Rais Macron awasili nchini Korea Kusini akitokea Japan

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph April 02, 2026 17:08 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Rais Macron na waziri mkuu wa Japan Sanae Takaichi mjini TokyoPicha: Franck Robichon/AFP

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili nchini Korea Kusini leo, baada ya kuzuru mshirika mwingine wa Marekani Japan ambako alisifu msimamo wa pamoja wa Ulaya.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili nchini Korea Kusini leo, baada ya kuzuru mshirika mwingine wa Marekani Japan ambako alisifu msimamo wa Ulaya, kauli iliyotafsiriwa kama pigo kwa Donald Trump juu ya vita vya Iran.

Ziara ya siku mbili ya Macron inajumuisha mkutano wake na Rais wa Korea Kusini Lee Jae Myung na kutembelea kumbukumbu ya kivita ili kutoa heshima kwa wanajeshi wa Ufaransa waliopigana katika vita vya Korea. Atajumuika pia katika jukwaa la kiuchumi na chakula cha jioni na wasanii wan chi hiyo.  Huko Japan, kiongozi wa Ufaransa alisaini nyaraka kuhusu madini muhimu na ushirikiano wa kijeshi.

Iran yatoa onyo kali, Trump atishia mashambulizi makubwa zaidi

xcv

Msemaji wa jeshi la IranEbrahim Zolfaghariamesema kuwa mashambulizi ya pamoja ya Marekani na Israel dhidi ya nchi yake hayajakuwa na athari kubwa, akidai kuwa mataifa hayo mawili hayana taarifa kamili kuhusu uwezo wa kijeshi wa Iran.

Amesisitiza kuwa Iran ina vifaa na mikakati ambayo haijafahamika vizuri na wapinzani wake, na hivyo kuonya kuwa hatua yoyote zaidi inaweza kukutana na upinzani mkali.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza, Yvette Cooper, ameanza mazungumzo kuhusu uwezekano wa kufungua tena Mlango wa Bahari wa Hormuz, njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta duniani.

Cooper ameishutumu Iran kwa “uzembe” na kusema kuwa hali ya sasa inahatarisha usalama wa usafirishaji wa kimataifa.

Aidha kwa upande wake rais Donald Trump akihutubia taifa Jumatano jioni, aliwahakikishia Wamarekani kuwa ataimaliza hali hiyo “haraka sana,” ingawa hakutoa muda maalum wa kumaliza mzozo huo.

Kauli yake imezua mjadala kuhusu hatua zinazoweza kuchukuliwa na Marekani na athari zake kwa amani na utulivu kimataifa.

Watoto wanne wauawa kwa shambulio la kisu Uganda

.

Watoto wanne wameuawa katika shambulio la kisu katika shule moja mjini Kampala, nchini Uganda.

Kwa mujibu wa polisi “Mshukiwa mwenye umri wa miaka 34 amekamatwa, na sababu ya kutekeleza mauaji hayo bado inachunguzwa,” Idara ya polisi ya Uganda imesema kupitia mtandao wa X.

Shule hiyo kwa jina Ggaba Early Childhood Development Program ipo eneo la Makindye katika mji mkuu wa Kampala

Gazeti la Uganda, Daily Monitor, limeripoti kuwa wakazi wa eneo hilo wanasema mshukiwa alisema yeye ni mzazi ili aruhusiwe kuingia shuleni humo, na baada ya kuzungumza na msimamizi wa shule hiyo aliwashambulia watoto hao.

Waathiriwa walikuwa na umri wa kati ya miaka miwili na mitatu, kwa mujibu wa gazeti hilo.

Mlango Bahari wa Hormuz uko wazi kwa meli ambazo si za “adui”

.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran, amesema taifa hilo linaruhusu meli kupita katika mlango bahari wa Hormuz ikiwa “hazimilikiwi na adui wao au kuhusika nao.”

“Mlango Bahari wa Hormuz uko wazi kwa meli ambazo si za “adui”.

Katika mahojiano ya televisheni, Esmail Baghaei anasema meli zinaruhusiwa kupita katika mlango bahari wa Hormuz baada ya ushirikiano na mamlaka ya Iran.

Akiangazia vita vinavyoendelea, msemaji huyo alisema kuwa “Iran haitavumilia kuzungushwa katika mzunguko wa vita, mazungumzo ya kusitisha vita, na makubaliano ya kusitisha vita”

Katika vita kati ya Israel na Iran vilivyodumu siku 12 mwezi Juni mwaka uliopita, Marekani ililenga vituo kadhaa vya kuzalisha nishati ya nyuklia nchini Iran.

“Walisema tuache, tukaacha, na baada ya miezi tisa wameanza tena” alisema Baghaei.

Raia 1800 wameuawa tangu utawala wa kijeshi kuchukua madaraka Burkina Faso- Ripoti

.

Zaidi ya raia 1,800 wa Burkina Faso wameuawa tangu kiongozi wa kijeshi Ibrahim Traore kuchukua madaraka miaka mitatu iliyopita na kutekeleza “uhalifu wa kivita na kukiuka haki za kibinadamu” ripoti ya Human Rights Watch inasema.

Ripoti hiyo inaelezea kuwa wa Burkinabe 1,837 wakiwemo watoto waliuawa katika visa 57 kati ya mwezi Januari 2023 na Agosti 2025.

Ripoti hiyo pia inasema mauaji hayo yalitekelezwa na wanajeshi wa taifa hilo, makundi yaliyojihami na makundi yenye itikadi kali.

Human Rights Watch inasema Traore na viongozi wengine sita wa ngazi ya juu ya jeshi “wanapaswa kuwajibishwa kwa maovu waliyotekeleza na kuchunguzwa ikiwemo viongozi watano wa makundi yenye itikadi kali”

Mamlaka za Burkina Faso bado hazijatoa tamko lolote kuhusu ripoti hiyo ya HRW.

Marekani imemuondelea vikwazo rais wa mpito wa Venezuela Delcy Rodriguez

.

Hatua hii inakuja chini ya miezi mitatu tangu Marekani kumkamata aliyekuwa rais wa taifa hilo, Nicolas Maduro na mkewe na sasa wanazuiliwa mjini New York wakikabiliwa na mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Rodriguez ambaye ni mshirika wa karibu wa Maduro, na aliyekuwa naibu rais, alikuwa amewekewa vikwazo mwaka 2018 kwa kukandamiza demokrasia.

Aliapishwa kuwa rais baada ya kuidhinishwa na bunge la Venezuela siku chache tu baada ya kukamatwa kwa Maduro.

Kupitia mtandao wa X, Rodriguez alikaribisha hatua hiyo na kusema kuwa “ Ni mwanzo mwema wa kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili”

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,394 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply