Urusi yaukosoa Umoja wa Ulaya kutaka kukagua meli baharini

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Juni 11, 2026 06:00 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Meli ya majini “Berlin” ikianza safari kwa ajili ya udhibiti wa vikwazo katika Bahari ya Mediterania katika operesheni IRINIPicha: Sina Schuldt/dpa/picture alliance

Urusi imelaani uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kuidhinisha meli za kijeshi katika bahari ya Mediterania kusimamisha na kukagua meli za kigeni zinazoshukiwa kuwa sehemu ya meli za kivuli zinazosafirisha mafuta ya Urusi.

Katika kauli yake ya Jumatano Urusi ilisema itachukua hatua zote muhimu za kisheria na nyingine ili kuzilinda meli zake katika bahari ya Mediterania.

Umoja wa Ulaya ulisema Jumatatu umepanua mamlaka ya operesheni IRINI, tume yake ya majini katika bahari ya Mediterania ambayo awali ilianzishwa kutekeleza marufuku ya silaha ya Umoja wa Mataifa dhidi ya Libya.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Urusi, Maria Zakharova, alisema hatua hiyi ilikuwa tishio kwa usalama wa baharini na akaushutumu Umoja wa Ulaya kwa kutishia meli za raia.

Alisema hakuna kitu kama meli za kivuli katika sheria ya kimataifa na maelezo haya yalikuwa ni uzushi wa kisiasa ulioanzishwa na Umoja wa Ulaya.

.

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,446 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply