Urusi inachunguza chanzo cha ajali yake ya kijeshi Crimea

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph April 01, 2026 12:08 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Urusi imesema imeanzisha uchunguzi leo Jumatano baada ya ndege ya kijeshi ya Urusi kuanguka katika eneo la Ukraine linalomilikiwa na Urusi la Crimea.

Kamati ya Uchunguzi mjini Moscow imesema ndege hiyo ilikuwa na wafanyakazi 7 pamoja na abiria 23. Kamati hiyo imesema tatizo la kiufundi ndilo lililosababisha ajali hiyo na hapakuwepo na ishara yoyote ya kushambuliwa kutoka nje lakini bado wanachunguza.

Ndege hiyo ilianguka katika eneo la milima la jiji la Kubyshev sio mbali kutoka mji wa Crimea wa Simferopol.

Uchunguzi unafanyika kubaini iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa aina yoyote wa usalama wa operesheni  ya ndege  au kuitayarisha ndege hiyo kabla ya kupaa angani.

Jeshi la Urusi kwa kawaida linatumia eneo hilo la Crimea kurusha makombora kuelekea Ukraine katika vita vyake dhidi ya jirani yake huyo vilivyoingia mwaka wake wa nne tangu vilipoanza Februari 24, mwaka 2022.

Israel yaishambulia tena Beirut

Moshi ukifuka kwenye viunga vya Beirut kufuatia mashambulizi mengine ya Israel kwenye mji mkuu huo wa Lebanon siku ya Jumatano (Aprili 1, 2026).Picha: Raghed Waked/REUTERS

Jeshi la Israel linasema limefanya mashambulizi mengine ya anga dhidi ya mji mkuu wa Lebanon, Beirut, usiku wa kuamkia Jumatano.

Jeshi hilo limedai kuwa mashambulizi hayo yalimlenga kamanda wa ngazi za juu wa kundi la Hizbullah na yule liliyomuita “gaidi mwengine mkubwa”.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka Wizara ya Afya ya Lebanon, watu saba waliuawa kwenye mashambulizi hayo na wengine 21 walijeruhiwa.

Wakaazi wa huko wameripoti miripuko mikubwa na moto karibu na uwanja wa ndege wa Beirut.

Awali, wanamgambo wa Hizbullah walikuwa wamerusha  makombora na droni kuelekea kaskazini mwa Israel, ambako watu kadhaa wanatajwa kujeruhiwa.

Israel, iliyoivamia tena Lebanon baada ya Hizbullah kujiunga na vita vinavyoendelea dhidi ya Iran, imesema inapanga kulitwaa na kulikalia eneo la kusini mwa Mto Litani, lenye ukubwa wa maili 20 kwenye mpaka wake wa kaskazini.

Tayari, Israel imethibitisha kupoteza wanajeshi wake 10, wakiwemo wanne waliouawa jana, kutokana na mashambulizi ya Hizbullah, inayojaribu kuwarejesha nyuma wanajeshi wa Israel. 

Marekani kuutathmini upya uhusiano wake na NATO

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, anasema nchi yake itautathimini upya uhusiano wake na NATO baada ya kumalizika vita dhidi ya Iran.Picha: Alain Jocard/AFP

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Marco Rubio, amesema nchi yake itatathimini upya mahusiano yake na muungano wa kijeshi wa NATO mara tu vita dhidi ya Iran vitakapomalizika.

Rubio alikiambia kituo cha televisheni cha Fox News kwamba Washington inalazimika kuangalia upya thamani ya NATO kwa nchi yake, akiongeza kwamba “uamuzi huo utafanywa na Rais Donald Trump.”

Kauli hiyo ya Rubio inakuja muda mchache baada ya Trump kutumia mtandao wake wa kijamii kuzikosowa vikali Uingereza na Ufaransa ambazo zimekataa kujiunga na vita dhidi ya Iran, zikisema hazikushauriwa kabla.

Badala yake, Trump aliyataka mataifa hayo kujitokeza yenyewe kuufunguwa Mlango Bahari wa Hormuz uliofungwa na Iran kwa meli zote zinazohusishwa na Marekani na Israel ama washirika wao.

Ufaransa iliikatalia Marekani kutumia anga lake kwa ndege zenye silaha kuelekea Israel.

Uamuzi kama huo ulishachukuliwa na Uhispania, ambayo imekataa anga na ardhi yake kutumiwa na Marekani kwa ndege zinazoishambulia Iran.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply