Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Mawaziri wa Jeshi la Ufaransa, Sébastien Lecornu, na wa Mambo ya Nje, Jean-Noël Barrot, wanatarajiwa siku ya Jumatatu, Desemba 30 mjini Beirut kwa ziara ya siku tatu kukutana na maafisa wa Lebanoni na kuutumia Mwaka Mpya pamoja na walinda amani wa Ufaransa wa UNIFIL waliotumwa kusini mwa Lebanoni. Kwa upande wa Lebanoni, ziara hii itakuwa fursa ya kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa Ufaransa ili kukomesha ukiukaji wa usitishaji mapigano wa Israel.

Sébastien Lecornu na Jean-Noël Barrot wanatazamiwa kukutana na mkuu wa jeshi la Lebanoni, Jenerali Joseph Aoun na mwakilishi wa Lebanoni ndani ya kamati ya ufuatiliajiwa wa usitishaji mapigano na Israel. Mikutano hii ni muhimu kwa sababu jeshi la Lebanoni limetakiwa kuchukua nafasi kubwa katika makubaliano ya kusitisha mapigano, kwa kutumwa kusini mwa Mto Litani kwenye mpaka na Israel.
Zoezi hili la kutumwa kwa wanajeshi wa Lebaoni haukukamilika zaidi ya mwezi mmoja baada ya kumalizika kwa mapigano. Linatatizwa na ukiukaji wa kila siku wa usitishaji mapigano ya jeshi la Israel, ambalo bado halijaondoka kabisa kusini mwa Lebanoni.
Ukiukaji mwingi
Ukiukaji huu, ambao umesababisha vifo vya takriban watu arobaini na karibu hamsini kujeruhiwa tangu kutangazwa kwa usitishaji mapigano, huchukua aina kadhaa. Kwa mfano, Waisraeli wanakataza wakazi wa vijiji vya mpakani kurudi nyumbani na kufanya uvamizi katika vijiji ambavyo hawakuwahi kufika hapo awali wakati wa vita.
Wakati wa operesheni hizi, jeshi la Israel linadai kuharibu miundombinu ya kijeshi ya Hezbollah. Viongozi wa kisiasa wa Lebanoni watawaomba mawaziri wa Ufaransa wanaozuru Beirut kuweka shinikizo ndani ya kamati ya ufuatiliaji wa usitishaji mapigano ili kuharakisha kuondoka kwa wanajeshi wa Israel na kuweza kutumwa kwa jeshi la Lebanoni.
All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.