Kesi ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu yazuiwa kurushwa mubashara,Na Humphrey Mgonja

Radio Fortune Africa -Na Cantona Joseph

https://zeno.fm/radio/radio-fortune-africa

h

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, imezuiwa kurushwa mubashara au kuchapishwa taarifa za ushahidi baada ya Mahakama kutoa agizo maalum la kulinda mashahidi wa siri wa kiraia.

Akisoma uamuzi huo leo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Franko Kiswaga, amesema zuio hilo limetolewa kwa mujibu wa maelekezo ya Mahakama Kuu. Ameeleza kuwa taarifa za mwenendo wa shauri hilo zitasomewa mahakamani hadharani, lakini utambulisho wa mashahidi wa siri utafichwa.

Hakimu Kiswaga pia ameiagiza Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuhariri taarifa za uwasilishaji wa shauri hilo ili kuhakikisha majina na maelezo yanayoweza kumtambulisha shahidi hayatajwe. Ameongeza kuwa mtu yeyote ikiwemo vyombo vya habari atakayetaka kuchapisha taarifa zinazohusu mashahidi atalazimika kupata kibali maalum, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya atakayekiuka.

Katika hatua ya leo, Lissu atasomewa taarifa za mwenendo wa upelekeaji shauri hilo Mahakama Kuu, bila kuhitajika kujibu chochote kwa sasa.

Hata hivyo, nje ya mwenendo wa shauri, viongozi wa Chadema wamelalamikia utaratibu wa ulinzi wa mahakama, wakidai kuwa kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliovaa kiraia ndani ya chumba cha mahakama ambao wanaamini ni askari polisi.

Lissu anakabiliwa na mashtaka ya uhaini ambayo, endapo atatiwa hatiani, adhabu yake ni hukumu ya kifo. Mpaka sasa amekaa rumande kwa zaidi ya miezi mitatu akisubiri mwenendo wa shauri kupelekwa Mahakama Kuu

Jeshi la Sudan linawatesa watu hadi kufa – Shirika la kutetea haki za binadamu

.

Shirika maarufu la kutetea haki za binadamu nchini Sudan limeshutumu jeshi la nchi hiyo na vikosi vya usalama kwa kuwatesa watu hadi kuwaua pamoja na kuwa na “vyumba vya kufanya mauaji”.

Kundi la Wanasheria wa Dharura lilisema lina taarifa za mamia ya watu waliokamatwa katika mji mkuu Khartoum.

Ilisema kuwa katika hali mbaya zaidi, baadhi ya walioshikiliwa baadaye walipatikana wakiwa wamekufa na ushahidi unaonyesha waliteswa.

Jeshi la Sudan liliuteka tena mji huo kutoka kwa wanajeshi wa Rapid Support Forces (RSF) mnamo mwezi Machi, ambapo wanapigana vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimeua makumi ya maelfu katika kipindi cha miaka miwili.

Jeshi halikujibu ombi la BBC la kutoa maoni yake siku ya Jumapili.

Myanmar inayokumbwa na vita kufanya uchaguzi mkuu wa kwanza tangu mapinduzi ya 2021

.

Myanmar itaanza uchaguzi wake mkuu mnamo mwezi Desemba 28, serikali yake ya kijeshi ilitangaza, katika kura ya maoni ambayo wengi wameishutumu wakisema ni kisingizio na itatumika kuongeza muda wa serikali ya kijeshi madarakani.

Hii itakuwa kura ya kwanza tangu serikali ya kijeshi kuchukua madaraka katika mapinduzi ya umwagaji damu mnamo 2021, na kumtia gerezani kiongozi aliyechaguliwa kidemokrasia Aung San Sung Kyi.

Myanmar imetumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe huku kukiwa na mapigano makali kati ya wanajeshi na makundi ya kikabila yenye silaha, ambao wengi wao wamesema hawataruhusu upigaji kura katika maeneo yao.

Mipango ya awali ya kufanya uchaguzi ilicheleweshwa mara kwa mara huku jeshi likijitahidi kuzuia uasi wa upinzani ambao umepata udhibiti wa sehemu kubwa ya nchi na hilo litafanya uchaguzi huu kuwa zoezi gumu kwa watawala wa kijeshi wa nchi hiyo.

Lakini kiongozi Min Aung Hlaing, ambaye aliongoza mapinduzi mabaya miaka minne na nusu iliyopita, amesema ni lazima upigaji kura uendelee, na ametishia adhabu kali kwa yeyote atakayekosoa au kukwamisha uchaguzi huo.

All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025


Discover more from cantonadigital

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply