Miaka 4 baada ya kuifungia Urusi, FIFA na IOC zasalia kimya uvamizi wa Marekani Iran

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph Imechapishwa: March 11, 2026 07:14 (EAT)

Vocalize Pre-Player Loader

Miaka minne imepita tangu vyama vya michezo duniani vichukue hatua ya kuifungua Urusi kutokana na uvamizi wake nchini Ukraine, hata hivyo uvamizi wa Marekani na Israel kwa nchik ya Iran ukiibua maswali ya upendeleo kwa vyama hivyo.

Rais wa Marekani, Donald Trump akiwa kwenye picha na rais wa FIFA, Gianni Infantino.
Rais wa Marekani, Donald Trump akiwa kwenye picha na rais wa FIFA, Gianni Infantino. © Andrew Caballeros-Reynolds/AFP

Vita zote hizi zilizuka baada ya kumalizika kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi na kabla ya michezo ya watu wenye ulemavu na kuelekea michuano ya kombe la dunia ya wakati wa majira ya joto.

Urusi ilivamia Ukraine siku nne baada ya sherehe za kufungwa kwa michuano ya Beijing mwaka 2022.

Marekani na Israel zilianza kuishambulia Iran siku 6 baada kumalizika kwa michezo ya Olimpiki majira ya baridi huko Milan-Cortina nchini Italia.

Mwaka 2022, ilichukua siku 4 tu kwa shirikisho la soka duniani FIFA na lile la Ulaya UEFA wakiungwa mkono na kamati ya kimataifa ya Olimpiki, kuwafungia wanamichezo wa Urusi na Belarus.

IOC ililaani “ukiukwaji wa makubaliano ya Olimpiki na serikali ya Urusi na Belarusi ambayo iliiunga mkono Moscow kwenye vita ya Ukraine.”

Baadhi ya wafuatiliaji wa mambo wametathmini namna Urusi ilifungiwa na FIFA katika mashindano yake kufuatia uvamizi wake huko Ukraine, licha ya kuwa hakukuwa na majadiliano yaliyofanywa kama ambavyo yanafanyika na Marekani ambayo itakuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka huu.

Wakosoaji wanahoji kwanini mpaka sasa vyama vya michezo duniani havijaichukulia hatua Marekani na Israel kutokana na uvamizi wao huko Iran.

Kwa baadhi wanaona kuwa FIFA, UEFA na IOC zinaiogopa Marekani ambayo imekuwa na ushawishi mkubwa kwenye siasa za dunia, na hasa namna ilivyojitwika kwa uzuri jukumu la maandalizi ya fainali za kombe la dunia mwaka 2026.

Aidha urafiki wa rais Donald Trump na rais wa Fifa Gianni Infantino, ukiongeza muktadha wa kwanini shirikisho hilo limeshindwa kuchukua hatua, baadhi ya wakosoaji wakitaka Marekani kunayang’anywa uenyeji.

Safari Rally 2026: Naivasha yajiandaa kwa mbio kali zaidi kwenye kalenda ya WRC

Naivasha, Kenya – Naivasha itachangamka tena wiki hii mashabiki wa mbio za magari wakimiminika kushuhudia Safari Rally 2026, raundi ya tatu ya Mashindano ya Dunia ya Mbio za Magari (WRC). Jumla ya madereva 46 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano yanayojulikana kama mojawapo ya magumu na yanayochosha zaidi duniani.

Kenya inaandaa Safari Rally kwa mwaka wa sita mfululizo
Kenya inaandaa Safari Rally kwa mwaka wa sita mfululizo © WRC

Timu ya Toyota Gazoo Racing itaingia ikiwa na dhamira ya kuendeleza ubabe wake nchini Kenya baada ya kushinda matoleo sita mfululizo ya Safari Rally.

Mwaka jana ushindi ulienda kwa dereva wa Wales Elfyn Evans, ambaye pia tayari ameshinda raundi ya Sweden msimu huu. Raundi ya kwanza ya mwaka huu huko Monte Carlo ilinyakuliwa na Oliver Solberg.

Safari Rally 2026 Itafanyika Lini?

Mashabiki wakishuhudia gari likipita
Mashabiki wakishuhudia gari likipita © WRC

Mashindano yatafanyika kuanzia Alhamisi Machi 12 hadi Jumapili Machi 15, 2026, yakifanyika kikamilifu Naivasha tofauti na miaka ya nyuma ambapo kulikuwa na tukio maalum jijini Nairobi kabla ya mashindano rasmi kuanza.

Safari Rally ya mwaka huu itaanza kwa Shakedown katika hatua mpya ya Nawisa Alhamisi asubuhi. Baada ya hapo, magari yataelekea katika Taasisi ya Mafunzo ya Utafiti wa Wanyamapori (WRTI), ambayo ni kituo cha huduma (service park), kwa ajili ya sherehe ya uzinduzi rasmi saa tisa alasiri.

Siku ya kwanza mashabiki watashuhudia hatua mbili za mwanzo (Camp Moran na Mzabibu) kabla ya magari kurejea mapumziko ya usiku.

Umbali na Muundo wa Mashindano

Safari Rally 2026 itakuwa na jumla ya takribani kilomita 350 za mbio za ushindani, huku magari yakisafiri zaidi ya kilomita 843 za njia za usafiri kati ya hatua mbalimbali.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatar Norrbottens lanrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islands


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply