Zelensky: Urusi imechagua ‘kuzidisha mashambulizi msimu wa pasaka’ badala ya kusitisha mapigano

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph April 04, 2026 12:08 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

xcv

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameishutumu Moscow kwa kuchagua “kuongeza kasi ya mashambulizi katika msimu wa sikukuu ya pasaka” badala ya kusitisha mapigano baada ya Urusi kutekeleza shambulio jingine kubwa la ndege zisizo na rubani na kombora dhidi ya Ukraine.

Raia sita waliuawa na wengine 40 kujeruhiwa huku Urusi ikirusha mamia ya ndege zisizo na rubani na makombora kote nchini Ukraine.

Mashambulizi makubwa ya mchana, ambayo hapo awali yalikuwa nadra, yamekuwa yakiongezeka.

Hayo yanajiri huku juhudi za kukomesha vita, zikiongozwa na Marekani, zikisimama tangu Rais wa Marekani Donald Trump na timu yake walipoelekeza nguvu zao kwenye mzozo wa Mashariki ya Kati.

Wakati huo huo, Zelensky alikubaliana na tathmini ya ujasusi ya Uingereza kwamba hali katika mstari wa mbele mashariki ilikuwa “nzuri zaidi” kwa Ukraine katika miezi 10, huku kusonga mbele kwa wanajeshi wa Urusi kukipungua.

Lakini hakujashuhudiwa usitishaji wa mashambulizi ya anga.

Katika eneo la Zhytomyr, magharibi mwa mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, waokoaji walilazimika kutafuta manusura chini ya vifusi vya nyumba zao huku safu nzima ya nyumba ikiharibiwa.

Katika eneo la Kyiv, ndege isiyo na rubani ilirekodiwa ikielekea kwenye jengo la ghorofa, kisha ikagonga ubavu wake, na kusababisha moto.

Kikosi cha uokozi nchini Iran chakabiliwa na msako hatari kinapomtafuta mwanajeshi wa Marekani

xcv

Ripoti za awali zinaonyesha kuwa rubani wa ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-15 iliyodunguliwa na Iran ameokolewa ikiwa itathibitishwa, tukio hili litaongeza kwenye historia ndefu ya operesheni za uokoaji wa kijeshi za Marekani (combat search and rescue – CSAR) zilizofanywa kwa miongo kadhaa.

Operesheni ya kumtafuta rubani ambaye ni mwanajeshi wa pili bado inaendelea nchini Iran, kwa mujibu wa shirika la habari CBS, mshirika wa BBC nchini Marekani.

Operesheni za uokoaji wa kivita (CSAR) huchukuliwa kuwa miongoni mwa shughuli ngumu zaidi na zinazohitaji uharaka mkubwa ambazo majeshi ya Marekani na washirika wake hujiandaa kuzitekeleza.

Nchini Marekani, vikosi maalum vya jeshi la anga hupatiwa mafunzo ya hali ya juu kwa ajili ya operesheni hizi za CSAR, na mara nyingi hupelekwa mapema karibu na maeneo ya migogoro ambapo kuna uwezekano wa ndege kupotea au kudunguliwa.

Artemis II: Wanaanga waelekea mwezini huku wakipiga picha ya ‘kushangaza’ ya dunia

xcv

NASA imechapisha picha za kwanza zenye ubora wa hali ya juu za dunia zilizopigwa na wafanyakazi wa misheni ya Artemis II walipofika katikati ya safari kati ya dunia na Mwezi.

Mkuu wa misheni hiyo, Reid Wiseman, ndiye aliyepiga picha hizo ambazo zimetajwa kuwa za kuvutia sana.

Picha hizo zilichukuliwa baada ya wafanyakazi kukamilisha mwendo wa mwisho wa injini ulioweka chombo chao kwenye njia sahihi kuelekea Mwezi.

Kwa mujibu wa taarifa za NASA, chombo cha Orion spacecraft kilikuwa umbali wa maili 142,000 kutoka Dunia na maili 132,000 kutoka mwezini wakati huo.

Mwanaanga Christina Koch alisema wana anga wote walijawa na furaha kubwa walipojulishwa kufikia hatua hiyo muhimu.

Hatua hiyo ilifikiwa takriban siku mbili, saa tano na dakika 24 tangu walipoondoka Duniani.

Picha ya kwanza, iliyopewa jina la “Hello, World,” inaonesha mandhari pana ya bahari ya Atlantiki ikiwa imezungukwa na mwanga wa anga huku dunia ikifunika mwanga wa Jua.

Pia kuna miale ya kijani inayoonekana katika ncha zote mbili za sayari.

Israel yadai kushambulia ‘miundombinu muhimu’ ya Tehran

XCV
Maelezo ya picha,Moshi ukifuka baada ya shambulio la anga huko Tehran mnamo Aprili 3

Jeshi la Israel (IDF) linasema limekamilisha “wimbi la mashambulizi dhidi ya maeneo ya miundombinu ya utawala wa kigaidi” mjini Tehran siku ya Ijumaa.

Taarifa mpya ya jeshi inasema ilishambulia eneo la ulinzi wa anga ambapo “makombora yaliyokusudiwa kulenga ndege yalihifadhiwa” pamoja na eneo la kijeshi “linalohusika na kuhifadhi taarifa za kitafiti za utawala”.

“Mashambulizi haya yaliyokamilika ni sehemu ya awamu inayoendelea dhidi ya mifumo na misingi muhimu ya utawala wa kigaidi wa Iran,” IDF inasema.

Awali iliarifiwa kwamba jeshi la Israel linasitisha kwa muda mashambulizi yake dhidi ya kusini mwa Iran, wakati juhudi za kumtafuta mwanajeshi wa ndege ya kivita ya Marekani aliyepotea zikiendelea.

Wakati huo huo, milipuko mikubwa imesikika mashariki mwa mji wa Tehran, kwa mujibu wa vyanzo viwili, alisema mwandishi mwandamizi wa BBC Persian.

Zaidi ya watu watatu pia wameiambia BBC kwamba wamesikia ndege za kivita zikiruka angani.

Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa mifumo ya ulinzi wa anga imewashwa katika mji huo.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,388 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply