ukifanye, kinawasaidia wao zaidi kuliko wewe.
Kuna watu wengi sana wamedumaa kwenye maisha kwa sababu ya kukubali kuwa na watu wa namna hii kwa muda mrefu.
Watu wa namna hii hawatakuja kukufikiria hata siku moja.
Watu hawa wakiona unaanza kutaka kusimama mwenyewe, wanachukia na wanaweza kuanza vita.
Uwe makini sana pale ambapo mtu wa namna hii anakuwa ni mtu wako wa karibu.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.