Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa
Na Cantona Joseph Imechapishwa: 01/03/2026



Taarifa kutoka Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, vyombo kadhaa vya habari vya serikali nchini Iran vimethibitisha kifo cha Ayatollah Khamenei.
Rais wa Marekani Donald Trump saa chache zilizopita alisema Kiongozi Mkuu huyo aliuawa wakati wa shambulio la pamoja na Israel katika maeneo kadhaa kote Iran.
Katika taarifa hiyo, haikutajwa ni jinsi gani Khamenei mwenye umri wa miaka 86 alivyofariki, au ni nani anayeweza kuchukua nafasi ya kiongozi.
Jamaa wa Khamenei pia wameuawa katika mashambulizi hayo
Hapo awali, vyombo vya habari vya serikali vilisema kwamba binti wa Khamenei, mkwewe na mjukuu wake pia waliuawa katika mashambulizi hayo.
Kulingana na Shirika la Habari la Fars, ambalo lina uhusiano na Kikosi cha Revolutionary Guard, kuna ripoti kwamba mmoja wa mabinti wa Khamenei ameuawa pia.
Katika picha: Hisia mseto nchini Iran huku mashambulizi yakiendelea
Hizi hapa ni baadhi ya picha kutoka ndani ya Iran tunapokaribia saa 24 tangu Israel na Marekani kuishambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati.






Rais na wengine wawili watasimamia kipindi cha mpito – Iran yatangaza

Iran imemtangaza kwamba rais wake, mkuu wa mahakama, na mmoja wa wanasheria wa Baraza la Walinzi – chombo chenye nguvu – watasimamia kipindi cha mpito kufuatia kifo cha Ayatollah Ali Khamenei.
Jopo la Wataalamu wa Uongozi – baraza la maulama – sasa litageukia linatarajiwa kumteua mrithi wa Khamenei, jambo ambalo katiba inasema lazima lifanyike haraka iwezekanavyo.
Kukufanyika kwa haraka kwa shughuli hiyokw wakati Iran inashambuliwa na Marekani na Israel kunaweza kuwa vigumu kutokana na sababu za kiusalama.
Khamenei mwenyewe aliteuliwa siku hiyo hiyo Ruhollah Ayatollah Khomeini alipokufa.
Moja kwa moja
Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi…

Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimethibitisha kwamba Kiongozi Mkuu Ali Khamenei ameuawa, katika mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran kutoka ambayo yalianza Jumamosi asubuhi (saa za ndani).
Haya hapa yaliyojiri kwa mukhtasari:
- Taarifa ya Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran, iliyosomwa vyombo kadhaa vya habari vya serikali, imethibitisha kuwa Ayatollah Khamenei aliuawa ofisini kwake mapema Jumamosi asubuhi.
- Mtangazaji mmoja, alisema nchi itaanza siku 40 za maombolezo huku akitokwa na machozi, .
- Zaidi ya watu 200 wameuawa wakati wa mashambulizi hayo, kulingana na shirika la Red Crescent, huku CBS News, mshirika wa habari wa BBC ikiripoti kuwa maafisa 40 wa Iran wameuawa.
- Kujibu mashamblizi hayo, Iran ilifanya msururu wa mashambulizi Mashariki ya Kati, hasa dhidi ya mataifa washirika wa Marekani na ambapo Marekani ina kambi za kijeshi, ikiwa ni pamoja na Dubai, Doha, Bahrain, na Kuwait.
- Uingereza inashiriki katika “operesheni zilizoratibiwa za ulinzi wa kikanda” kulinda raia wa Uingereza na washirika wa kikanda, Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer amesema.
- Rais Donald Trump hapo awali alisema Khamenei alikuwa “mmoja wa watu waovu zaidi katika historia” na kwamba kifo chake kilikuwa “fursa kubwa zaidi kwa Wairan kurujirudishia nchi yao”. Alisema Marekani itaendelea kuishambulia Iran kwa mabomu – huku milipuko ikiendelea kusikika katika mji mkuu wake Tehran.
- Marekani haiwezi kutangaza vita bila idhini ya bunge – na operesheni hii imegawanya wabunge, kwa kiasi kikubwa kulingana na vyama.
- Umoja wa Mataifa pia umesema operesheni hiyo ya kijeshi inadhoofisha amani katika eneo hilo.
Iran yaonya kuhusu ‘mashambulizi mabaya’
Tumepokea taarifa hivi punde kutoka kwa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ikionya kwamba watashambulia kambi za Marekani na Israel.
“Operesheni mbaya zaidi ya katika historia ya vikosi vya jeshi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaanza kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na vituo vya kigaidi vya Marekani muda mfupi ujao,” inasema.
Televisheni ya taifa ya Iran: Khamenei aliuawa ofisini kwake

Tukiangazia tena maelezo zaidi taarifa ya Baraza Kuu la Usalama la Iran, iliyosomwa kwenye vituo vya Televisheni vya serikali hapo awali.
Baraza hilo limesema kuwa Ayatollah Khamenei aliuawa mapema Jumamosi asubuhi katika ofisi yake “alipokuwa akitekeleza majukumu yake”.
Kwa kutumia picha za satelaiti, BBC Verify hapo awali ilithibitisha uharibifu mkubwa wa sehemu za Jumba la Uongozi, ambalo ni ofisi ya Khamenei mjini Tehran.
Shirika la Habari la Tasnim linalohusiana na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema kwamba kifo cha Khamenei ofisini mwake ni dhibitisho kwamba ripoti kwamba alikuwa akijificha zilikuwa “vita vya kisaikolojia vya adui”.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.