Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Imechapishwa: March 25, 2026 12:27 (EAT)



Msemaji wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya ya Iran, ambaye ni kamanda mkuu wa kijeshi wa nchi hiyo (bila kutaja jina la Marekani na Trump) amezungumzia kuhusu “taifa lenye nguvu kubwa duniani” – akisema “usiite kushindwa kwako makubaliano”.
Ebrahim Zolfaghari amesema katika ujumbe wa video uliochapishwa na vyombo vya habari vya Iran leo kwamba “je, kiwango cha mgogoro wenu wa ndani kimefikia hatua ambapo mnajadiliana wenyewe?”
“Hautaona uwekezaji wako katika eneo hilo wala bei za zamani za mafuta tena, hadi utakapoelewa kwamba utulivu katika eneo unahakikishwa na mkono wenye nguvu wa vikosi vyetu vya kijeshi. Utulivu huja kupitia nguvu,” Zolfaghari alisema.
Aliongeza kwamba “mtu kama sisi hatuwezi kufikia makubaliano na mtu kama wewe. Sio sasa, wala milele”.
Waziri Lukuvi wa Tanzania afariki dunia

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu, na Mbunge wa jimbo la Isimani, William Lukuvi ameaga dunia.
Kifo chake kimetokea leo tarehe 25 mwezi Machi mwaka 2026, saa moja asubuhi, katika hospitali ya Benjamini Mkapa jijini Dodoma, taarifa ya Ikulu ya Tanzania imeeleza.
Lukuvi alikuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo hospitalini hapo.
Lukuvi amekulia umoja wa Vijana CCM. Alianza kuwa Naibu Waziri baadaye Mkuu wa mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam wakati wa Rais Mkapa.
Rais Kikwete alimteua kuwa Waziri katika wizara tofauti. ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge Sera na Uratibu.
Katika awamu ya utawala wa John Pombe Magufuli, alimteua kuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
Rais Samia alimtoa kwenye baraza la mawaziri na kumfanya kuwa mshauri wa masuala ya uhusiano wa umma, kisha kumrejesha kuwa waziri baada ya uchaguzi wa 2025.
Bei ya mafuta yashuka huku Trump akizungumzia mazungumzo ya amani ya Iran

Bei ya mafuta imeshuka barani Asia baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema mazungumzo ya kukomesha vita yanaendelea, huku Iran ikisema meli “zisizo na uadui” zinaweza kutumia njia muhimu ya meli katika Mlango Bahari wa Hormuz.
Mafuta ghafi yalishuka kwa 5% hadi $99.29 (£74.16) kwa pipa, huku mafuta yaliyouzwa Marekani yakishuka kwa zaidi ya 5.5% hadi $88.41.
Trump alisema Jumanne kwamba mazungumzo ya kukomesha vita yanafanyika kwa “sasa” na kwamba watu ambao Marekani ilikuwa ikijadiliana nao “wanataka kufanya makubaliano haraka iwezekanavyo” – dai linalopingwa na maafisa wa Iran.
Siku ya Jumatatu, maafisa mjini Tehran walisema madai ya mazungumzo kati ya Marekani na Iran yalikuwa “habari bandia”, huku mashambulizi kati ya Israel na Iran yakiendelea.
Trump alisema Makamu wa Rais JD Vance na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio walihusika katika majadiliano ya kukomesha vita.
Rais aliongeza kwamba mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yamesababisha “mabadiliko ya utawala”, akirudia madai yake kwamba viongozi wa Iran wamekubaliana kwamba hawatakuwa na silaha ya nyuklia tena.
Lakini Iran hapo awali ilikanusha madai kwamba ilikuwa imewasiliana na Marekani, ikisema hilo ni jaribio la kudanganya masoko.
Iran yasema meli ‘zisizo na uadui’ zinaweza kupita salama Mlango-Bahari wa Hormuz

Iran imesema kwamba meli “zisizo na uadui” zinaweza kupita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz huku kukiwa na mlolongo wa usafiri baharini kupitia njia hiyo ya maji ambayo imesababisha mgogoro mkubwa zaidi wa nishati duniani.
Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, ujumbe wa Iran kwa Umoja wa Mataifa ulisema meli zinaweza kupita “salama” kwenye njia ya baharini, “mradi tu hazitashiriki wala kuunga mkono vitendo vya uchokozi dhidi ya Iran na kufuata kikamilifu kanuni za usalama zilizotangazwa.”
Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ulitumwa kwa Baraza la Usalama lenye wanachama 15 na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumapili. Kisha ukasambazwa Jumanne miongoni mwa wanachama 176 wa shirika la meli la Umoja wa Mataifa lenye makao yake makuu London linalohusika na kudhibiti usalama wa meli za kimataifa na kuzuia uchafuzi wa mazingira.
Meli zitaruhusiwa kusafiri kwenye Mlango Bahari “kwa uratibu na mamlaka husika za Iran”, taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii ilisema.
Hata hivyo, Iran haikufafanua katika taarifa kuhusu kanuni ambazo vyombo vya majini vinapaswa kufuata ili kusafiri kwa usalama kwenye njia ya Mlango Bahari, ambayo karibu moja ya tano ya usambazaji wa mafuta na gesi asilia duniani hupitia.
Matamshi ya Iran yalikuja huku Rais wa Marekani Donald Trump akisema mazungumzo yanaendelea ili kukomesha vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, licha ya Iran kukanusha hapo awali kwamba pande hizo zilikuwa katika mazungumzo.
Qatar inasema “haishiriki” katika juhudi zozote za upatanishi kati ya Marekani na Iran

Qatar imetangaza kwamba “haishiriki” katika juhudi zozote za upatanishi wa moja kwa moja kati ya Marekani na Iran, ikibainisha kwamba inaunga mkono “njia za kidiplomasia” zinazolenga kukomesha vita, kulingana na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar Majid Al-Ansari.
“Kwa sasa hakuna juhudi za moja kwa moja za Qatar zinazohusiana na upatanishi kati ya pande hizo mbili,” Al-Ansari alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kila wiki katika Wizara ya Mambo ya Nje, akielezea kwamba “lengo la Qatar katika hatua ya sasa ni kuilinda nchi na kushughulikia hasara zinazotokana na mashambulizi mbalimbali ambayo imekabiliwa nayo
Alibainisha kwamba msimamo wa Qatar tangu siku ya kwanza ya vita “umekuwa wazi, kwamba vita hivi lazima vimalizike kwa njia za kidiplomasia, na huu ndio msimamo wetu kuhusu migogoro yote duniani
Katika muktadha huu, Al-Ansari alisema kwamba mawasiliano na Iran “kwa kawaida hutegemea misimamo na vitendo vyake, haswa kuhusu mashambulizi ambayo nchi za eneo hilo zimefanyiwa,” akiongeza, “Iran lazima iamue jinsi inavyoweza kujenga upya uaminifu uliopotea kwa sababu ya mashambulizi yake dhidi ya uhuru wetu”.
Kuhusu “uratibu” kati ya Qatar na Marekani, alisema: “Sisi ni washirika wa upande wa Marekani, na tunafanya kazi kuwasiliana nao ili kuweka wazi taswira kamili, hasa kwa kuwa shambulio dhidi ya Jimbo la Qatar limesababisha matokeo mabaya kwa uchumi wa Qatar”.
Katika suala hili, Al-Ansari alisema kwamba “shambulio la vituo vya gesi huko Ras Laffan lilisababisha kupungua kwa uzalishaji kwa asilimia 17, huku hasara zikifikia takriban dola bilioni 100 kwa kipindi cha miaka mitano, na shughuli za ukarabati zinaweza kuchukua muda sawa”.
Marekani kupeleka maelfu ya wanajeshi zaidi Mashariki ya Kati

Pentagon inatarajiwa kutuma maelfu ya wanajeshi kutoka kikosi maalumu cha Jeshi la Marekani, 82nd Airborne Division, kwenda Mashariki ya Kati, kwa mujibu wa Reuters. Hatua hiyo itaoongeza nguvu za kijeshi za Marekani huku Rais Donald Trump akizungumza kuhusu uwezekano wa makubaliano na Tehran kuhusu kumaliza vita.
Reuters iliripoti kwa mara ya kwanza tarehe 18 Machi kuwa utawala wa Trump ulikuwa unafikira kutuma majeshi zaidi, hatua ambayo ingeweza kupanua uwezekano wa kuhusisha operesheni ndani ya ardhi ya Iran.
Hatua kama hiyo ingeongeza hatari katika mzozo ambao tayari umeshaingia wiki ya nne na kuathiri masoko ya kimataifa. Maafisa hao, waliokuwa wakizungumza kwa sharti la kutotambulika, hawakutoa maelezo ya mahali ambapo wanajeshi hao watapelekwa au lini watapofika katika eneo hilo.
Kuhusu hili, msemaji wa White House, Anna Kelly alisema “Kama tulivyoeleza, Rais Trump daima ana chaguo zote za kijeshi kwenye mikononi yake,”.
Hadi sasa, hakuna uamuzi uliofanywa kutuma majeshi ndani ya Iran yenyewe, alisema chanzo kimoja, lakini hatua hii itaongeza uwezo wa Marekani kwa ajili ya operesheni zinazoweza kufanyika baadaye katika eneo hilo.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.