UN yafichua majaribio ya mauaji dhidi ya viongozi ya Syria

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Kiongozi mpya wa Syria Ahmad al‑SharaaPicha: Syrian Presidency/Handout/Anadolu/picture alliance

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imefichua kuwa Rais wa Syria pamoja na mawaziri wawili wa serikali Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Mambo ya Nje—walilengwa katika majaribio matano ya mauaji yaliyoshindikana mwaka jana.

Matangazo

Ripoti hiyo iliyotolewa Jumatano na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres inaangazia kwa kina mazingira ya kiusalama nchini Syria na juhudi za makundi ya kigaidi kudhoofisha serikali mpya ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Rais Ahmad al‑Sharaa, Waziri wa Mambo ya Ndani Anas Hasan Khattab na Waziri wa Mambo ya Nje Asaad al‑Shibani walilengwa katika majaribio matano tofauti ya mauaji. Hata hivyo, hakuna shambulio lililofanikiwa.

Majaribio hayo ya mauaji yanadaiwa kufanywa na kundi linalojiita Saraya Ansar al‑Sunnah, ambalo linatajwa kuwa kibaraka wa kundi la Dola la Kiislamu IS.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa majaribio hayo ya mauaji ni ishara kwamba kundi la Dola la Kiislamu bado lina uwezo wa kupanga mashambulizi makubwa na lina nia ya kudhoofisha serikali mpya ya Syria kwa kutumia mianya ya kiusalama na mazingira ya kutokuwa na uhakika nchini humo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2026


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply