Jeshi la Somalia latwaa udhibiti Jimbo la Kusini Magharibi

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa : March 31, 2026 7:10 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Kikosi cha Walinda Amani wa Umoja wa Afrika katika eneo la Baidoa, Kusini Magharibi mwa Somalia.Picha: Ed Ram/Getty Images

Jeshi la Somalia limetwaa udhibiti wa jimbo la Kusini Magharibi, hatua iliyomfanya rais wa jimbo hilo kujiuzulu wiki mbili baada ya serikali yake kusema ilikuwa inavunja mahusiano na serikali kuu mjini Mogadishu.

Wanajeshi wa Somalia waliripotiwa kuingia kwenye mji mkuu wa jimbo hilo, Baidoa, siku ya Jumatatu (Machi 30).

Baidoa ni wa kimkakati wenye makao makuu ya kikosi cha kimataifa wa walinda amani na mashirika kadhaa ya kibinaadamu, kwenye eneo hilo lililoathirika kwa ukame, migogoro na wakimbizi wa ndani.

Rais wa jimbo hilo, Abdiaziz Hassan Mohamed Laftagareen, aliandika kupitia mtandao wa Facebook kuwa amejiuzulu wadhifa wake, siku chache baada ya kuchaguliwa kuongoza tena kwa muhula mwengine wa miaka mitano.

Wakaazi wengi wameukimbia mji wa Baidoa na baadhi ya mashirika ya misaada yamesitisha shughuli zao, wakihofia mapigano kati ya wanajeshi wa serikali kuu na vikosi vya jimbo hilo.

Mawaziri wa kigeni wa EU waitembelea Bucha

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, anaongoza ujumbe wa mawaziri wa kigeni wa mataifa wanachama wa Umoja huo kukitembelea kitongoji cha Bucha nchini Ukraine siku ya Jumanne (Machi 31, 2026).Picha: John Thys/AFP

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, anaongoza ujumbe wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Poland na Italia kukitembelea kitongoji cha Bucha cha Ukraine kilichokombolewa kutoka jeshi la Urusi.

Ziara hiyo inakusudia kuadhimisha miaka minne tangu wilaya hiyo ya mji mkuu wa Ukraine, Kiev, kukombolewa kutoka mikononi mwa wanajeshi wa Urusi na kuibuwa ukatili mkubwa wa kivita uliotendeka.

Bucha, iliyo magharibi mwa Kiev, ilikaliwa na vikosi vya Urusi katika siku za mwanzo za vita vilivyoanzishwa na Urusi mnamo Februari 2022.

Baada ya wanajeshi wa Ukraine kufanikiwa kukirejesha mikononi mwao, miili ya raia ilikutikana imetapakaa kwenye mitaa ya kitongoji hicho, huku ikiwa imefungwa mikono kwa nyuma.

Haraka, Bucha ikageuka kuwa alama ya uhalifu wa vita hivyo, na baadaye Umoja wa Mataifa ulithibitisha vifo vya mamia ya raia.

Maafisa wa Urusi wanaendelea kukanusha tuhuma za mauaji hayo na badala yake wanadai ukatili wa Bucha lilikuwa tukio lililobuniwa na Ukraine yenyewe.

Ukraine yafikia makubaliano na mataifa ya Ghuba

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine (kushoto) akiwa na mwenyeji wake, Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, mjini Jeddah siku ya tarehe 27 Machi 2026.Picha: Ukrainian Presidential Press Service/AFP

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema nchi yake imefikia makubaliano ya kihistoria kati ya nchi yake na ya mataifa ya Ghuba, akizitaja Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Qatar.

Akizungumza kwenye hotuba yake ya jioni ya Jumatatu (Machi 30), Zelensky alisema Ukraine pia “inashirikiana na Kuwait na Jordan na tayari imepokea maombi kutoka Bahrain na Oman.”

Chini ya makubaliano hayo, Ukraine itakuwa inatuma mifumo ya ulinzi, utaalamu wa kijeshi na ufundi kwa mataifa hayo ya Ghuba, nayo itapewa ushirikiano kwenye masuala mengine ya usalama.

Kwa mujibu wa Zelensky, tayari makubaliano yamefikiwa kwa ajili ya kuimarisha mifumo ya ulinzi wa anga, utengenezaji wa pamoja wa silaha na ushirikiano kwenye sekta ya nishati.

Hayo yote yanatokana na ziara ya hivi karibuni ya Zelensky kwenye eneo la Ghuba, wakati huu nchi yake yenyewe ikiendelea kukabiliana na uvamizi wa Urusi uliongia mwaka wake wa nne, huku vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran vikipamba moto kwenye eneo zima la Mashariki ya Kati.

Walinda amani wengine wa Umoja wa Mataifa wauawa Lebanon

Kikosi cha Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) kimesema askari wake wengine wawili wameuawa kwenye mashambulizi ya pili ndani ya kipindi cha masaa 24 kusini mwa nchi hiyo.

Mmoja wa wanajeshi wa Indonesia kwenye Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) akiwa kwenye kijiji cha Adaisseh kilicho mpakani na Israel.Picha: Mahmoud Zayyat/AFP

Kwenye taarifa yake, UNIFIL ilisema walinda amani hao kutoka Indonesia waliuawa baada ya gari yao kushambuliwa kwa mripuko usiofahamika, huku wengine wawili wakijeruhiwa, ambapo mmoja ana hali mbaya.

Mauaji hayo ya Jumatatu (Machi 30) yalitanguliwa na yale ya Jumapili, ambapo mwanajeshi mwengine mmoja wa Indonesia kwenye kikosi cha UNIFIL aliuawa kwa kombora la Israel.

Jeshi la Lebanon lilisema pia kuwa mwanajeshi wake mmoja ameuawa, huku shirika la habari likiripoti wapiganaji watatu wa Hizbullah nao wakiuawa kwenye viunga vya kusini vya mji mkuu, Beirut.

Israel, kwa upande wake, ilithibitisha wanajeshi wake wanne kuuawa kwenye eneo hilo.

Umoja wa Mataifa, Ufaransa na Uhispania zimelaani mauaji hayo dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa. 

Bei ya mafuta yapanda tena soko la dunia

Moshi ukifuka kwenye Bandari ya Dubai baada ya mashambulizi ya Iran kwenye eneo hilo.Picha: Fatima Shbair/AP Photo/picture alliance

Bei ya mafuta imeripotiwa kupanda tena kwenye soko la dunia kutokana na athari za moja kwa moja za vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Iran, ambavyo leo vimeingia siku yake ya 32.

Mapema asubuhi ya Jumanne (Machi 31), pipa moja la mafuta liliuzwa kwa dola 115.17 za Kimarekani kwenye masoko ya Asia, ikiwa ni muda mchache baada ya meli nyengine ya mafuta kushambuliwa kwenye bandari ya Dubai.

Meli hiyo iitwayo Al Salmi ilikuwa imebeba mapipa milioni mbili kutokea Kuwait na Saudi Arabia na mamlaka za Dubai zinasema zinaendelea na juhudi za kuuzima moto uliozuka baada ya kushambuliwa na droni kutokea Iran.

Siku ya Jumatatu (Machi 30), meli nyengine inayomilikiwa na Ugiriki iliripoti kulengwa na makombora mawili ikiwa kwenye pwani ya Ras Tanura nchini Saudi Arabia. 

Touadéra aapishwa tena kutawala Jamhuri ya Afrika ya Kati

Rais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amerejea madarakani kwa muhula mwengine wa tatu wa miaka saba.Picha: Michael Brochstein/ZUMA/IMAGO

Rais Faustin-Archange Touadéra wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameapishwa kuhudumu kwa muhula wa tatu miezi mitatu baada ya kutangazwa mshindi kwenye uchaguzi uliokuwa na utata.

Touadéra sasa atatawala tena kwa muhula mpya wa miaka saba.

Alitangazwa mshindi kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba mwaka jana, ambao uligomewa na muungano wa vyama vya upinzani, kufuatia mabadiliko ya katiba ya mwaka 2023 yaliyoondowa ukomo wa mihula ya kutawala na kuongeza urefu wa kila muhula kuwa miaka saba badala ya mitano ya awali.

Vyama vya upinzani viliyakataa matokeo ya uchaguzi huo, ambayo yalimpa Touadéra ushindi wa asilimia 78.  

Akila kiapo siku ya Jumatatu (30 Machi), Touadéra alisema anadhamiria “kujenga uchumi unaojitegema na usimamizi wa wazi wa rasilimali za taifa” hilo.

Sherehe ya kuapishwa kwake ilihudhuriwa na marais wa Kongo na visiwa vya Komoro.

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,344 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply