Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani
https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Na Cantona Joseph : February 28, 2026 05:50 (EAT)

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahamoud Ali Youssouf akihutubia huko mjini Addis Abbeba, EthiopiaPicha: Amanuel Sileshi/AP Photo/picture alliance
Umoja wa Afrika umetoa wito Jumamosi wa kupunguza mvutano baada ya Marekani na Israel kuishambulia Iran, na kuonya kwamba kwamba mgogoro huko Mashariki ya Kati unaweza kuwa na athari kwa watu wa bara hilo.
Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahamoud Ali Youssouf amezitaka pande zote kujizuia, kupunguza mvutano haraka na kuendelea na mchakato wa mazungumzo ya kina.
Mahamoud ameendelea kuwa kuongezeka kwa mgogoro huo kunaweza kuzidisha hali ya ukosefu wa utulivu duniani, pamoja na athari kubwa kwa masoko ya nishati, usalama wa chakula na ustawi wa kiuchumi hasa barani Afrika kunakoshuhudiwa mizozo na matatizo ya kiuchumi.
Pakistan: Tumewaua wanajeshi 331 wa Taliban huko Afghanistan

Wanajeshi wa Taliban wa Afganistan wakiwa katika mapambano na Pakistan huko NangarharPicha: REUTERS
Serikali ya Pakistan imesema Jumamosi kuwa imewaua wanajeshi 331 wa Taliban na kuharibu miundombinu na silaha kadhaa wakati wa mapigano mabaya zaidi ya mpakani na jirani yake Afghanistan.
Waziri wa Habari wa Pakistan Attaullah Tarar ametoa taarifa mpya kuhusu operesheni iliyopewa jina la “Ghazb lil Haq” inayoendelea na kusema pia kuwa zaidi ya wapiganaji 500 wa Taliban wa Afghanistan walijeruhiwa na maeneo 37 kote Afghanistan yalilengwa.
Mapigano makali kati ya Pakistan na Afghanistan yalizuka Alhamisi jioni katika eneo la mpakani mwa nchi nchi hizo mbili baada ya Islamad kuituhumu Kabul kuwahifadhi wanamgambo wa kundi la Taliban wa Kipakistan TPP wanaofanya mashambulizi ndani ya ardhi yake.
Marekani na Israel zaishambulia Iran ambayo pia imejibu

Moshi ukifuka kutokana na mashambulizi kadhaa ya Marekani na Israel mjini TehranPicha: Tasnim News Agency/ZUMA/picture alliance
Rais Donald Trump amesema Marekani imeanza “operesheni kubwa za kijeshi nchini Iran” baada ya Israel kufanya mashambulizi kadhaa katika Jamhuri hiyo ya Kiislamu.
Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti mashambulizi kote nchini humo. Miripuko kadhaa ya mabomu imesikika katika mji mkuu wa Iran huku shambulio la kwanza likiwa limefanyika karibu na ofisi za Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.
Haikubainika mara moja ikiwa Khamenei mwenye umri wa miaka 86 alikuwa ofisini mwake wakati wa mashambulizi hayo kwa kuwa hajaonekana hadharani kwa siku kadhaa tangu kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi yake na Marekani ambayo imepelekea meli na ndege za kivita huko Mashariki ya Kati.
Trump na Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamesema kuwa baada ya mashambulizi hayo, Wairan wanapaswa kuchukua hatma yao mikononi mwao. Hata hivyo serikali ya Tehran imesema rais Masoud Pezeshkian yuko hai na salama. Iran pia imejibu kwa kushambulia kambi za jesh la Marekani katika mataifa ya Qatar, Bahrain na Umoja wa Falme za kiarabu.
Mashambulizi haya yanafanyika wakati mazungumzo yalikuwa yakiendelea ili kujaribu kuishinikiza Iran kufikia makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia. Nchi jirani ya Iraq imetangaza kuifunga anga yake huku ving’ora vikisikika kote Israel baada ya jeshi la ulinzi IDF kutangaza kuwa mfululizo wa makombora yamefyetuliwa kuelekea Israel. Mashirika mbalimbali ya ndege yamesitisha safari zao huko Mashariki ya Kati.
UN yatahadharisha tabia ya kutumia mabavu kutatua mizozo

Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa Volker TurkPicha: DW
Mkuu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa amesema viongozi wamekuwa wakitumia madaraka vibaya na kutoa kipaumbele kwa matumizi ya nguvu kutatua mizozo, hali inayopelekea kuongezeka kwa idadi ya mizozo kote duniani.
Volker Turk ameliambia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hapo jana mjini Geneva kuwa kunashuhudiwa “mparaganyiko duniani” kufuatia kitendo cha kuchukulia kawaida matumizi ya nguvu, huku akitolea mifano mizozo ya Sudan, Ukraine na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu.
Turk amesema idadi ya migogoro inayohusisha silaha imeongezeka maradufu tangu mwaka 2010 na kufikia karibu migogoro 60, huku akitamatisha kuwa kwa sasa dunia inazidi kuwa eneo hatari zaidi.
Ghana: Raia wetu 55 waliuawa katika vita nchini Ukraine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Samuel Okudzeto Ablakwa akiwa na mwenzake wa Ukraine Andrii Sybiha mjini KievPicha: Tetiana Dzhafarova/AFP/Getty Images
Serikali ya Ghana imesema raia wake wapatao 55 wameripotiwa kuuawa katika vita nchini Ukraine, huku ikiahidi msako mkali dhidi ya wanaohusika na mipango haramu ya kuwarubuni na kuwasafirisha raia wa nchi hiyo hadi urusi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana Samuel Okudzeto Ablakwa alifanya ziara wiki hii mjini Kyiv kujadili kuhusu hatima ya Waghana wawili waliokamatwa kwenye mstari wa mbele wa vita.
Hii ni idadi inayoongezeka katika miezi ya hivi karibuni ambapo nchi kadhaa za Afrika ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda, Afrika Kusini, na Gambia, zimekuwa zikigundua kuwa raia wao walidanganywa kupewa ajira na mishahara minono na badala yake wakajikuta wamesajiliwa katika jeshi la Urusi, huku wengi wakiuawa au kukamatwa kwenye uwanja wa vita.
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026
afghanistan, africa, albania, algeria, America, american-samoa, andorra, angola, anguilla, antarctica, antigua-and-barbuda, argentina, armenia, aruba, arusha, australia, austria, azerbaijan, bahamas, bahrain, bangladesh, barbados, belarus, Belgium, belize, benin, bermuda, bhutan, bolivia, bosnia-and-herzegovina, botswana, Boukinafaso, brazil, brunei-darussalam, bulgaria, burkina-faso, burma, burundi, california, cambodia, cameroon, canada, cape-verde, cayman-islands, central-african-republic, Chad, chicago, chile, china, christmas-island, cocos-keeling-islands, colombia, comoros, congo, cook-islands, costa-rica, cote-divoire-ivory-coast, Croatia, cuba, cyprus, czech-republic, darsalaam, democratic-peoples-rep-north-korea, democratic-republic-of-the-congo-kinshasa, denmark, djibouti, dodoma, dominica, dominican-republic, dr-congo, dubai, east-timor-timor-leste, ecuador, egypt, egypty, el-salvador, england, equatorial-guinea, equitorial-guinea, eritrea, estonia, eswatini, ethiopia, falkland-islands, faroe-islands, federal-states-of-moldova, fiji, finland, Florida, france, french-guiana, french-polynesia, french-southern-territories, gabon, gaza, georgia, germany, ghana, gibraltar, goma, Greece, greenland, grenada, guadeloupe, guam, guatemala, guinea, guinea-bissau, guyana, habari, haiti, holy-see, honduras, hong-kong, houston, hungary, iceland, india, indonesia, Iowa, iran, iran-islamic-republic-of, iraq, ireland, israel, italia, italy, ivory-coast, jamaica, japan, jordan, karatu, kazakhstan, kilimanjaro, kinshasa, kiribati, kiswahili, korea, kosovo, kuwait, kyrgyzstan, lao, latvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourg, Lebanon, liberia, macau, madagascar, malawi, malaysia-maldives, Mali, malta, marshall-islands-martinique-mauritania-mauritius, massechutes, mayotte, mazingira, mbeya, meru, mexico, miami, micronesia, monaco-mongolia-montenegro, montserrat, morocco, mozambique-myanmar, mtwara, mwanza, namibia, nauru, nepal, netherlands, netherlands-antilles, nevada, new-caledonia, new-zealand, newyork, nicaragua, niger, nigeria, niue, north-macedonia, northern-mariana-islands, norway, oman, pakistan, palau, palestine, palestinian-territories, panama, papua-new-guinea, paraguay, peoples-democratic-republic, peru, philadhephia, philipians, Philippines, pitcairn-island, poland, politics, Portugal, puerto-rico, qatar, Norrbottens lan, republic-of-brazzaville, republic-of-south-korea, reunion-island, romania, Russia, russian-federation, rwanda, sahara-occidental, saint-kitts-and-nevis, saint-lucia, saint-vincent-and-the-grenadines, samoa, san-marino, sao-tome-and-principe, saudi-arabia, saudiarabia, scotland, Senegal, serbia, seychelles, sierra-leone, Singapore, singida, slovakia-slovak-republic, slovenia, solomon-islands, somalia, southafrica, spain, sri-lanka, sudan, suriname, swaziland-eswatini, sweden, switzerland, syria, syrian-arab-republic, tabora, taiwan-republic-of-china, tajikistan, tanzania, texas, thailand, the-gambia, tibet, timor-leste-east-timor, togo, tokelau, tonga, toronto, trinidad-and-tobago, tunisia, turkey, turkmenistan, turks-and-caicos-islands, tuvalu, uganda, united-arabs-emirates, united-kingdom, united-states, uruguay, uzbekistan, vancover, vanuatu, vatican-city-state-holy-see, venezuela, vietnam, virgin-islands-british, virgin-islands-u-s, wallis-and-futuna-islands
Discover more from cantonadigital
Subscribe to get the latest posts sent to your email.