Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph ,Imeandikwa: March 18, 2026 15:09 (EAT)



Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC) kinaendelea na operesheni dhidi ya shabaha za Marekani, Israeli na za kikandaPicha: Sobhan Farajvan/Pacific Press/Sipa USA/picture alliance
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran bado linapambana licha ya hasara kubwa. Muundo wao wa uongozi unasaidia kuendeleza mapambano, lakini wachambuzi wanaona ishara za shinikizo linaloongezeka ndani ya mfumo wa madaraka.
Siku kumi na nane baada ya Marekani na Israel kuanzisha mashambulizi dhidi ya Iran, yaliyomuua Kiongozi Mkuu Ali Khamenei katika saa za mwanzo za vita na kuwaangamiza pia viongozi wengine wa kisiasa na kijeshi, ilionekana kana kwamba kitovu cha madaraka cha Jamhuri ya Kiislamu kingekuwa kimeyumba vibaya.
“Hata hivyo, kadri wiki ya tatu ya vita inavyoanza, inaonekana tathmini hiyo haiendani na hali halisi. Muundo wa madaraka wa Iran umeweza kushinda mshtuko wa awali,” mchambuzi wa Mashariki ya Kati Habib Hosseini-Fard aliiambia DW.
Licha ya kupata mapigo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran (IRGC) linaendelea kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali dhidi ya Marekani, Israel na baadhi ya mataifa ya Kiarabu jirani. Wanategemea mfumo wa kamandi uliosambaa na uliounganishwa vyema.
Hali hiyo inaonekana kuendelea hata baada ya Israel kusema Jumanne kuwa imemuua Ali Larijani, katibu wa Baraza la Juu la Usalama wa Taifa la Iran, pamoja na kiongozi wa wanamgambo wa Basij Gholamreza Soleimani katika shambulizi lingine Jumatatu.
Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) ilisema Iran imefanya zaidi ya mashambulizi 300 dhidi ya Oman, Saudi Arabia, Israel, Jordan, Cyprus, Uturuki, Azerbaijan, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar, Iraq, Kuwait na Bahrain katika kipindi cha wiki mbili.
Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia ilisema ilidungua zaidi ya droni 60 katika anga yake tangu usiku wa manane, hali inayoonyesha ukubwa wa mzozo huo. Umoja wa Falme za Kiarabu pia uliripoti kifo cha mtu mmoja na majeruhi mwingine kutokana na mabaki ya makombora ya Iran yaliyoanguka.

Utawaka wa Iran umethibitisha kuuawa kwa Mkuu wa usalama wa Iran Ali Larijani (katikati) katika shambulio la Israel siku ya Jumapili.Picha: Iranian President’s Press Office/UPI Photo/IMAGO
Mfumo wa uongozi unaobadilika
Katika hali hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amekataa mazungumzo, akisema hakutakuwa na usitishaji wa vita iwapo Marekani na Israel wataendelea kushambulia maeneo ya Iran.
Inaonekana bado anaweza kutegemea mfumo imara wa kijeshi, huku IRGC ikiwa mhusika mkuu mwenye uwezo wa kujibu kwa kubadilika kulingana na hali.
Jeshi hilo lilianzishwa baada ya Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 kwa sababu watawala wapya hawakuamini jeshi la zamani la enzi za Shah. Lengo lake lilikuwa kuzuia mapinduzi ya kijeshi na kulinda itikadi ya dola.
Pamoja na jeshi la kawaida, IRGC sasa ni sehemu ya vikosi vya ulinzi vya Iran na iko chini ya kiongozi wa kisiasa na kidini wa taifa hilo, Kiongozi Mkuu Mojtaba Khamenei. Idadi ya wanajeshi wake inakadiriwa kufikia hadi 200,000.
Kwa mujibu wa Hosseini-Fard, katika miongo miwili iliyopita IRGC imebadilika kutoka taasisi yenye mfumo wa ngazi za juu hadi mtandao ulioenea, ambapo makamanda wa majimbo wana mamlaka makubwa ya kufanya operesheni hata bila amri ya moja kwa moja kutoka makao makuu.
Aliongeza kuwa kina cha kimkakati cha Iran na maghala ya makombora yaliyo chini ya ardhi vinaifanya isiwe rahisi kuharibu uwezo wake wa kijeshi kwa muda mfupi, hali inayoeleza kuendelea kwa mashambulizi licha ya madai ya Marekani kuwa imeharibu shabaha nyingi.
Marekani na Israel zimesema shabaha zaidi ya 15,000 tayari zimeshambuliwa kwa mashambulizi ya anga, lakini Iran bado inaendelea kushambulia miji ya Israel kwa makombora. Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad pia ulilengwa na droni na makombora mapema Jumanne. Mataifa ya Ghuba na usafirishaji katika Ghuba ya Uajemi pia yameathiriwa.
Kwa nini Iran bado ina uwezo wa kupigana
Mchambuzi wa siasa Reza Talebi anaonya dhidi ya kudhani kirahisi kwamba udhaifu wa dola unaweza kusababisha kuanguka kwa mfumo wa madaraka nchini Iran.
Anasema wahusika wenye misimamo ya kiitikadi ndani ya jeshi na vyombo vya usalama wamefungamana kwa karibu na uhai wa mfumo huo. Aidha, IRGC si tu jeshi bali pia inadhibiti miundombinu ya kiuchumi na kiitikadi ndani na nje ya Iran.
Hii inajumuisha Kikosi cha Quds kinachosimamia operesheni za nje ya nchi pamoja na makundi ya wanamgambo Mashariki ya Kati yanayounga mkono malengo ya Iran. Pia inadhibiti kampuni kubwa ya ujenzi ya Khatam-al-Anbia inayohusika na miradi mikubwa ya kimkakati.
Kwa mujibu wa Talebi, uhusiano huo wa karibu wa kisiasa, kiuchumi na kijeshi hufanya iwe vigumu kwa mfumo huo kuachia madaraka kwa haraka au kwa hiari. Ikiwa sehemu ya nje ya mfumo itadhoofika, hali hiyo inaweza kuongeza mvutano na migogoro ya ndani badala ya kusababisha kuanguka kwa ghafla.
Iwapo mfumo ungeporomoka kabisa, anaongeza, hali inaweza kufanana zaidi na migogoro ya Syria au Afghanistan badala ya mpito wa madaraka ulio wa utaratibu.

Muundo wa uongozi wa IRGC unafanya iwe vigumu kuuangusha kwa urahisi, na wachambuzi wanasema yumkini malengo ya Marekani na Israel kupelekea mabadiliko ya utawala hayatafanikiwa.Picha: Hamed Malekpour/Islamic Consultative Assembly News Agency/AP Photo/dpa/picture alliance
Kuanguka kamili hakutarajiwi
Talebi anaamini kuwa kuanguka kabisa kwa mfumo wa usalama wa Iran si lazima kuwa lengo la Marekani na Israel. Kwa mtazamo wa Israel, mfumo dhaifu lakini unaofanya kazi unaweza kuwa rahisi kutabirika kuliko ombwe la madaraka.
Kwa mujibu wa Hosseini-Fard, Marekani na Israel sasa zinaonekana kulenga kudhoofisha uwezo uliosalia wa kijeshi wa Iran na kufungua tena Mlango wa Hormuz, huku zikifanya mashambulizi maalum dhidi ya taasisi za usalama ili kuhamasisha maandamano ya ndani.
Hata hivyo, alisema uwezekano wa kusitishwa kwa mapigano au kuanguka kwa Walinzi wa Mapinduzi kwa sasa ni mdogo. Baada ya mshtuko wa awali, Iran iliongeza hali ya sintofahamu katika Mlango wa Hormuz, na kuongeza shinikizo kwa uchumi wa dunia.
Kwa mashambulizi dhidi ya miundombinu na vituo vya kijeshi katika eneo la Ghuba, mzozo huo unaendelea kupanuka.
“Uwezekano mkubwa ni kuendelea kwa vita — ama katika kiwango cha sasa au kwa kuongezeka zaidi,” alisema.
Iran yashambulia Israel na mataifa jirani ya Ghuba

Shambulizi la Marekani na Israel katika eneo la viwanda la Isfahan nchini Iran mnamo Machi 14, 2026Picha: UGC/AFP
Iran imejibu mauaji ya mmoja wa viongozi wake wakuu aliyeuawa katika shambulio la anga kwa mashambulizi dhidi ya majirani zake wa Ghuba na Israel kwa kutumia baadhi ya makombora yake ya kisasa ya kukwepa ulinzi wa anga.
Mashambulizi mapya yaliripotiwa mapema leo, katika mkoa mkubwa wa mashariki wa Saudi Arabia, ambao ni makazi ya visima vyake vingi vya mafuta, Kuwait, Bahrain, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.
Nchini Iran, kinu cha nyuklia cha Bushehr kililengwa kwa kombora lakini hakukuwa na majeraha wala uharibifu. Haya ni kulingana na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA baada ya kupokea ripoti kutoka Tehran.
Mkuu wa IAEA, Rafael Grossi, amesisitiza wito wake wa kujizuia zaidi wakati wa mzozo huo ili kuzuia hatari ya ajali ya nyuklia.
Zelensky na Starmer wahimiza uungwaji mkono zaidi Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ameziita Urusi na Iran kuwa ni nchi “ndugu katika chuki” akitafuta kuungwa mkono na Waziri Mkuu wa Uimgereza Keir Starmer.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (kushoto) akizungumza na waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer wakati wa mkutano mjini London mnamo Machi 17, 2026Picha: Suzanne Plunkett/AFP
Katika mazugnumzo yake na waziri mkuu wa Uingereza mjini London, Zelensky amewataka washirika wa Ukraine kutoisahau nchi yake, na akapendekeza kwamba Marekani na mataifa mengine yatumie teknolojia ya Ukraine ya kupambana na droni katika vita vya Mashariki ya Kati ambavyo pia vimeufufua uchumi wa Urusi baada ya Marekani kuiondolea vikwazo vya mafuta yake kwa muda katika juhudi za kupunguza shinikizo kwenye usambazaji wa kimataifa uliosababishwa na vita katika Mashariki ya Kati.
Kwa upande wake, Starmer amesema haikubaliki kamwe Putin kuwa ndiye anayefaidika na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
NRC: Mamia waliuawa na kujeruhiwa katika shambulizi la Kabul
Baraza la Wakimbizi la Norway NRC, limesema leo kuwa mamia ya watu waliuawa na kujeruhiwa katika shambulio la anga la wiki hii lililofanywa na Pakistan kwenye kliniki ya matibabu ya waraibu wa dawa za kulevya Kabul.

Uharibifu uliofanywa na shambulizi la droni katika nyumba ya makazi katika eneo la Sarah Gharghai area, huko Quetta, Pakistan, mnamo Machi 14, 2026Picha: Naseer Ahmed/REUTERS
Mkurugenzi wa NRC, nchini Afghanistan Jacopo Caridi, amesema shirika hilo lisilo la kiserikali lilikuwa na timu za maafisa wake katika eneo hilo muda mfupi baada ya mashambulizi hayo kusaidia katika juhudi za uokoaji.
Ameiambia AFP kwamba kutokana na kile walichokiona na kile walichojadiliana na wengine waliohusika katika juhudi za dharura za uokoaji, wanaweza kusema kuwa mamia ya watu waliuawa na kujeruhiwa.
Caridi alithibitisha kushambuliwa kwa kituo hicho cha matibabu na na kusema moja ya majengo yake lilichomwa na kuharibiwa kabisa.
Pia amesema kufikia jana asubuhi, vikosi vya uokoaji bado vilikuwa vinajaribu kutoa miili kutoka kwenye vifusi na kutafuta njia za kufikia sehemu za eneo hilo ambapo kuta ziliporomoka.
Uingereza na Rwanda mahakamani juu ya mkataba wa wahamiaji
Uingereza na Rwanda zitakutana katika Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi (PCA) huko The Hague kuanzia leo Jumatano, huku Kigali ikidai zaidi ya pauni milioni 100 kutoka kwa Uingereza .

Wahamiaji wanaojaribu kuvuka ujia wa bahari ya Atlantiki, waokolewa mnamo Juni 15, 2022Picha: Ben Stansall/AFP
Maafisa kutoka nchi hizo mbili watawasilisha kesi yao katika kikao cha siku tatu mbele ya mahakama hiyo ya kimataifa iliyoanzishwa mwaka 1899 kusuluhisha mizozo ya kimkataba kati ya mataifa.
Maafisa kutoka Rwanda watawasilisha kesi yao leo Jumatano, huku mawakili wa Uingereza wakijibu kesho Alhamisi. Pande zote mbili zitahitimisha uwasilishaji wao siku ya Ijumaa.
Jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo ya PCA litasimamia kesi hiyo na huenda likachukuwa miezi kadhaa kutoa uamuzi.
Tayari mataifa hayo mawili yako kwenye mvutano baada ya Uingereza kupunguza misaada kwa Rwanda, ikiituhumu kuwaunga mkono waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.