Malengo ya Marekani kwa Iran ni tafauti na ya Israel

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph,Imechapishwa : March 20, 2026 15:33 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Marekani, Tulsi Gabbard, anasema malengo ya nchi yake kwenye vita vya Iran hayafanani na ya Israel.Picha: Lenin Nolly/NurPhoto/picture alliance

Mkuu wa Usalama wa Taifa wa Marekani, Tusli Gabbard, amesema malengo ya nchi yake kwenye vita vyake nchini Iran ni tafauti na ya mshirika wake, Israel, licha ya kuanzisha uchokozi wa pamoja dhidi ya taifa hilo la Ghuba.

Akizungumza mbele ya kamati ya usalama wa taifa ya bunge la Marekani siku ya Alkhamis (Machi 19), Gabbard alisema malengo yaliyowekwa na Rais Donald Trump yanatafautiana na yale yaliyowekwa na serikali ya Israel.

“Tunaweza kuona kupitia operesheni hizi kwamba serikali ya Israel imejikita kwenye kuuvunja uongozi wa Iran. Rais Trump ameelezea kwamba malengo yake ni kuuharibu uwezo wa Iran kurusha makombora ya masafa marefu, uundaji wa makombora hayo na jeshi lao la baharini,” alisema mkuu huyo wa usalama wa taifa.

Hata hivyo, kauli yake inaonekana kwenda kinyume na ile ya Waziri wa Vita wa Marekani, Pete Hegseth, ambaye wakati akizungumzia uwasilishaji wa pendekezo la kupatiwa dola bilioni 200 za ziada bungeni, alisema fedha kama hizo zinahitajika “kuwauwa watu wabaya.”

“Kiasi cha dola bilioni 200 nafikiria kiwango hicho kinaweza kutusogeza. Bila shaka kunahitajika fedha kuwauwa watu wabaya. Kwa hivyo tunarudi Congress na jamaa huko kuhakikisha tunapewa fedha za kutosha kutimiza kinachofanyika, kuhakikisha silaha zipo sio tu za kutosha bali hata za ziada.” Alisema Hegseth kwenye kauli inayoashiria kuwa malengo ya Marekani na Israel ni mamoja panapohusika “kuwauwa watu wabaya”.

Waziri wa Vita wa Marekani, Pete Hegseth, anasema ataomba bungeni dola bilioni 200 zaidi kwa ajili ya vita dhidi ya Iran.Picha: Brendan Smialowski/AFP

Waziri huyo wa Vita alisema pia kwamba “hakuna muda maalum uliowekwa kumaliza vita hivyo hadi pale Rais Trump atakapoamuwa kwamba ameridhika na matokeo yake.”

Marekani ilishiriki mashambulizi ya South Pars

Licha ya Rais Trump kusema kuwa nchi yake haikujuwa kuhusu mashambulizi ya Israel kwenye visima vya gesi vya Iran yaliyozuwa ulipizaji kisasi wa kiwango cha juu wa Iran, Israel imesema mashambulizi hayo yalifanyika kwa ushirikiano na Pentagon, ingawa imeahidi kuwa hayatajirejea.

Rais Donald Trump wa Marekani anasema nchi yake haikujuwa kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya visima vikubwa kabisa vya mafuta duniani vinavyomilikiwa na Iran.Picha: Luis M. Alvarez/AP Photo/picture alliance

Kupitia mtandao wake wa Truth Social, Trump aliandika siku ya Jumatano (Machi 18) kuwa amedai kuwa nchi yake haikuwa imejulishwa wala kushirikishwa kwenye mashambulizi hayo dhidi ya visima vya gesi katika eneo linalomilikiwa kwa pamoja na Qatar na Iran, ambavyo ndivyo vikubwa kabisa duniani, akitowa wito wa kutorejewa na kuitishia Iran isijaribu kuendeleza mashambulizi yake dhidi ya miundombinu ya nishati ya majirani zake. 

Lakini jioni ya Alkhamis, maafisa watatu tafauti wa kijeshi wa Israel walinukuliwa na vyombo vya habari wakisema mashambulizi hayo yaliratibiwa kwa ushirikiano wa pamoja kati yao na Marekani.

Maafisa hao walisema, hata hivyo, kwamba tukio kama hilo halitarejewa, ikitafsiriwa kunatokana na katazo la Trump, mshirika mkubwa wa Israel.

Iran yajibu mashambulizi

Iran ilijibu mashambulizi hayo kwa kuviripuwa kwa makombora visima vya mafuta na gesi nchini Qatar, Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu, mataifa ambayo Tehran inayatuhumu kuruhusu ardhi zake kutumiwa na maadui zake kuishambulia. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, anasema nchi yake haitaacha kujibu mashambulizi yoyote dhidi ya miundombinu yake ya nishati.Picha: Jean Marc Ferré/MAXPPP/picture alliance

Uongozi nchini Iran umeapa kuendelea kujibu mashambulizi kadiri yanavyoelekezwa kwake na ukiwakosowa vikali wale wanaoitolea Tehran kuacha mashambulizi yake bila kulaani na hata kutaja kuwa imekuwa ikijibu tu uchokozi dhidi yake, ambao hadi sasa umeshaangamiza maisha ya watu zaidi ya 2,000 wakiwemo watoto, wanawake, na viongozi wakuu wa kisiasa, kijeshi na kidini.

Waziri wa Mambo ya Nje, Abbas Araghchi, alimkosoa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ambaye siku ya Jumatano alitowa wito wa kusitishwa mara moja kwa mashambulizi baada ya Iran kushambulia visima vya gesi vya Ras Laffan nchini Qatar. 

“Rais Macron hajasema chochote kuhusu mashambulizi ya tarehe 7 Machi yaliyofanywa Marekani na Israel dhidi ya maghala ya mafuta mjini Tehran. Lakini wasiwasi wake unatokana na majibu yote. Msiba huu!” Aliandika mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu.

Araghchi alirejela msimamo wa Tehran kwamba haitajizuwia kuchukuwa hatua yoyote endapo miundombinu yake itashambuliwa tena na kwamba vita vitamalizika tu pale suala la uharibifu wa maeneo yake ya kiraia litakaposhughulikiwa kikamilifu.

Bei za mafuta zimepanda kwa takribani asilimia 10 kwenye soko la dunia kutokana na vita hivyo.
 

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,310 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply