Uganda-DRC: Museveni na Tshisekedi wanuia kuendeleza mapambano yao dhidi ya kundi la ADF

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Tshisekedi, alipokelewa siku ya Jumatano, Oktoba 30 mjini Entebbe na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni. Wawili  hao walijadili kwa kirefu operesheni ya pamoja ya kijeshi iliyotekelezwa na majeshi yao mawili mashariki mwa DRC dhidi ya kundi lenye silaha la asili ya Uganda ADF. Pia walizungumzia suala la kuongezeka kwa mvutano kati ya Kinshasa na Kigali, ikichochewa na maendeleo ya M23 huko Kivu Kaskazini.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amempokea rais wa DRC, Félix Tshisekedi, Oktoba 30, 2024.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amempokea rais wa DRC, Félix Tshisekedi, Oktoba 30, 2024. © Darko Vojinovic & Christophe Ena, AP – Montage AFP

Yoweri Museveni hajawahi kuchukua msimamo hadharani kuhusu mzozo kati ya Kinshasa na Kigali. Baadhi ya viongozi wa Kongo hata wanamshutumu rais wa Uganda kwa kuunga mkono M23. Kampala inajitetea na kudai kuunga mkono mazungumzo kati ya Kinshasa na M23. Lakini mwisho wa mkutano wake na Félix Tshisekedi mnamo Oktoba 30, hakujatajwa mada hii nyeti.

Akihitimisha mazungumzo yao, Yoweri Museveni alielezea mijadala hiyo kama “yenye ufanisi na yenye matumaini makubwa, kimsingi katika mchakato wa amani”. Sauti sawa ya matumaini kutoka kwa Rais wa Kongo Félix Tshisekedi, ambaye anaondoka Entebbe “kwa matumaini kwamba walichosema kitatimia” na anaeleza kwamba anategemea “hekima” ya mwenyeji wake.

Operesheni ya kuwasaka ADF inaendelea

Katika hatua nyingine, viongozi hao wawili wamethibitisha kuendelea kwa Operesheni Shujaa, iliyozinduliwa mwezi Novemba 2021 dhidi ya wapiganaji wa ADF, jina la kundi lenye asili ya Uganda, lenye mfungamano na kundi la Islamic State, linalohusika na mashambulizi mabaya na ambayo yanaenea Ituri na Kivu Kaskazini. Tathmini ya mfumo huu ilifanywa mwanzoni mwa mwezi na majeshi hayo mawili. Marais hao walionyesha kuridhishwa kwao na maendeleo ya kampeni hii.

Mwezi Septemba mwaka huu, operesheni ya pamoja ilisababisha kuachiliwa kwa angalau mateka tisa. Ikumbukwe, hata hivyo, kwamba ADF, kwa mujibu wa vyanzo vya Umoja wa Mataifa, inaendelea kuhusishwa na mauaji ya zaidi ya raia 340 tangu mwezi uni, na idadi kubwa ya watu huko Beni na Lubero ambapo wahanga 264 wamerekediwa. Vurugu hizi zinaambatana na maendeleo ya ADF katika maeneo ya uchimbaji madini ya eneo la Lubero.

Hatimaye, katika sulala la miundombinu, Yoweri Museveni alisisitiza dhamira yake ya kushiriki katika ujenzi wa barabara ya Kasindi-Beni-Butembo na, ikiwezekana, ujenzi wa barabara ya Bunagana-Rutshuru-Goma. Kauli iliokaribishwa na Félix Tshisekedi, ambaye anaona katika mpango huu kujumuika kwa DRC katika jumuiya ya Afrika Mashariki.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment