Urusi na Ukraine zaendelea kushambuliana kwa makombora

Radio Fortune Africa -Ukweli na Burudani

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

Vocalize Pre-Player Loader

Na : Cantona Joseph|RFA

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy na mwenzake wa Urusi Vladmir PutinPicha: Mandel Ngan/Andrew Caballero-Reynolds/AFP

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Telegraph na mkuu wa kijeshi wa mji wa Kyiv, Timur Tkachenko, mashambulizi hayo ya Urusi yalisababisha moto mkubwa uliotanda katika sehemu kubwa ya mji huo.

Maafisa nchini Ukraine wamesema leo Jumatano kwamba mashambulizi ya makombora na droni yaliyofanywa na Urusi nchini humo yamewaua watu sita na kusababisha kukatika kwa umeme nchini kote. 

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Telegraph na mkuu wa kijeshi wa mji wa Kyiv, Timur Tkachenko, mashambulizi hayo ya Urusi yalisababisha moto mkubwa uliotanda katika sehemu kubwa ya mji huo. 

Katika upande mwingine, Ukraine nayo imesema imefanikiwa kukishambulia kiwanda cha kemikali cha Bryansk nchini Urusi, ingawa haikuelezwa ni kwa kiwango gani shambulizi hilo limefanya uharibifu.

Mashambulizi haya yanajiri wakati mkutano wa kuutatua mzozo huo kati ya Rais Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin ukisititishwa kwa muda baada ya Urusi kutupilia mbali pendekezo la kusitisha mapingano. Hata hivyo Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban amesema maandalizi ya mkutano huo yanaendelea.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply