Korea Kaskazini yarusha kombora la masafa marefu katika Bahari ya Japani

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Korea Kaskazini imerusha “kombora la masafa marefu” siku ya Alhamisi, Oktoba 31, jeshi la Korea Kusini limesema, jaribio la kwanza la silaha la Pyongyang tangu Seoul ilipoishutumu kwa kutuma maelfu ya wanajeshi nchini Urusi.

Televisheni inaonyesha kombora la Korea Kaskazini likirushwa katika kituo cha treni cha Seoul, Oktoba 31, 2024.
Televisheni inaonyesha kombora la Korea Kaskazini likirushwa katika kituo cha treni cha Seoul, Oktoba 31, 2024. AP – Lee Jin-man

Jeshi la Korea Kusini lilionya siku moja kabla kwamba Korea Kaskazini, ikiwa na silaha za nyuklia, ilikuwa ikijiandaa kufanya majaribio ya kombora la balestiki lenye uwezo wa kuvuka mabara la ICBM, au hata kufanya jaribio la nyuklia, labda kabla ya uchaguzi wa urais nchini Marekani mnamo 5 Novemba.

Jeshi la Korea Kusini “limegundua kombora la balestiki lililorushwa kutoka ardhi ya Pyongyang kuelekea Bahari ya Mashariki mwendo wa saa 1:10 asubuhi (sawa na 12:10 mchana) leo,” makao makuu ya majeshi ya Korea Kusini yamesema, yakitumia jina la Kikorea la Bahari ya Japani.

“Kombora la balestiki linakisiwa kuwa kombora la masafa marefu lililorushwa kwa pembe ya juu,” kimesema chanzo kimoja. Korea Kaskazini kwa ujumla hufanyia majaribio makombora yake yenye nguvu zaidi na ya masafa marefu zaidi kwenye njia ya kuelekea juu, yaani kwenda juu na si nje, ili kuepuka kuruka juu ya nchi jirani.

“Jeshi letu limeongeza kiwango chake cha tahadhari na linashiriki kwa karibu taarifa kuhusu kombora la balistiki la Korea Kaskazini na mamlaka ya Marekani na Japani, na kudumisha hali ya juu ya kujitayarisha,” makao makuu ya majeshi ya Korea Kusini yameongeza.

China inatiwa wasiwasi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Lin Jian, amesema China imeeleza “wasiwasi” wake kuhusu hali ilivyo kwenye Rasi ya Korea. Pia alitoa wito wa “suluhisho la kisiasa kuhusu swali la rasi hii”. Tukio hilo la jaribio la kiombora limekuja saa chache baada ya wakuu wa ulinzi wa Marekani na Korea Kusini kuitaka Pyongyang kuondoa wanajeshi wake nchini Urusi, ambapo Washington inasema kuwa wanajeshi 10,000 wametumwa kwa ajili ya maandalizi ya hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi ya vikosi vya Ukraine.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2024


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply