Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph, Imechapishwa : March 19, 2026 07:33 (EAT)



Israel imeyashambulia maeneo ya kusini mwa Lebanon ukiwemo mji wa Tyre.Picha: Kawnat Haju/AFP
Israel imefanya mashambulio mapya katika maeneo ya kusini mwa Lebanon. Watu kadhaa wanaripoti kujeruhiwa katika hujuma hizo.
Israeli ilifanya mashambulizi katika miji iliyo kusini mwa Lebanon, na kusababisha watu wengi kujeruhiwa. Hayo yameripotiwa na vyombo vya habari vya serikali Ijumaa.
Shirika rasmi la habari la kitaifa la Lebanon limeripoti kamba ndege za kivita za adui Israeli zilishambulia alfajiri, zikiilenga miji ya Bafliyeh na Hanine katika wilaya za Tyre na Bint Jbeil na kuongeza kuwa vikosi vya Israel vilikuwa vimeishambulia miji mingine mitano kusini mwa nchi.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya walumbana na Orban hukusu Ukraine

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán ametumia kura ya veto kuzuia mkopo mpya kwa ajili ya Ukraine.Picha: dts Nachrichtenagentur/IMAGO
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameelezea ghadhabu yao kwa waziri mkuu wa Hungary Viktor Orbán kuhusu uamuzi wake wa kuzuia mkopo mpy kwa Ukraine licha ya ahadi ya awali.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameelezea ghadhabu yao kwa waziri mkuu wa Hungary Viktor Orbán kuhusu uamuzi wake wa kutumia kura ya turufu kuzuia mkopo mpya wa euro bilioni 90 kwa Ukraine licha ya ahadi ya awali.
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz alisema baada ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya uliofanyika mjini Brussels jana Alhamisi kwamba hatua ya Orban ni kitendo cha kutokuwa mwaminifu sana na kitu kama hicho hakijawahi kutokea.
Kwa masikitiko makubwa sana kwa viongozi wenzake wengi wa Umoja wa Ulaya, Orbán alikuwa ameidhinisha mkopo huo katika mkutano uliopita mnamo Desemba kabla ya serikali yake kubadili mkondo katika mzozo na Ukraine kuhusu kusitishwa kwa usafirishaji wa mafuta kutoka Urusi.
Merz alisema jambo hili litaacha makovu makubwa, akionya kuhusu athari kwa mabadiliko ya msimamo ya Orbán.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameunga mkono maoni ya Merz akisema makubaliano ya pamoja kuhusu mkopo huo lazima yaheshimiwe na kutekelezwa bila kuchelewa, kwa mujibu wa kanuni ya ushirikiano wa uaminifu.
Rais Deby aamuru mashambulizi ya kulipiza kisasi Sudan

Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby ameliamuru jeshi lifanye mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa kila shambulizi linalotokea Sudan.Picha: Israel Matene/REUTERS
Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby ameamuru mashambulizi y akulipiza kisasi kwa kil shambulizi litakalotokea Sudan. Uamuzi huu unafuatia shambulizi la dori lililowaua wtu 17 nchini Chad.
Rais wa Chad Mahamat Idriss Deby amefanya mkutano wa baraza la ulinzi na usalama usiku wa kuamkia leo na kuliamuru jeshi kulipiza kisasi kuanzia usiku kwa shambulio lolote linalotoka Sudan. Haya ni kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya rais iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Serikali ya Chad ilisema Alhamisi kwamba droni kutoka Sudan liliwaua watu 17 ilipoushambulia mji wa Tine ulioko mpakani mashariki mwa Chad. Tukio hilo lililotokea Jumatano jioni lilikuwa la hivi karibuni nchini Chad kutokana na mzozo unaotolewa nchini Sudan, ambapo kikosi cha wapiganaji wanamgambo wa RSF kimekuwa kikipigana na jeshi la Sudan tangu Aprili 2023.
Wapiganaji hao wamefanya operesheni kadhaa karibu na mpaka wa Chad, na kusababisha vifo upande wa Chad.
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Chad ametahadharisha kwamba mzozo wa Sudan haupaswi kuenea hadi mpakani.
Urusi na Ukraine zashambuliana, watu wawili wauwawa

Magari ya uokozi yakufanya operesheni ya uokoaji baada ya shambulizi la droni la UrusiPicha: State Emergency Service of Ukraine in Odesa region/Handout/REUTERS
Mashambulizi ya Urusi na Ukraine yamewaua watu wawili kila upande wa mpaka leo Ijumaa, huku meli mbili za mizigo zenye bendera ya kigeni zilizojaa nafaka zikishambuliwa kusini mwa Ukraine.
Maafisa wametangaza kuwa mashambulizi ya usiku kucha kat ya Ukraine na Urusi yalitokea wakati rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alipotangaza kwamba wapatanishi kutoka Kyiv walikuwa wakisafiri kwenda Marekani kwa lengo la kuanzisha tena mazungumzo ya pande tatu na Urusi.
Mkuu wa eneo la kusini mwa Ukraine la Zaporizhzhia alisema mashambulizi ya Urusi huko yalimuua mwanamke wa miaka 30 na kumjeruhi mvulana mmoja, 10, na mwanamume mmoja, 48.
Jeshi la anga la Ukraine lilitangaza kwamba Urusi ilikuwa imeshambulia nchi hiyo kwa kutumia ndege zisizo na rubani 156 na kwamba mifumo ya ulinzi wa anga ilikuwa imeziangusha 133 kati yao.
Shambulio la Urusi lililenga maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na mji wa bandari wa kusini wa Odesa ambapo maafisa walisema meli mbili za mizigo zilizojaa nafaka zilikuwa zimeharibiwa, na kwamba wafanyakazi wawili walijeruhiwa.
Belarus yawaachia wafungwa 250 wa kisiasa

Rais wa Belarus Alexander LukashenkoPicha: Roman Naumov/Picvario Media/picture alliance
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ameamrisha kuachiwa huru kwa wafungwa 250 wa kisiasa kama sehemu ya makubaliano na Marekani ya kuiondolea baadhi ya vikwazo.
Hii ndiyo hatua ya hivi karibuni ya rais huyo kujaribu kuimarisha mahusiano yake na Magharibi.
Lukashenko ametoa msamaha kwa wafungwa hao baada ya kukutana na mjumbe maalum wa Rais wa Marekani Donald Trump, John Coale katika Mji Mkuu wa Belarus Minsk.
Coale amewaambia waandishi wa habari kuwa marekani sasa itaiondolea Belarus vikwazo kutoka benki zake mbili za taifa na wizara ya fedha ya nchi hiyo.
Kiongozi wa upinzani wa Belarus aliye uhamishoni Svetlana Tsikhanouskaya ameipongeza hatua ya kuachiwa kwa wafungwa hao akidai ni “wakati wa afueni kubwa na matumaini.”
Freiburg yafuzu robo fainali Ligi ya Ulaya

Wachezaji wa Genk na Freiburg wakipambana katika mechi ya Ligi ya UlayaPicha: Markus Verwimp/kolbert-press/IMAGO
Klabu ya Freiburg imetinga hatua ya robo fainali ya mashindano ya Ligi ya Ulaya baada ya kuifumua Genk ya Ubelgiji 5-1 usiku wa kuamkia Ijumaa.
Katika mechi ya mkumbo wa kwanza ya raundi ya mtoano ya 16 bora, Freiburg ilikuwa imefungwa 1-0 huko Ubelgiji na sasa baada ya matokeo ya Alhamis, imefuzu kwa jumla ya mabao 5-2.
Freiburg sasa watakuwa wanachuana na Celta Vigoya Uhispania baada ya klabu hiyo ya la Liga kuifunga Lyon 2-0.
Klabu nyengine ya Ujerumani VfB Stuttgart imeondolewa kwenye mashindano hayo baada ya kuzabwa 2-0 na mabingwa wa Ureno FC Porto.
Stuttgart wameondolewa kwa jumla ya mabao 4-1.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.