Mkuu wa jeshi la Iran atishia kulipiza kisasi mauaji ya Larijani

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Mwandishi RFA ,Imeandikwa: March 18, 2026 05:09 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Mkuu wa jeshi la Iran Amir Hatami ametishia kuanza kulipiza kisasi “madhubuti” kwa mauaji ya mkuu wa usalama Ali Larijani katika shambulio la anga la Israel.

Mkuu wa jeshi la Iran atishia kulipiza kisasi mauaji ya Larijani

.
Maelezo ya picha,Ali Larijani

Mkuu wa jeshi la Iran Amir Hatami ametishia kuanza kulipiza kisasi “madhubuti” kwa mauaji ya mkuu wa usalama Ali Larijani katika shambulio la anga la Israel.

“Kwa wakati na mahali mwafaka, jibu la uamuzi, la kuzuia, na la kujutia litatolewa kwa Marekani ya jinai na utawala wa Kizayuni wenye kiu ya umwagaji damu,” Hatami alisema katika taarifa yake.

Aliongeza kuwa Larijani na vifo vya “mashahidi wengine vitalipizwa kisasi”.

Walinzi wa Mapinduzi wa Iran, ambao ni tofauti na jeshi, wanasema tayari wamerusha makombora katikati mwa Israeli “kulipiza kisasi” kwa kifo cha Larijani, shirika la habari la AFP linaripoti.

Marekani na Israel dhidi ya Iran: Yaliotokea mapema leo hadi kufiki sasa

.

Haya ndiyo matukio ya hivi punde tunapoendelea kukuletea habari za moja kwa moja za vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran:

  • Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimethibitisha kuuawa kwa Ali Larijani, katibu mashuhuri wa Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran, katika shambulio la anga.
  • Larijani ndiye afisa mkuu zaidi kuuawa tangu Kiongozi Mkuu Ali Khamenei
  • Mkuu wa jeshi la Iran ameapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya Larijani kwa kutishia “jibu la maamuzi, la kuzuia na la kujutia”.
  • Walinzi wa Mapinduzi wa Iran, ambao ni tofauti na jeshi, wanasema tayari wamerusha makombora katikati mwa Israeli “kulipiza kisasi” kifo cha Larijani, AFP inaripoti.
  • Huko Israel, watu wawili wamekufa kufuatia shambulio la kombora la Iran huko Tel Aviv
  • Jeshi la Israel linaendelea kushambulia maeneo ya Hezbollah nchini Lebanon.
  • Wizara ya Afya ya Lebanon imesema takriban watu sita wameuawa na wengine 24 kujeruhiwa katika mashambulizi mawili ya Israel katikati mwa Beirut, AFP inaripoti.
  • Shirika la Umoja wa Mataifa linasema kuwa kombora lilipiga mtambo wa nyuklia wa Iran, lakini hakukuwa na uharibifu wowote.
  • Jeshi la Marekani limesema kuwa limeshambulia maeneo ya makombora ya Iran karibu na mlango wa bahari wa Hormuz
  • Naye Donald Trump ameikashifu Nato na washirika wengine, na kudai Marekani “haihitaji tena au kutamani” msaada wao katika vita vya Iran baada ya hapo awali kuwaomba msaada.

Katika picha: Matukio ya baada ya mashambulizi mabaya ya Iran huko Tel Aviv

Tunapata picha mpya kutoka Tel Aviv za uharibifu kutokana na mashambulizi ya Irani ambayo yalisababisha vifo vya takriban watu wawili.

.
Maelezo ya picha,Uharibifu kutokana na shambulio la kombora kwenye jengo katika kitongoji cha Tel Aviv cha Ramat Gan
.
Maelezo ya picha,Huduma za dharura zajibu uharibifu kutokana na shambulio la kombora la Iran huko Ramat Gan
.
Maelezo ya picha,Makombora yaliyorushwa kutoka Iran yanaonekana katika anga ya Tel Aviv

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

CantonaDigital
CantonaDigital

Listen Live Radio Fortune Africa
Ukweli Na Burudani.

-Be ready to be Impacted, Inspired & Empowered.

-Keep watching our Channels

Cantona Cast Television,

Fortune Television Network (FTN)

Donation
Paypal https://www.paypal.com/donate/?hosted_button_id=6EKXMLNW8W6A2&fbclid=IwY2xjawQxeChleHRuA2FlbQIxMABicmlkETFRdkNBRndpclRDQTB5bXZZc3J0YwZhcHBfaWQQMjIyMDM5MTc4ODIwMDg5MgABHq960uGsyU3ABRIBc2h-iXGhHATvuEqe55gFsQ-rDb0fT-Z7SIQ3TV8LnkpD_aem_ybU2SvBlvyqrVsS9NAczRw

An attitude determines an altitude.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025

5,451 posts
0 followers

Fediverse Followers


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply