Mawaziri wa nishati wa Marekani na Ulaya wakutana Ugiriki.

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Mawaziri wa Marekani wamekutana na waziri mkuu wa Ugiriki mjini Athens kujadili masuala ya nsiahti kwa ajili ya Ukraine.Picha: Louiza Vradi/REUTERS

Mawaziri wa nishati kutoka Marekani na nchi za Ulaya wamkutana mjini Athens, Ugiriki kujaribu kutafuta njia ya kuisadia Ukraine katika usambazaji wa gesi ili kukabiliana na msimu mkali wa baridi.

Mawaziri wa nishati kutoka Marekani na nchi za Ulaya wamefanya mazungumzo jana Alhamisi nchini Ugiriki kuhusu jinsi ya kutumia mtandao mpya wa mabomba ya kikanda ulioboreshwa ili kuisambazia vyema nishati Ukraine iliyoharibiwa na vita huku utawala wa Trump ukitaka kuongeza zaidi mauzo ya nje ya gesi kwenda Ulaya.

Waziri wa nishati wa Marekani Chris Wright na waziri wa mambo ya ndani Doug Burgum walikuwa wakihudhuria mkutano huo mjini Athens, ulioandaliwa na Baraza la Atlantiki, shirika la kutoa maoni ya kitaalamu lenye makao yake makuu mjini Washington.

Walijiunga na zaidi ya maafisa 80 wa Marekani, mawaziri wa nishati wa Umoja wa Ulaya, na watendaji kutoka kwa makampuni yanayoongoza ya gesi asilia ya Marekani iliyoyeyushwa.

Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis alisema jana jioni kwamba Ugiriki imebarikiwa na eneo la kipekee sana la kijiografia, na ndio kiingilio cha asili cha gesi asilia iliyoyeyushwa ya Marekani kuingia Ulaya.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply