Meli zaendelea kupita Hormuz chini ya mpango maalum wa UN

Na Cantona Joseph June 25, 2026 01:38 (EAT)

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Migogoro Mashariki ya Kati

Meli zilianza kupita katika Mlango-Bahari wa Hormuz chini ya mpango wa shirika la Baharini la Umoja wa Mataifa – IMO.Picha: Wen Xinnian/Xinhua/IMAGO

Meli zilianza kupita katika Mlango-Bahari wa Hormuz jana Jumatano chini ya mpango mpya wa shirika la shughuli za Baharini la Umoja wa Mataifa – IMO.

Meli zilianza kupita katika Mlango-Bahari wa Hormuz Jumatano chini ya mpango mpya wa shirika la shughuli za Baharini la Umoja wa Mataifa – IMO. Mpango huo utawezesha mamia ya meli zenye mabaharia wapatao 11,000 waliokwama katika eneo hilo la Ghuba kusafiri kupitia Hormuz. Kufikia Jumatano alasiri, kampuni ya ufuatiliaji wa baharini Kpler ilirekodi safari 25 za meli za mizigo siku ya Jumanne, na 17 Jumatano. Katibu Mkuu wa IMO Arsenio Dominguez aliuita mpango wa uokoaji kuwa hatua ya kurejesha usalama wa baharini. Hata hivyo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi wa Iran limesema leo Alhamisi kuwa itawezekana tu kupita salama katika Mlango-Bahari wa Hormuz kwa kutumia njia zilizoidhinishwa na Iran, na kwamba njia mpya iliyotangazwa bila uratibu na Iran haikubaliki na ni hatari kwa usalama. Jeshi hilo limesema litachukua hatua dhidi ya meli ambazo hazifuati masharti.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio anazuru Mashariki ya Kati kuwahakikishia washirika wake kuhusu kujitolea kwa Marekani katika eneo hilo. Alifanya mazungumzo na Rais wa Falme za Kiarabu Mohammed bin Zayed Al Nahyan siku ya Jumatano. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema wawili hao walijadili makubaliano ya muda yaliyofikiwa kati ya Marekani na Iran pamoja na usafiri salama wa meli kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz. Rubio alisema kwamba Marekani “itaungana kikamilifu” na washirika wake katika eneo la Ghuba wakati wa mazungumzo na Tehran.

All Rights Reserved © Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,495 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply