Waziri Mkuu wa India alihutubia Bunge la Israel

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na Cantona Joseph Imechapishwa : February 26, 2026 13:35 (EAT)

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amelihutubia Bunge la Israel (Knesset) akiahidi ushirikiano, urafiki na heshima na taifa la Israel ambalo hadhi yake kimataifa imetiwa doa kutokana na vita vyake katika Ukanda wa Gaza.

Narendra Modi ambaye yuko ziarani huko Israel kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kibiashara na ulinzi, ameongeza pia kuwa India inasimama imara na Israel kufuatia shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023.

” Pia ninawasilisha salamu za rambirambi za dhati kutoka kwa watu wa India kwa kila maisha yaliyopotea na kwa kila familia ambayo iliathirika kufuatia shambulio la kigaidi la Hamas mnamo Oktoba 7, ” alisema Modi.

Waziri Mkuu huyo wa India alikutana na mwenzake wa Israel Benjamin Netanyahu, ziara ambayo imeibua ukosoaji mkali nchini India ambayo kihistoria imekuwa ikiwaunga mkono Wapalestina, lakini sasa kunashuhudiwa mabadiliko ya sera ya kigeni ya India chini ya uongozi wa Narendra Modi.

Papa Leo XIV kufanya ziara katika mataifa manne ya Afrika

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV akiwahutubia wauminiPicha: Alessandra Tarantino/AP Photo/picture alliance

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV anatarajia mwezi Aprili kufanya ziara katika mataifa manne ya Afrika ikiwa ni pamoja na Algeria, Cameroon, Angola na Guinea ya Ikweta.

Kiongozi huyo wa kidini atautembelea mji mkuu wa Algeria na eneo la Annaba kuanzia Aprili 13 hadi 15, ikiwa ni ziara ya kwanza katika taifa hilo la kiislamu la Afrika Kaskazini.

Akiwa huko Cameroon na Angola,  Papa Leo anatarajia kutoa wito wa amani  na mazungumzo ya kijamii kufuatia migogoro ya muda mrefu ya makundi yanayotaka kujitenga na mbayo yamekuwa yakisababisha vifo vya raia.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026

afghanistanafricaalbaniaalgeriaAmericaamerican-samoaandorraangolaanguillaantarcticaantigua-and-barbudaargentinaarmeniaarubaarushaaustraliaaustriaazerbaijanbahamasbahrainbangladeshbarbadosbelarusBelgiumbelizebeninbermudabhutanboliviabosnia-and-herzegovinabotswanaBoukinafasobrazilbrunei-darussalambulgariaburkina-fasoburmaburundicaliforniacambodiacamerooncanadacape-verdecayman-islandscentral-african-republicChadchicagochilechinachristmas-islandcocos-keeling-islandscolombiacomoroscongocook-islandscosta-ricacote-divoire-ivory-coastCroatiacubacyprusczech-republicdarsalaamdemocratic-peoples-rep-north-koreademocratic-republic-of-the-congo-kinshasadenmarkdjiboutidodomadominicadominican-republicdr-congodubaieast-timor-timor-lesteecuadoregyptegyptyel-salvadorenglandequatorial-guineaequitorial-guineaeritreaestoniaeswatiniethiopiafalkland-islandsfaroe-islandsfederal-states-of-moldovafijifinlandFloridafrancefrench-guianafrench-polynesiafrench-southern-territoriesgabongazageorgiagermanyghanagibraltargomaGreecegreenlandgrenadaguadeloupeguamguatemalaguineaguinea-bissauguyanahabarihaitiholy-seehondurashong-konghoustonhungaryicelandindiaindonesiaIowairaniran-islamic-republic-ofiraqirelandisraelitaliaitalyivory-coastjamaicajapanjordankaratukazakhstankilimanjarokinshasakiribatikiswahilikoreakosovokuwaitkyrgyzstanlaolatvia-lebanon-lesotho-liberia-libya-liechtenstein-lithuania-luxembourgLebanonliberiamacaumadagascarmalawimalaysia-maldivesMalimaltamarshall-islands-martinique-mauritania-mauritiusmassechutesmayottemazingirambeyamerumexicomiamimicronesiamonaco-mongolia-montenegromontserratmoroccomozambique-myanmarmtwaramwanzanamibianaurunepalnetherlandsnetherlands-antillesnevadanew-caledonianew-zealandnewyorknicaraguanigernigerianiuenorth-macedonianorthern-mariana-islandsnorwayomanpakistanpalaupalestinepalestinian-territoriespanamapapua-new-guineaparaguaypeoples-democratic-republicperuphiladhephiaphilipiansPhilippinespitcairn-islandpolandpoliticsPortugalpuerto-ricoqatarrepublic-ofrepublic-of-brazzavillerepublic-of-south-koreareunion-islandromaniaRussiarussian-federationrwandasahara-occidentalsaint-kitts-and-nevissaint-luciasaint-vincent-and-the-grenadinessamoasan-marinosao-tome-and-principesaudi-arabiasaudiarabiascotlandSenegalserbiaseychellessierra-leoneSingaporesingidaslovakia-slovak-republicsloveniasolomon-islandssomaliasouthafricaspainsri-lankasudansurinameswaziland-eswatiniswedenswitzerlandsyriasyrian-arab-republictaborataiwan-republic-of-chinatajikistantanzaniatexasthailandthe-gambiatibettimor-leste-east-timortogotokelautongatorontotrinidad-and-tobagotunisiaturkeyturkmenistanturks-and-caicos-islandstuvaluugandaunited-arabs-emiratesunited-kingdomunited-statesuruguayuzbekistanvancovervanuatuvatican-city-state-holy-seevenezuelavietnamvirgin-islands-britishvirgin-islands-u-swallis-and-futuna-islandswallis-and-futuna-islandswallis-et-futunawashington-dcwestern-saharayemenzambiazambiezimbabwe

Advertisement

Share this:


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply