Polisi Tanzania yawaachilia viongozi wanne wa CHADEMA

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John HechePicha: CHADEMA

Polisi nchini Tanzania imewaachilia huru viongozi wanne wa chama kikuu cha upinzani chini humo CHADEMA waliokamatwa kwa madai ya kuratibu na kupanga maandamano ya vurugu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwezi uliopita, Hayo yamesemwa na chama hicho.

Miongoni mwa walioachiliwa kwa dhamana ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMAJohn Heche, ambaye alikamatwa Oktoba 22 na kuhojiwa kuhusu tuhuma za ugaidi, kulingana na wakili wake, na Amani Golugwa.

Maandamano yaliyotokea Oktoba 29 na baada yaliiingiza Tanzania katika mgogoro mkubwa zaidi wa kisiasa. Chama cha upinzani CHADEMA na baadhi ya wanaharakati wa haki za binadamu walisema zaidi ya watu 1,000 waliuawana vikosi vya usalama wakati vilipojaribu kuwadhibiti waandamanaji.

Hata hivyo, serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo kwa karibu asilimia 98 ya kura, ilikanusha idadi hiyo ya watu lakini bila kutoa takwimu kamili.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a comment