Marekani na Iran zakubali kusitisha mapigano kwa wiki mbili

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na  Cantona Joseph April 08, 2026 12:08 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Rais wa Marekani Donald Trump amesema atasitisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa muda wa wiki mbili, huku juhudi za upatanishi zikionyesha dalili za makubaliano ya masharti.

Zaidi ya vifo 1500 vimeripotiwa nchini Lebanon, Israel ikiapa kuendelea na mashambulizi

.

Tangu kuanza kwa vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran mwezi mmoja uliopita, zaidi ya watu 1,530 wameuawa nchini Lebanon, baada ya Israel kuanzisha mashambulizi ya kuwalenga wapiganaji wa Hezbollah, Shirika la habari la AFP limeripoti.

Idadi hiyo ya vifo kulingana na AFP ilitolewa na wizara ya afya ya Lebanon, ambayo inajumuisha vifo vya wanawake 102 na Watoto 130. Zaidi ya watu 4,812 wamejeruhiwa.

Licha ya kusitishwa kwa mapigano nchini Iran, Israel imesisitiza kuwa makubaliano hayo hayajumuishi Lebanon na wataendelea kulenga kundi la Hezbollah.

Katika wiki kadhaa zilizopita, Israel imewatuma wanajeshi wake kusini mwa Lebanon na kudhibiti eneo karibu na mto Litani, Israel ikiapa kuwa lazima iondoe tishio la Hezbollah.

Mapema leo Israel imetekeleza mashambulizi kusini mwa Lebanon.

Falme za kiarabu “ilishinda” vita hivyo

.

Mshauri wa rais wa Falme za Kiarabu amesema kuwa taifa hilo “lilipata ushindi” baada ya kushambuliwa mara kadhaa na Iran tangu kuanza kwa vita hivyo.

“Tulishinda kupitia ulinzi wa kitaifa wa kihistoria uliolinda uhuru, heshima, na kutunza mafanikio yetu baada ya kuchokozwa,” alisema Anwar Gargash.

“Leo, tunasonga mbele tukikabiliana na mazingira magumu kwenye ukanda wetu tukiwa na nguvu zaidi, uelewa zaidi, na uwezo thabiti wa kushawishi mustakabali wa siku za usoni.”

Wizara ya ulinzi ya taifa hilo imekuwa ikichapisha taarifa ya jinsi imekuwa ikidungua makombora ya Iran.

Hapo jana katika taarifa waliyoitoa, tangu kuanza kwa vita hivyo wameweza kudundua ndege zisizo na rubani 2221, makombora ya majini 26 na makombora ya kibalistiki 520.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Oman, ameipongeza Pakistan kwa juhudi zao za kuhakikisha mkataba huo unaafikiwa na kusema kuwa anatumai utakuwa wa kudumu.

“Tutafanya kila tuwezalo kuunga mkono usitishaji mapigano” – Keir Starmer

.
Maelezo ya picha,Waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer

Waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer amesema `watafanya kila wawezalo kuhakikisha makubaliano ya kusitisha vita kwa muda nchini Iran yanadumu`

“Tumepokea vyema makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoafikiwa na yataleta afueni kwa ukanda huo na kote duniani` alisema Starmer

“Pamoja na washirika wetu tutaunga mkono makubaliano hayo ya kusitisha vita hadi suluhu ya kudumu ipatikane na Mlango Bahari wa Hormuz ufunguliwe`

Ofisi ya Waziri huyo mkuu imetangaza kuwa atasafiri kukutana na viongozi wa mataifa ya Ghuba na kutangaza atakavyounga mkono makubaliano ya kusitisha vita.

Katika mikutano na viongozi wa kikanda, atasisitiza uungwaji mkono usioyumba wa Uingereza na hitaji la azimio la kidiplomasia la muda mrefu ili kuhakikisha usitishaji mapigano unapelekea makubaliano ya kudumu.

Pia atashiriki katika mazungumzo kuhakikisha Mlango Bahari wa Hormuz unasalia wazi.

Wairani wakusanyika mjini Tehran baada ya tangazo la kusitishwa mapigano

.

Raia wa Iran wamekusanyika katika mji mkuu wa taifa hilo, Tehran, wakiwa wamebeba bendera ya taifa na mabango yenye picha ya Kiongozi Mkuu Mojtaba Khamenei.

Raia wa Iran wamejitokeza katika barabara za mji wa Tehran baada ya kutangazwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda.

.

Kusitishwa kwa vita hivyo kwa muda kumepokelewa kwa hisia mseto miongoni mwa raia wa Iran.

Kuna afueni kwa sababu viwanda vya nishati havitashambuliwa tena, lakini kwa wale ambao wanapinga utawala wa taifa hilo, hawajalipokea vyema.

.

Tumepata ‘ushindi kamili’ – Trump

.

Rais Donald Trump wa Marekani amesema hakuna shaka kwamba Marekani imepata “ushindi kamili” baada ya kukubaliana kuhusu kusitisha vita kwa wiki mbili na Iran.

Katika mahojiano na Agence France Presse baada ya tangazo lake, alisema kwamba urani iliyorutubishwa ya Iran “itajadiliwa kikamilifu” chini ya makubaliano hayo.

“Vinginevyo nisingekubali,” Trump alisema, bila kutoa maelezo yoyote kuhusu kile ambacho kingetokea kwa Iran.

Alipoulizwa kama angerudi kutoa tena vitisho kama vya awali vya kuharibu mitambo ya nishati na madaraja ya Iran ikiwa makubaliano hayo yangevunjika, alichosema tu ni: “Utalazimika kufuatilia hili.”

Trump, ambaye anatarajiwa kusafiri hadi China mwezi ujao kukutana na mwenzake wa China Xi Jinping, alisema: “Nasikia hivyo” alipoulizwa kama Beijing ilihusika katika kumfanya mshirika wake mkuu Tehran kujadiliana kuhusu makubaliano ya kusitisha mapigano.

Iran yajiona mshindi baada ya kustahimili vita dhidi ya Marekani na Israel

.

Serikali ya Iran na vyombo vya habari vya taifa hilo vinasema kuwa makubaliano ya kusitisha mashambulizi kwa muda ni ushindi mkubwa kwa utawala wa taifa hilo.

Katika taarifa iliyotolewa na Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, Iran imesema imeafikia karibu malengo yake yote ya vita hivyo na kuwa adui wake amepata pigo la kihistoria.

Ikumbukwe kwamba vita hivyo vilianza na kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa taifa hilo Ali Khamenei na viongozi wengine wakuu wakijeshi na hii ilikuwa tishio kubwa kwa utawala wa Iran.

Iran inajiona mshindi kwa kuweza kustahimili vita vilivyoanzishwa na Israel na Marekani kwa zaidi ya siku 30.

Israel yaunga mkono rasmi usitishaji mapigano lakini ‘haujumuishi Lebanon’

.

Israel imetoa taarifa rasmi kuhusu kusitisha mapigano na Iran.

Israel inaunga mkono uamuzi wa Rais Trump wa kusimamisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa wiki mbili ikiwa Iran itafungua mara moja Mlango Bahari na kusimamisha mashambulizi yote dhidi ya Marekani, Israel na katika nchi za eneo hilo.

Israeli pia inaunga mkono juhudi za Marekani kuhakikisha kwamba Iran sio tena tishio la nyuklia, kombora na ugaidi kwa Marekani, Israeli, majirani wa Kiarabu wa Iran na ulimwengu.

Marekani imeiambia Israeli kwamba imejitolea kufikia malengo haya, ambayo pia ni ya Marekani, Israeli na washirika wa kikanda wa Israeli, katika mazungumzo yajayo.

Usitishaji mapigano wa wiki mbili haujumuishi Lebanon.

  • Katika muktadha: Hapo awali, Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif alisema kusitisha mapigano kulihusisha Lebanon.

zilizopitaIsrael haijatoa taarifa yoyote mpaka sasa kuhusu usitishaji wa mapigano

s

Hadi sasa, Israel haijatoa taarifa rasmi kuhusu tangazo la kusitisha mapigano kati ya Marekani na Iran. Haijulikani ni kwa kiwango gani Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alihusika katika maamuzi ya Rais Donald Trump.

Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, ambaye amekuwa mpatanishi kati ya Marekani na Iran, amesema makubaliano ya usitishaji wa mapigano yanajumuisha pia nchi ya Lebanon, ambapo Israel ina vikosi vya ardhini.

Viongozi wa Israel wamekuwa wakisema hawataondoka Lebanon hadi tishio kutoka Hezbollah liondoke. Hata hivyo, hakuna ishara kwamba Israel imekubali kusitisha operesheni zake Lebanon au sehemu nyingine.

Kama vita vitamalizika kwa msingi wa “mapendekezo 10 kutoka Iran” yaliyotajwa na Trump, itachukuliwa kuwa ni mafanikio ya kimkakati kwa Tehran. Hata hivyo, wanasiasa wa mrengo wa kulia wanaomuunga mkono Netanyahu wanaweza kupinga makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano, hasa kama yanahusisha Lebanon, na hivyo kumweka Netanyahu njia panda kisiasa nchi hiyo ikiingia kwenye uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Bei ya mafuta duniani yashuka baada ya tangazo la Trump la usitishaji wa mapigano

s

Bei ya mafuta duniani imepungua kwa kiasi kikubwa baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kutangaza makubaliano ya kusitisha mapigano kwa wiki mbili.

Mapema Jumanne, pipa moja la mafuta uliouzwa kwenye masoko ya kimataifa ulikuwa na thamani ya dola 103.42, huku mafuta ya Marekani yakiwa karibu na dola 103.25 kwa pipa. Hata hivyo, bei bado iko juu kuliko kipindi cha kabla ya mzozo kuanza Februari 28.

Mtaalamu wa uchumi wa nishati kutoka Japan, Ichiro Kutani, alisema kushuka kwa ghafla kwa bei kunahusiana moja kwa moja na tangazo la Trump. Hata hivyo, bei haiwezi kurudi katika kiwango chake cha awali cha takribani dola 70 kwa pipa kwa sababu ya uharibifu wa miundombinu katika baadhi ya maeneo ya Mashariki ya Kati.

Wakati huo huo, masoko ya hisa barani Asia yamepanda: Nikkei 225 ya Japan imeongezeka kwa takribani 4% na ASX 200 ya Australia kwa karibu 3%.

Pakistan yasifu ‘hekima’ ya Marekani na Iran baada ya kusitishwa mapigano mara moja

s
Maelezo ya picha,Sharif (kushoto) na Trump wakionekana kuteta kwneye mkutano ulioitwa “Board of Peace” uliofanyika Januari mwaka huu huko Davos, Switzerland.

Pakistan, ambayo ni mpatanishi katika mzozo wa Marekani na Iran, imesifu hatua ya nchi hizo mbili kukubaliana kusitisha mapigano kwa wiki mbili.

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amesema pande zote zimeonyesha “hekima na uelewa mkubwa” kwa kukubali hatua hiyo, akiongeza kuwa zimeendelea kushiriki kwa njia chanya katika juhudi za kuleta amani na utulivu.

Amesema usitishaji wa mapigano umeanza kutekelezwa mara moja, huku akizialika pande zote mbili jijini Islamabad Ijumaa kwa mazungumzo zaidi yanayolenga kufikia makubaliano ya kudumu.

Kauli hiyo a Pakistan ilitolewa dakika chache kabla ya muda wa mwisho uliowekwa na Rais wa Marekani Donald Trump wa kufikia makubaliano.

Marekani na Iran zakubaliana kusitisha mapigano kwa wiki mbili

s

Rais wa Marekani Donald Trump amesema amekubali kusitisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa muda wa wiki mbili, kufuatia pendekezo la wapatanishi katika mgogoro huo.

Trump alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya mazungumzo na viongozi wa Pakistan, akiwemo Waziri Mkuu Shehbaz Sharif, ambao waliomba muda zaidi kwa juhudi za kidiplomasia.

Katika ujumbe wake, Trump alisema hatua hiyo inahusishwa na kufunguliwa kwa Mlango wa Hormuz kwa usalama, njia muhimu ya biashara ya mafuta duniani.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi amesema Iran iko tayari kusitisha mapigano iwapo mashambulizi dhidi ya nchi hiyo yatakomeshwa, ikiashiria makubaliano ya masharti kati ya pande hizo mbili.

Wakati huo huo, Pakistan imesema usitishaji wa mapigano umeanza kutekelezwa mara moja, hatua inayochukuliwa kama nafasi kwa pande zote kupunguza mvutano.

Trump pia amesema Marekani imepokea mapendekezo ya masuala 10 kutoka Iran, akiyataja kuwa ni msingi unaoweza kufanyiwa kazi kupitia mazungumzo, huku akieleza kuwa tofauti nyingi zilizokuwepo tayari zimepunguzwa.

Vita kati ya Marekani, Israel na Iran vilianza Februari 28 na vimeathiri masoko ya kimataifa, hasa bei ya mafuta.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,446 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply